Selelii: Rostam ni mmiliki wa Dowans, Richmond

Selelii: Rostam ni mmiliki wa Dowans, Richmond

Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni: Kamati ya Bunge... ya watUNGA SHERIA WANATUMIA USHAHIDI YA KUAMBIWA MITAANI ... eEE MUNGU... NIEPUSHE NA MAUPUUZI KAMA HAYA.
 
Tunaposema Tanzania ipo utumwani ni wachache tu wanalielewa hili.
Anayeweza kuhakikishia jamvi hili kuwa tuna serikali aseme hapa!
Nchi ipo utumwani zaidi ya ule wa Babel waliowekwa waisrael kwa zaidi ya miaka 40.
Nasi pia imevuka miaka 40, hatuna 'taifa', tupo chini ya milki ya 'waajemi wa wairan'.
Dawa ya hali hii ni moja tu! Mageuzi thabiti kama ya Zbar -1964, kupambana na kuung'oa usultani wa RA uliteka mamlaka ya nchi na uhai wa taifa, ndipo tutangaze Uhuru kamili maana in real sense 'Not Yet Uhuru' hapa TZ! Tutasubiri malaika waje watutoe utumwani humu? kamwe! maana hata viongozi hawajitambui, style ya wale 'manamba' wa enzi. Free Mansons via RA wamewateka akili na utashi, wamekwisha kazi.
 
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni: Kamati ya Bunge... ya watUNGA SHERIA WANATUMIA USHAHIDI YA KUAMBIWA MITAANI ... eEE MUNGU... NIEPUSHE NA MAUPUUZI KAMA HAYA.

Hajasema wa mitaani, amesema "walioambiwa"... Ungeliuliza kwanza iwapo huo ushahidi waliambiwa under oath au laa, "upuuzi" natumai ungelipungua zaidi!!
 
Rahaaaaaaaaaa!!!!!!!! Utamuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!Rahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!! acha bwana, hapa ni patamu sana. Kama vile unakaribia kulenga kuachia kitu

Watanzania wa hivi wako wengi, wengine wanamachungu, hasira na ghadhabu juu ya mafisadi, wengine wanasikia utamu na raha kama ya ....! Nchi hii mwenyewe alisha kufa 14/10/1999 tuliobaki ni wahamiaji! Tungekuwa wana wa nchi hii, tungefanya kama Tunisia!
 
Salva Rweyemamu kesho akiamka anatuma email kwenye vyombo vya habari kukanusha!

atasema Selelii ni kizabin zabina, mtu hatari, muongo, mdebwedo just as usual atatumia lugha za mitaani na kukanusha open issue kama hii
bcoz yy ndie mfaidika na ufisadi as well
 
Natoa hoja: wananchi nchi nzima tuandamane na kuitaka serikali imchunguze na kumchukulia hatua kali rostam aziz.
 
Tangu lini ukaona mwenye pesa akachukuliwa hatua Tanzania??, hili jambo sasa liwe katika mikono ya wananchi wenyewe maana hao viongozi wetu na justice system ni marehemu. THEY DON'T EXIST!!. I do not condone what happened in Tunisia (deaths), but i support the efforts made and i can see it calling here in TZ!!
 
Ukweli umejulikana. Sasa ni muda muafaka wa kuacha kumjadili RA badala yake 2je na hoja za jinsi gani 2zuie hayo mapesa yasilipwe kwa huyo muiran na rafiki zake wanaoihujumu nchi. French revolution iliwezekana,why not bongo? Lets kam with majibu....,
 
So what? kama ulijua hivyo ulishindwa vipi kushawisha wenzio kuiwajibisha serikali mlipokuwa mjengoni? Wewe, Sitta ah mnanichefua tu. Sasa uko nje utafanya nn. Mjengo wa gharama na kifahari yanayotoka mjengoni SIFURI.
 
Wanazidi kuumbuana wenyewe kwa wenyewe. Jamani jamani,ngoja tuu safari hii baada ya Lucas Seleli ,Samuel Sitta na Tido Mhando kuondolewa kwenye nyadhifa zao za awali sasa ni zamu ya Dr.Hosea na Salva Rweyemamu(mzee wa kukanusha ukweli).

Wanafanya juu chini wawalipe Dowans kabla ya bunge kuanza na bunge likianza moto utawaka nasikitika kuna watu watapoteza heshima zao wakiwemo Anne Makinda na wengineo na italeta mpasuko mkubwa CCM.
 
Hakika kama kuna watu nilowahi kuwapenda wakiwa bungeni basi mstaafu kwa njia ya mizengwe selelii nimekukumbuka sana,umepotea utazani ulikwisha toweka duniani?Jamani mwanamageuzi wangu nakukumbuka sana,pamoja na kwamba ulifanyiwa mizengwe usirudi je?wanamageuzi wenzako kama sitta japo huja kukuona?jitokeze mzee japo kauli yako yatosha juu ya huu ukandamizaji haki kwa wapinzani,binafsi waelewa umafia wa ccm na yote ulotendewa,yatosha kuyasamehe na wananchi na mungu wetu sote atakulipa!...kwa ubaya na uzuri
 
Kumbe mnajua RA ndiye mmiliki wa Dowans,sasa kelele mnazopiga dhidi ya viongozi wa nchi zinatoka wapi wakati RA si kiongozi wa TZ?


....Alitiliwa Majalo na Nani hadi Akaweza Kutufunga Watanzania Baola Kisigino??? Mkuu, Upo Uwanjani halafu Huangalii Mpira Wenyewe..?????:A S 39:
 
Akizunguma na Kituo cha Redio cha Zenji FM, 96.8 cha Zanzibar katika kipindi maarufu cha ‘Mwangaza wa Habari’, Selelii ameeleza kuwa aliambiwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz anahusika na Kampuni ya Richmond na pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Caspian, na hili kamati teule tuliambiwa na mwandishi wa habari aliyebobea, ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu bwana Salva Rweyemamu,” alisisitiza Selelii.

“Ushahidi mwingine tulioambiwa kamati teule ya Bunge kwamba mmiliki wa Kampuni ya Richmond ndiye mmiliki wa Kampuni ya Caspian,ni mfanyakazi wake mwenyewe(Rostam),ambaye alithibitisha kwamba mawasiliano yote ya Dowans yalikuwa yakipitia katika kampuni ya Caspian”, alithibisha Selelii.

“Mtu mwingine ambaye alituthibitishia kwamba Kampuni ya Richmond na Dowans ni kitu kile kile,ni mtoto wa mwanasheria maarufu sana nchini aliyekuwa akiitwa Mukaddas, ambaye ndiye aliyesaidia hata kupata nyumba ambayo walipanga, ambaye yeye ndiye alikuwa akilipia pango ya nyumba hiyo,kuanzia wakati wa Richmond na baadaye Dowans” alisema.
Sasa ile siri mliyoficha ili serikali isiporomoke yote kama alivyosema Mwakyembe ni ipi? Au mtaitoa mwaka 2015 baada ya jamaa kumaliza ngwe yake?
 
Hatimaye CCM kimemlipa mtu waliyedai kutokumfahamu huko Dowans; mhhhh, dunia hii!!!!!!!!!! He watu tukakisubiri hii CCM kule kwenye sanduku la kura 2015.
 
Back
Top Bottom