Mzee Mwanakijiji,
Kama hujui majibu wacha mimi nikusaidie kujibu; kama una majibu ila unamtega Dr basi ulegee!
a. Hakuna chombo kinachotenda haki Tanzania, sio kamati ya Richmond, sio Lowassa, sio JK, sio katibu wangu wa kijiji. Kila anyekuwa na nafasdi huitumia kumlima aliye chini yake. Haki itafute huko huko majuu, huku kwetu hata haki ya kufa na kulazwa kwenye kitanda cha milele pia inaweza kunyang'anywa na ukaishia kusua sua Mortuary.
b. Hata kama sijaridhika nifanye nini? Niunde ya kwangu? Hiyo kamati imeundwa na rais, sasa unataka na mimi niwe rais? Mbona Dr. Slaa hajaridhika na amefanya nini zaidi ya kupiga kelele zisizo na majibu bungeni? Maoni yangu kwenye hili hayana maana yoyote, hayakuongezei wewe wala wasomaji wako tonge la ugali wa muhogo. Badala yake yanaongeza chuki tu na kusababisha watu wengi kuchukia na kufa kwa pressure. Mwenye maamuzi haya ni rais wa nchi na bahatii mbaya tulimchagua kwa uzuri wa sura yake na wala sio uzuri wa matendo yake. Hivyo kuridhika au kutokuridhika kwangu nitakuonyesha kwenye kisanduku cha kupiga kura ya rais.
c. Sasa kama serikali imeficha Meremeta, you damn waandishi wa habari! mpo kwa ajili ya nini? Nendeni mkafukue kule walikoficha kisha tuanikieni wote tuone. Sasa unataka mimi nisiridhike na baada ya hapo niende kufukua huo uchafu ulikofichwa? Mimi ni daktari bwana, siogopi kuufutwa uchafu ulikojificha. Huwa nakagua kinyesi, napitisha mkono kwenye ile kitu inayoliwa usiku ili niangalie kama ni nzima au la. Unafikiri nitashindwa kutumbukiza kono langu kwenye hii chafu chafu ya Meremeta?
d. Aafadhali amejiuzia yeye kuliko angewauzia wageni. Hivi mzee Mwanakijiji wewe vipi hujui deals za nchi hii? Kuna deals kuanzia kwa Matona mpaka kule Ikulu. Leo mimi nimefanya deals zangu tatu, narudi home kama shujaa kwa familia na watoto wangu. Wasio jua deals wamekimbilia Ulaya baada ya hapa kuwashinda. Kwa tulioko TZ, deals ni sehemu ya maisha yetu. Tunazidiana speed tu. Njoo Bongo na ukamatwe pale Morogoro kwasababu gari lako halina fire extinguisher; traffic anakuambia safari hii haipo tena labda utoe 50,000 nikutafutia hiyo kifaa. Utafanya nini?
e. Uza yote hayo kwa makaburu bana! Waswahili tumeroga hatujui kitu chochote. Uliona wapi wenye akili wanakimbia nchi yao ili wakabebe mabox na kuwaachia wageni wanafaidi nchi yao? Watanzania wote bana! ni vichaa, akili zetu kama za yule mbwa, anabweka kwa mbali huku mwizi anapakua asali tu. Tunawaona wezi kwanini tunapigia kelele USA na sio kuja hapa Manzese tushirikiane na akina Dr. Slaa. Kwanini tunaunga mkono vyama hewa ambavyo hata havijazaliwa badala ya kuunga mkono chama kama CHADEMA ambacho kiko miaka mingi hata kama ni cha ukoo? Ukitaka kushiriki unaenda kuoa mjuu wa Mtei, usijali hata ukiwa na mke tayari, sisi hapa mitala inaruhusiwa. Karibu viongozi wetu wote wana mitala, hata mheshimiwa rais ana kamtala kake anavinjari usiku usiku na kwenye facebook yake anaweka busy. Ukisikia mbongo anasema yuko busy, jua anatongoza au anshughulikia totoz! mpya. Walinzi wanaachiwa washughulikie ile mama ya zamani! Zuma style.
f. Hiyo sheria ya kuhujumu uchumi lini ilifanya kazi? Sasa unataka sheria iliyofeli sasa tuitumie kwa mafisadi ili ifeli zaidi? Kwanza mafisadi wote ni marafiki wa raisi sasa unataka mimi nifanye nini? Unataka nikosane na raisi wangu? Hapana bana! hawa mafisadi washughulikieni wenyewe huko mitaani kama mnavyochoma moto vibaka. Mkiwaleta kwetu wabunge tuwajadili, tutawaachia maana ni wenzetu au wametusaidia pesa za kampeni zetu. Chomeni moto huko huko kwenu kwa kutumia njia nyingi. Wengi wao wanapenda ngono, wapelekee totozi wenye ngoma, wengi wanapenda kitimoto, ongezeeni fat humo baada ya muda pressure ipande na kuwaua. Wengi wanapenda miti shamba, ongezeni na ile mionzi ya Warusi.