Nilikuwa kwenye halaiki Yesu alipokufa
Nikamuona alivyoning'inia mwokozi wangu
Nikaiona taji ya miiba
Na vijito vya damu yake
Huyu ndiye tabibu wetu
Sasa mmemfanyia nini?
Nikajitosa miguuni na kwa hasira nikaita,
Ni nani kamtundika hapo juu
Mtoto wa amani,
Ni nani kamtundika hapo juu
Jitokeze unikabili,
Ni nani kamtundika hapo
Na halaiki ikanichekelea,
Nikageuka nikaiona nyundo
Nyundo mkononi mwangu