Sehemu za kutembelea hapa Dar

Sehemu za kutembelea hapa Dar

Hebu anaetaka camping aje PM twende sio lazima awe KE hata mkiwa ME fresh tu

tuwe mtu 4 twendeni hii coming weekend Jumapili, Mad Max hebu nielekeze

mgeni ninaetokea Hapa Mbezi Mwisho,nielekeze napita njia ipi hadi nifike nipe idea idea

halafu ntajazia jazia nyama na Google Map,Last sunday niliboeka kinoma ikabd nifanye tour ya kuzunguka Dar nzima kuhakikisha tu ule mshale wa mafuta unatoka kwenye full unainama kidogo,ndio ikawa mwisho wa tour yangu.

Jumapili ijayo nataka nijaribu tena huko...
Daaa.
Hayo mafuta ungeyanyonya ukayahamishia kwangu 🤣🤣🤣🤣
 
Pamoja sana. Unaweza kwenda day trip. Itakua chini ya elfu 20 kwa mtu ila mkiwa wengi inakua cheap. Bei zipo hivi:
  • Kiingilio 2500 (kwa mtu),
  • Hela ya guide 20,000 (guide mmoja anahudumia watu 10 so mkienda 10 kila mtu anachangia elfu 2 so better mkiwa crew)
  • Boat elfu 10 (sio lazima)
  • Ukitaka camp tent zipo za 15,000 (maximum watu 4) na zipo kubwa za 40,000 izo ata watu 10.
  • Ukienda na camera kubwa unailipia elfu 5, drone 50,000 ila nadhani hautaenda nazo.
  • Ndani hamna vyakula (ila wameanza kutengeza mahala pa kula) so nunua bites na vinywaji nje.
  • Gari kuingia elfu 5 ila ukipaki nje free.
Washkaji wakarimu sana pale yaani wako peace knm. Utaenjoy sana boss.

Hapa Hiking on top kabisa unakua unaiona Dar kwa chini. Wamejenga ngazi sahivi kupanda rahisi.

View attachment 2391100

Hapa chini camping pembeni mwa bwawa.
View attachment 2391103


PS: Gharama naweza kua nimekosea kidogo sana. Ila zinaenda humo humo.
Asante kwa kushare je unaweza kwenda mwenyewe kama ni msichana usalama wake upoje?
 
Natumaini wewe unaesoma uzi huu ni mzima wa afya.

Nimekuwa nikikaa hapa Dar kwa muda mrefu kidogo na kumakinika na kazi tu. Hii imekuwa ni 'one way go and return home'. Kwa sasa naona kuna umuhimu wa kutembea sehemu mbalimbali za kutulia na hata kuona jinsi watu wanavyokula maisha hapa Dar.

Kwa hiyo kama kuna anayejua sehemu mbalimbali nzuri iwe ni bichi, klabu, migahawa au mahali mtu anaweza kwenda kutuliza akili kidogo kwa muda na kurudi ambazo zipo hapa Dar. Na hizo sehemu nikienda kutulia hata vinywaji na chakula gharama ya chini iwe 20k.

Kuwe na watu wengi ambao wanakuja sehemu hiyo, muingiliano uwepo kidogo wa watu, hata kukiwa na 'vibe' kidogo sawa kabisa. Eneo na jina la mahali ndicho nachohitaji ili nianze kwenda kupoa siku za wikiendi na siyo kuzubaa tu nyumbani.

Kwa msaada wa google maps yote yanawezekana!
Kama Una kampan nenda pachkonjo kigamboni stress-free zone
 
Usalama upo bro. Sio mchana wala usiku. Usalama mkubwa sana. Ni misitu iliochini ya TFS (Tanzania Forest Service) Agency.

Diamond Platnumz ndio ameupa umaarufu zaidi baada ya kupigia baadhi ya vipande kwenye video ya Mtasubiri alioimba na Zuchu.

View attachment 2391237

Lakini pia wakati Jokate ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alikua na campaigns nyingi sana kule kama Ushoroba Marathon na pia aliwahi mtumia Diamond kama balozi kutangaza utalii wa pale Ushoroba.

View attachment 2391238

Baadhi ya picha (Sio zangu hizi)

View attachment 2391239

View attachment 2391240
Hakyanan najuaga haya maeneo yapo lushoto huko sijui. My goodness kwanini sijawahi kujua aisee... Naanza ziara rasmi. Kumbe Dar ni balaa sana nilikua naboreka bure..siku nimeenda bagamoyo hadi snake park kaole, na Dar zoo nikajua nimemaliza maeneo ya asili. Damn damn damn, I love nature..pindi nipo Iringa nilikuaga naenda hadi tosamaganga kwenye maporomoko afu man alone bila demu
 
Tupange twende namimi, then tukifika kila mtu anaweza jipa mda flani alone kutafakari yalompeleka. Tunanunua vyuku kienyeji tinaweka kwenye ice tunaenda kuchoma hh

Tupange twende namimi, then tukifika kila mtu anaweza jipa mda flani alone kutafakari yalompeleka. Tunanunua vyuku kienyeji tinaweka kwenye ice tunaenda kuchoma hh

Tupange twende namimi, then tukifika kila mtu anaweza jipa mda flani alone kutafakari yalompeleka. Tunanunua vyuku kienyeji tinaweka kwenye ice tunaenda kuchoma huko
Wewe umewahi kwenda
 
Okay itategemea na interests zako. Ila me naweza kukushauri kama unapenda nature, tembelea sehemu hizi:

1. Pugu Natural Forest (Ushoroba) Hii ipo opposite na Minaki Secondary, kwahiyo daladala ni kama 2000/= jumla kutokea Ubungo.
Hapo utaweza kufanya hiking, camping, kuendesha boat, etc.
Gharama jiandae kuanzia 20k hadi 80k kutegemea na huduma.
View attachment 2390959

2. Vikindu forest reserve. Hii ipo opposite na kiwanda cha juice cha Bakhresa kipo Mbagala kwa mbele nimepasahau jina.
Activities ni sawa kabisa na Pugu hapo namba 1 ila ni cheaper na kasoro hiking hawana milima.

View attachment 2390964

Me kwa hizo mbili ndio recommend kama mtu wa kurelax mfano na bebe au friends.

Beaches, Malls, na sehemu zingine watakupa wadau.
Hizi za kibabe sana
 
Back
Top Bottom