Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Screenshot_20211219-214639.jpg
 
Wakati mwingine inatokea tu pale ambapo unataka ushushwe sehemu ambayo gari haitakiwi kushusha abiria. Mimi kuna siku niliwahi waomba Rungwe wanishushe Eso badala ya kwenda hadi Stendi Kuu wakaniambia pale hawaruhusiwi kushusha labda nikae mlangoni then watapunguza tu speed kidogo ili nishuke.

Na kweli walivyofika wakapunguza speed huyo nikaruka zangu wakatambaa uzuri sikuwa na mizigo nilikuwa na begi moja tu la mgongoni ndiyo maana hata nao walikubali vinginevyo ukiwa na mizigo hawakubali kukushusha sehemu kama hiyo maana hekaheka za kushusha mizigo yako inabidi gari isimame kabisa.

Sasa kwenye hizi daladala za mjini ndiyo kabisa imekuwa kama mazoea abiria kuomba kushushwa sehemu zisizoruhusiwa tena unaweza kuta ndiyo wengi kuliko hata wanaoshukia kwenye vituo rasmi. Watu tumeruka hadi kwenye treni ile ya mjini Gerezani-Pugu ambayo kuteleza na kukanyagwa mguu ni dakika sifuri sembuse magari.

Mdogo wangu umeshindikana
Unaruka kwenye magari??

Mimi bado sijajaribu huo mchezo.
 
Back
Top Bottom