Selelii agoma kurudi Bungeni!?

Status
Not open for further replies.
Safi kabisa!!! Kata mzizi wa fitina

kimokole
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-online.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Wed Jun 2010
Posts 6
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
 
Nawashukuru wote mliotoa michango kunihusu na hasa mliolenga maisha binafsi, pili nikupongeze sana Dr kigwangala kwa kujibu post hii nikiomba ukaze buti maana safari bado ni ndefu na wale wenye mawazo kuwa kila anayegombea Nzega katumwa basi pole zao na hasa nikiwajulisha kuwa selelii kurudi nzega kama Mbunge ni miujiuza! maana kabanwa kila kona ndo kwanza kaondoka jana kwenda Dom nadhani kuna mpambe ake humu Jf kampigia simu kibaya zaidi ana ahadi nyingi zisizotekelezeka kwenye maeneo mengi lakini cha kusikitisha zaidi kwa muda wa miaka mitano kuna maeneo hajakanyaga kabisa what do you expect kwa wapiga kura? ametumia miaka mitano kuzungumzia ,asuala ya Rich mond ambayo wana kijiji wa Mwamesu wala hawajui what is Rich mond; kama kuna wanao kereka sana na hili karibu Nzega mumuokoe Ndugu yenu hali yake ni mbaya kupita maelezo. keep it up Dr kigwangala!

Miaka mitano anazungumzia RICHMOND.......miaka 5 seleli anazungumzia Richmond? kweli akutukanaye hakuchagulii tusi
Dr H.K tafuta wapiga debe wenye akili huyu anaharibu... Richmond ni pigo kwa Watz wote haijalishi wanaijua ama hawaijui...ni Richmond hizi ndizo zimewafanya wanakijiji hao waendelee kuwa katika umaskini mkubwa hata kama hawaijui....selelii ana haki ya kusimama na kuchalenji ubadhirifu kama huu, si lazima wanakijiji waijue kwa sababu ni system hiyo hiyo iliyowanyima access ya habari na elimu ya uraia...
Dr huyu mpambe bomu la machozi
Mix with yours
 
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi.
Wengine wanadhani mimi na wewe tuna ubia, naomba tu kusema hapa kwamba sikufahamu wala sijawahi kuwasiliana na wewe wala kujadili lolote lile kuhusu azma yangu ya kuwania Ubunge Nzega! Naomba tu pia niwataarifu ndugu zangu wanaJF kwamba mimi sina ubia na mtu yeyote yule katika harakati zangu za kuwania Ubunge, sijaombwa na wazee, sijatumwa na mtu yeyote yule - ila ni nafsi na dhamira yangu pekee iliyonituma kuutafuta Ubunge wa Nzega!

Jimbo la Nzega lina mtego tu kwamba yeyote atakayejitokeza kugombea basi atadhaniwa kuwa ametumwa na mtu, hususan akiwa na ushawishi na anakubalika zaidi ya Selelii! Hili lilijitokeza hata pale nilipoamua kutangaza nia yangu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pale Habari maelezo! Hili linakuja kutokana na Selelii kujipambanua kama ni mbunge shupavu anayepambana na ufisadi! Wengi wanakuja kufikiri kwamba jimbo la Nzega lina maslahi ya watu fulani wanaoitwa mafisadi...na kwamba yeyote anayempinga Selelii basi anaungwa mkono na au ametumwa na hawa watu.....and this is a big misnomer! Kugombea Uongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, na hatuwezi kuliacha jimbo chini ya Selelii kwa kuhofia kusemwa tumetumwa! Tayari kuna watu zaidi ya watano wamekwishatangaza nia ya kuwania Jimbo la Nzega. Hivi wote hawa ni vibaraka wa mafisadi?

Regards,
Dr. Hamisi Kigwangalla.

Big Dr komaa nao, ubunge wako mwaka huu labda wakologe kama kawaida yao, kwn nacikia huyo Seleleii anashirikiana na mwa mama mmoja wa hpo nzega hapo ni mwanga kinoma kuwa makini watakumaliza
 
Mwenye macho haiambiwi ona, mkuu una post 41 zote zinamponda au mkejeli Samwel Sitta na Lucas Seleli. Mwenye macho anaona na kuujua ukweli, fisadis at work!.

