Selfika na JF: Snap it. Show it

X wangu nae ananitisha, video zangu eti atavujisha.. AAaaah
😂😂😂
Ye ana movie X anayo picha
Asubutu kuvujisha azalilike yeye

Huyu kijana jaman
Haimbagi kwa stress, style yake is the best...

Hee mbona kama nimeweka vina, Depal nisindikize studio kesho, nahisi nina kipaji na mimi🤣🤣
 
Safari ni fupi Sana...

Msichana alikuwa amekaa kwenye Bus, iliposimama akaingia mama akakaa karibu naye. Mama akawa anamfinya na kumsukuma yule msichana kwa mikoba yake mikubwa, Bwana mmoja akaona yanayotendeka, kwa hasira akamuuliza Msichana, kwanini hasemi kitu kwa yale anayofanyiwa na huyo mama?

Binti akajibu akitabasamu "Sio lazima niwe mkali na kuzungumzia kila kitu. "Safari ni fupi sana" na nitateremka kwenye kituo kinachofuata"

Haya maneno "Safari ni fupi sana" yanafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, maana tukijua
kuwa safari yetu hapa duniani ni fupi, na kwamba kituo cha "kushuka" kipo usoni, basi hakuna haja ya kudhulumu, kutesa, kuonea wengine, kutambia mali au madaraka, kutosamehe wengine, kuwa na tabia mbaya, kupuuza kusali, kuwa mkarimu na kukosa shukuru kwa mema mengi tunayotendewa.

Je, kuna mtu ameuvunja Moyo wako? Kuwa Mtulivu "Safari ni fupi"

Je, kuna mtu alikudharau, akakudanganya? Kuwa Mtulivu "Safari ni fupi"

Umedhulumiwa, kuporwa, kuonewa? Usihamaki. "safari ni fupi"

Wamesahau wema wako? Wamekukimbia au kufukuzwa? Wanakudharau? Kuwa Mtulivu "Safari ni fupi"

Tujaze nyoyo zetu, Utu wema, ukarimu, haki, upole, huruma, upendo, shukrani, hofu MUNGU na kuwatendea wengine mema.
Kumbuka,_*"Safari ni Fupi".*
Tusisahau hilo Wapendwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…