Selfika na JF: Snap it. Show it

Yaani sio tu kuwa hao wachungaji %80 wameacha kufundisha mpendwa,bali hawaelewi kabisaaa!
Ndo maana makanisani watu wanaingia na kutoka km walivyo no changes,kitu ambacho sio sawa!
 
Yaani sio tu kuwa hao wachungaji %80 wameacha kufundisha mpendwa,bali hawaelewi kabisaaa!
Ndo maana makanisani watu wanaingia na kutoka km walivyo no changes,kitu ambacho sio sawa!
Mkuu sio kwamba mafundisho ya kweli hayapo, bali kwa sababu ya watu waliowengi kupenda miujiza ndio maana kuna baadhi ya mitume na manabii wa uongo (kama ilivyoandikwa) wanatumia huo mwanya kuvuna washirika. Watu
Wachache sana wamejaa neno ambao wana uwezo wa kuzipima roho za hao manabii wa uongo.
Mimi siwezi kuabudu sehemu ambayo haina mafundisho ya kweli.
Yani mtu na akili zako ukaanze kukanyaga chumvi?
 
But Kwenye fundisho la kuzijaribu hizo roho pana moto hapo.. Kwanini Henoko ( Enoch ) hata walichomoa kuingiza nyaraka zake ? Kuna Level ya kiroho mtu akifikia ili kuitest spirit yake kuna mawili au zaidi, uwe juu yake kiroho au muwe sawa kiroho tofauti na hapo unaweza hisi anatumika na mapepo.. Kama mnatembea kwenye realms tofauti kupambanua roho ya mtu ni kazi sana, cha msingi ni kumsikiliza Roho Mtakatifu ana guide wapi.. Kuna watu wanatembea katika dimension za juu sana, unakuta hata mtembeo wake na Mungu unaweza kukuchanganya ni kama Henoko ilivyokuwa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.
 
Umesema kweli. Kukiwa na semina ya Neno la Mungu (kujifunza tu neno la Mungu) watu hata hawaji. Tangaza sasa kuna maombi na maombezi. Au Ile tu semina; muda wa neno watu hata hawajali; ufike muda wa maombi sasa afu waambiwe Mtumishi atamuombea mtu mmoja mmoja weeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sahihi kabisa, ila hawa manabii wa kibongo yani kama uko vizuri kiroho ni rahisi sana kuzijua nia zao.
 
Watu wanapenda sana miujiza. Ndio maana kuna wachungaji fake wanatengeneza shuhuda za uongo iki kupata attention ya washirika wao.
Kwenye masuala ya kiroho hakuna kitu kizuri kama kujaa neno, huwezi yumbishwa na kitu chochote.
Watu wanaabudu wanadamu bila kujua.
 
But tuna kazi ya kufanya. Kama wapendwa hatutorudi msalabani ni ngumu kuona 100% ya undiluted power of God .
Sanaaa tena tuna kazi kubwa!
Leo tu nimetoka kumsikiliza baba angu Mwalimu,anasema kanisa limemfungia RM nje,halitaki udhihirisho wa nguvu za Mungu, eti wanasema wana utaratibu wao na misingi yao isije ikaharibika, matokeo yake watu wana shida wanai gia na kutoka na shida zao!
Mapokeo ndo yamekua kipaumbele!

But Yesu yuko malangoni,uamsho mkubwa unakuja tutaelewana tu!
 
Najua watakaokuelewa ni wachache sana
 

Asante Baba Mchungaji...

Wachungaji wa siku hizi hawa manabii na mitume wengi wamejikita kwenye injili ya utajirisho (prosperity gospel) na ni nadra sana kusikia tena nguvu ya msalaba wala damu ya Yesu dhidi ya dhambi za mwanadamu. Makanisa mengi sasa yamegeuka na kuwa ofisi za wanasaikolojia ambako watu wanakwenda kupunguziwa mizigo yao japo kwa muda tu ili wajisikie vizuri. Permanent baby Christians. Ukiwahubiria mambo magumu ya kutubu dhambi, kujikana nafsi na kujitwisha msalaba wa Yesu kila siku wanakukimbia. Ndiyo maana wanasaikolojia hawa wa kiroho kama Joel Osteen wamefanikiwa sana.

Tusiwalaumu. Labda ndiyo maono yao waliyopewa. Bila shaka utakaporudi Ethiopia utasimama katika kweli na kuihubiri injili ya kweli ngumu - injili ya nguvu ya msalaba na damu ya Yesu katika kutuondolea dhambi. Unayo kazi nzito mbele yako. Jiandae vizuri ewe Jemedari wa Bwana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…