Mkuu big up upo makini, tunapenda watu wanaochallenge kwa facts kama hizi. Jamaa hawezi kucomment kitu kwani umemgusa pabaya.
 
Najaribu kuingia serikalini.

Siku nikifika nafasi ambayo ninaweza kumshughulikia RA atapata cha moto tu. Sijali itachukua miaka mingapi lakini nitafikia lengo langu tu. Na mtu wa kwanza kushughulika naye atakuwa RA. Lazima arudishe na kulipa kila senti hadi ya mwisho.

Sorry RA nitakuwinda popote utakapokuwa duniani hata huko kwenu Iran nitakufuata. Umeiweka nji hii njia panda na kuifanya kama ni property yako ya mfukoni.
 
"Ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe" Muacheni SELELII wetu, ni mpiganaji mbayaaaaaaa:embarrassed:
 
Wana Nzega plz nawaomba mrudisheni Mh.Selilii maana ni mmoja wa watu makini katika siasa za bongo zenye fitina kibao,nadhani si wakati wa nyinyi kupokea kanga na fulana oversize kutoka kwa hao wanaojiita ni watetezi wenu.Huyo Dr nadhani ni vizuri akatumia elimu yake kusaidia jamii kwa nyanja nyingine.

SERVED TO SERVE
"We are the family of Almight God"
 
Najaribu kuingia serikalini.

Siku nikifika nafasi ambayo ninaweza kumshughulikia RA atapata cha moto tu. Sijali itachukua miaka mingapi lakini nitafikia lengo langu tu. Na mtu wa kwanza kushughulika naye atakuwa RA. Lazima arudishe na kulipa kila senti hadi ya mwisho.

Sorry RA nitakuwinda popote utakapokuwa duniani hata huko kwenu Iran nitakufuata. Umeiweka nji hii njia panda na kuifanya kama ni property yako ya mfukoni.

Good, lakini uwe makini asije akakuwinda wewe kabla hujafika huko unakotaka kufika ndiyo uanze kazi. Nakushauri uanze sasa hata kama ni kumvizia milima ya sekenke.
 
KIngwalangwala gombea tu kama roho yako inapenda na kama una mtaji wa wananchi wakuuunga mkono kila mtu mwenye nia akiwa sawa kwa muujibu wa sheria naagombee popote kupitia chama chochote hii mambo ya jimbo langu hii si nchi za mama zao bwana
 
Go man go! Wahaya wansema hata mkulima mzuri sana ufikia mahala akapumzika! Seleli ni mkulima nzuri sana itakuwa vizuri wana-Nzega wakamwambia apumzike kidogo, avute pumzi anarudi 2015 kwa nguvu mpya, kasi mpya ma hari mpya!
 
Mimi sijazielewa hizi degree za huyu daktari (MD, MPH, MBA), labda kama hiyo MD ni 'Managing Director', ndipo zitaendana na hizo nyingine, vinginevyo kama anamaanisha 'Medical Doctor' kama wale washkaji zangu wanaopiga lile buku zito la Muhimbili, nina wasiwasi huyu ni msanii flani, hana hizo degree. Hilo degree la MD balaa lake usiombe, washkaji niliomaliza nao skonga wakajiunga na chama hilo bado hawajamaliza masomo, wakati mimi tayari nilishaingia mzigoni kitambo na degree ninayo tayari. Huyu anadanganya. Huwezi kupiga MD halafu ati ukasome hizo degree za Mzumbe, wapi na wapi? Mwongo huyu, na wala simshangai, wanasiasa ndio tabia zao kudanganya elimu, sasa hivi watu wameshaona kujiita 'Dr' ni dili la kupatia kura, ila huyu kachemsha kiukweli, anadanganyia na lidigrii la kiukweli kama MD? Noma mwanangu, yaani nimechoka. Bora hata angedanganyia na PhD feki kama wenzie kibao hukohuko kwenye siasa. E bana ningekuwa na simu ya msela wangu Kainerugaba Msemakweli ningemtonya amfuatilie huyu mbwiga, si ajabu ni fisadi wa elimu.
 
