Kila mwanaume 1 anaporudi nyumbani, anaenda kuipa matumaini familia yake, hata kama hana senti tano! Uwepo wake na tabasamu na kurudi kwake, kunainong'oneza familia "IPO KESHO....KUNA MAISHA BADO....TUNA ULINZI WA KUTOSHA. BADO LIPO TUMAINI.."
_
Mwanaume anatembea na mengi sana kichwani na moyo wake, na hawezi kuyasema, kama wanaume wangelikuwa wanawaeleza wake zao namna wanavyopambana kwa ajili ya familia zao, wanawake wangelikufa kwa mshtuko.
Si ajabu ndiyo maana wanaume tunakufa mapema, maana tunauawa na mengi!....