Hahahaaa halafu nimekumbuka kuna siku tulienda sehemu fulani mie na rafiki yangu wanaongea lugha hatuielewi.
Sie tulienda zetu kujizururia tu sasa wakati tunavuka barabara akapita jamaa mmoja speed na baiskeli yaani alitukosakosa ilibaki kidogo atugonge.
Sasa akatuongelesha maneno kwa ile lugha yao hatukuelewa yule rafiki yangu akadakia kwa nguvu "MWENYEWE" pale barabarani mbele za watu haki nilicheka.