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi.
Wengine wanadhani mimi na wewe tuna ubia, naomba tu kusema hapa kwamba sikufahamu wala sijawahi kuwasiliana na wewe wala kujadili lolote lile kuhusu azma yangu ya kuwania Ubunge Nzega! Naomba tu pia niwataarifu ndugu zangu wanaJF kwamba mimi sina ubia na mtu yeyote yule katika harakati zangu za kuwania Ubunge, sijaombwa na wazee, sijatumwa na mtu yeyote yule - ila ni nafsi na dhamira yangu pekee iliyonituma kuutafuta Ubunge wa Nzega!

Jimbo la Nzega lina mtego tu kwamba yeyote atakayejitokeza kugombea basi atadhaniwa kuwa ametumwa na mtu, hususan akiwa na ushawishi na anakubalika zaidi ya Selelii! Hili lilijitokeza hata pale nilipoamua kutangaza nia yangu kwa umma kupitia vyombo vya habari, pale Habari maelezo! Hili linakuja kutokana na Selelii kujipambanua kama ni mbunge shupavu anayepambana na ufisadi! Wengi wanakuja kufikiri kwamba jimbo la Nzega lina maslahi ya watu fulani wanaoitwa mafisadi...na kwamba yeyote anayempinga Selelii basi anaungwa mkono na au ametumwa na hawa watu.....and this is a big misnomer! Kugombea Uongozi ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, na hatuwezi kuliacha jimbo chini ya Selelii kwa kuhofia kusemwa tumetumwa! Tayari kuna watu zaidi ya watano wamekwishatangaza nia ya kuwania Jimbo la Nzega. Hivi wote hawa ni vibaraka wa mafisadi?

Regards,
Dr. Hamisi Kigwangalla.

Hamisi [dogo]

mimi nakufahamu mdogo wangu; nakumbuka sana wakati unachacharika pale intern... nakushauri ukae kimya hii forum sio pale intern mlipokua mnalamba CCD za elfu mbili na tabia ya ajabu ya ku-lobby kwa yule jamaa wa vyumba. wewe ni mwanasiasa ndio lakini spidi unayokuja nayo ni sawa na muendesha basikeli kwa kasi asiyeweza kusiki ahoni itokayo nyuma

kaa chini na utafakari ubora wako... tunakujua sana na tutaweka wazi sifa zako na hasa kauli zako!!! wew umetumwa na mko kama kumi na kitu hivi huwa mnasema mzee ametutuma vijana tupambane... SHAURI YAKO MKUU BORA UKAE KIMYA UACHE WATU WAJAZE HII THREAD

HUNA QUALITIES ZA SELELII HATA NUSU
 
Ahsante sana Zyansiku kwa kunifagilia na kunipa pongezi...
Dr. Hamisi Kigwangalla.

Inaniwia vigumu kuelewa nani kati ya Zyansiku na Kigwangalla mwenye upeo mdogo wa kuelewa mambo. Wakati unategemea Kigwangalla ampuuze Zyansiku na pumba zake yeye anampigia vigelegele. Dr. concentrate kwenye kampeni zako kuliko kukubali kusafishwa kwa uchafu! Wewe siyo mara yako ya kwanza kugombea Nzega so be realistic.

Mara ya mwisho mliposhindwa kura za maoni je sababu ilikuwa nini? Hamkukubalika?( Leo 5 years on) umefanya nini Nzega kukufanya/kujiona ukubalike hadi watu waseme umetumwa? Lakini mjue bila ya mambo ya ufisadi na upiganaji wa mbunge wenu ndio kumefanya hata nyinyi mpate umaarufu (ndio maana safari hii mna ujasiri hata wa kwenda maelezo).

Kwamba mnapambana na outspoken MP kila mtu atakuwa interested. Otherwise kama Seleli asingekuwa maarufu ingetuchukua muda mrefu sana kujua hata majina yenu na wala kugombea Nzega isingekuwa habari.

Naomba kutoa hoja.
 
Wakuu,

Acheni kuwa negative sana, mtaishia kukatisha tamaa watu wengi sana.

