Selfika na JF: Snap it. Show it

Usiseme Kwa nguvu ndo linaanza anza 😂😂lisije likaghair nikabaki na tungumi kma zamani
Hapo ndio limeanzaaa litazidi kuongezeka haliwezi rudi kirahisi... Shikilia hapohapo Usiachieee 👌!
 
Gushepu dear penz na hta nikitaka lianze jipya kilawiki inawezekana tu ni suala la maamuzi😂😂😂😂
Wacha wee!! watu na nyota zenyuuuuu 👌👌👌! Enjoy mamaa Maisha Ndio hayahayaaaaaa!!!
 
Wee hio ya bamia ndio ikije mamy??
Mahitaji
🍃Bamia kumi (10)
🍃Mafuta ya maji (African Black castor oil au coconut oil au olive oil)
🍃Juice ya Tangawizi
🍃Asali

Jinsi ya kuandaa
🌿Osha bamia zako vizuri kuondoa uchafu wote
🌿unaweza kukata kata kuwa vipande vidogo vidogo au ukamenya tu (kuexpose undani wake)
🌿Weka kwenye sufuria yako safi
🌿Ongeza maji kiasi (kikombe kimoja au viwili vinatosha) na ufunike
🌿Chemsha kwa dakika 10 hadi 15 mpaka ile gelly au ute wa bamia uwe umetoka wa kutosha
🌿Epua na uache ipoe kwa dakika kadhaa
🌿Baada ya hapo chuja kuondoa vipeke na upate gelly tuu

Kama unatengeneza steaming
🌿chukua ute ulioupata gawanya mara mbili
🌿Nusu ya kwanza changanya na tangawizi na asali na mafuta yoyote ya kimiminika (hasa Castor oil)
🌿Baada ya kuosha nywele kwa shampoo (hakikisha nywele zako ni safi) paka mchanganyiko kwenye nywele zote
🌿Vaa shower cap au steamer na ukae kwa dakika 30+
🌿Osha kwa maji mengi
🌿Chukua ule mchanganyiko uliobaki changanya na mafuta kijiko kimoja hapa utakua umepata (Leave in Conditioner)
🌿Nywele zako zikiwa mbichi na safi pakaa vizuri kuanzia kwenye ngozi hadi kwenye ncha.
🌿Chambua vizuri nywele zako kidodgo kidogo kuhakikisha imeingia vizuri kwenywe nywele zote.
🌿Unaweza kusuka mabutu (bantu knots) au twists za njia mbili au tatu au nywele za mistari kawaida nywele lazima ziwe na unyevu kabisa.
🌿Ukiona zinakauka unanyunyiza maji tena.
🌿Ukimaliza acha zikauke vizuri utaendelea kupaka mafuta yako kama kawaida ili kuzifanya zing’ae.
🌿Ukifumua unapata mawimbi mazuri unaweza kubana utakavyo nywele zako.
 
Asante dear nitafanya hivo nione!! Shukrani sana!!
 
Kwa sisi nywele kavu ni nzuri hii??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…