Hata hao mnaowaona mashujaa leo waliwapinga/waliwaondoa madarakani watu wengine.

Kugombea ni haki ya raia yeyote anayetaka, na kwa mbunge mchapa kazi hata siku moja hatakiwi kuwaogopa watu wapya wanaotaka kugombea kwenye majimbo yao. Wananchi sio wajinga, kama katimiza wajibu wake basi watampa kura. Waswahili wanasema kitanda usichokilalia, huwezi kujua Kunguni wake. Mtu anaweza kuwa hero kitaifa lakini kumbe kule kwao akawa na matatizo mengi sana. Akina Malecela waliangushwa kule kwao shauri ya mambo hayo hayo.

Kama ilivyo JF siku zote, mchambueni huyu mgombea na kama ana madudu huko nyuma basi yaanikeni hapa. Hii ya kuanza kuita watu mafisadi au wametumwa na mtu bila hata kuwa na chembe ya ushahidi kwa kweli inashusha hadhi nzima ya JF where we dare to speak openly with facts.

Dr Nakutakia mafanikio mema na nguvu na afya njema maana mpambano wa ubunge kwa Tanzania ni hekaheka kubwa. Muhimu ni dhamira yako mwenyewe na ndio itakusuta au kukushangilia maana wewe mwenyewe ndio unajua ukweli wote kwanini unaenda huko jimboni. Jitahidi sana kutokutumia njia chafu maana hazitakusaidia.
 
same, urambo, kyela, nzega, simanjiro, nk. tatizo si mabadiliko ndugu, tatizo ni dhamira iliyo nyuma yenu.... namjua hamisi vizuri sana na dhamira zake pia.... NEED WE GO DEEPER?
 
Mimi sijazielewa hizi degree za huyu daktari (MD, MPH, MBA), labda kama hiyo MD ni 'Managing Director', ndipo zitaendana na hizo nyingine, vinginevyo kama anamaanisha 'Medical Doctor' kama wale washkaji zangu wanaopiga lile buku zito la Muhimbili, nina wasiwasi huyu ni msanii flani, hana hizo degree. Hilo degree la MD balaa lake usiombe, washkaji niliomaliza nao skonga wakajiunga na chama hilo bado hawajamaliza masomo, wakati mimi tayari nilishaingia mzigoni kitambo na degree ninayo tayari. Huyu anadanganya. Huwezi kupiga MD halafu ati ukasome hizo degree za Mzumbe, wapi na wapi? Mwongo huyu, na wala simshangai, wanasiasa ndio tabia zao kudanganya elimu, sasa hivi watu wameshaona kujiita 'Dr' ni dili la kupatia kura, ila huyu kachemsha kiukweli, anadanganyia na lidigrii la kiukweli kama MD? Noma mwanangu, yaani nimechoka. Bora hata angedanganyia na PhD feki kama wenzie kibao hukohuko kwenye siasa. E bana ningekuwa na simu ya msela wangu Kainerugaba Msemakweli ningemtonya amfuatilie huyu mbwiga, si ajabu ni fisadi wa elimu.

Mkuu huyu jamaa namfahamu na ndiyo maana sikutaka kuchangia hii thread.Kwa kifupi tu MD yake ni genuine na aliipata MUCHS siku zile.Hili nina uhakika nalo 100%.Hizo MPH na MBA nilisikia kutoka chanzo changu cha uhakika kuwa alizipata Sweden.Mkuu siku nyingine unapomshutumu mtu,tena kwa kashfa,usitumie hisia,jaribu kwanza kutulia na kuchunguza ili uje na vielezo stahiki.
Elimu yake haina tatizo labda kwenye mengineyo.
 
same, urambo, kyela, nzega, simanjiro, nk. tatizo si mabadiliko ndugu, tatizo ni dhamira iliyo nyuma yenu.... namjua hamisi vizuri sana na dhamira zake pia.... NEED WE GO DEEPER?
Go deeper man go......ningeshangaa kama ningesoma negative response dhidi ya zyasiku au huyu Dr toka kwa mtanzania. Hakika ningeshangaa sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom