Sehemu za kutembelea hapa Dar

Sehemu za kutembelea hapa Dar

Umeeleza vizuri, vp usalama wa hizo boat za kwenda na kurudi, nilisikia watu wakipoteza uhai kwenye hizo boat na wengine kunusurika hasa za mbudya, sijui kama kuna maboresho.


Boats za kwenda Mbudya zipo salama ila usalama wa safari unapungua mida ya jioni kwa kuwa mawimbi yanakuwa makubwa kiasi.. so kama unaogopa ile panda shuka ya mawimbi ya bahari basi nenda Mbudya mapema asubuhi, enjoy kisha ugeuze mapema pia.. Yaani usivuke saa 10 jioni uwe usharudi au upo ndani ya boat unarudi mainland.
 
Ila viongozi wa jiji inabidi kujitafakari sana. Miji mingine mikubwa ya nchi huwa ina sehemu za muhimu, ambazo kwetu hamna.

1. Central Square/City park - kwa dar sijui hii ipo wapi lakini ni muhimu sana kwenye mji huwa panakuwa sehemu ya kupumzika na watu kukusanyika hasa usiku/jioni....mfano kwa kenya wana Uhuru Park, Jivanjee Garden, Paris kama Eiffle Tower n.k...Zanzibar ndio kama Fordhani hivi.

2. Viwanja vya michezo, sehemu za michezo za umma....hizi nadhani hamna kabisa...kila mahali pamejengwa kiholela na magorofa mengi yasiyo na tija...sehemu zilizowazi hazijawekewa utaratibu mzuri, mfano leaders club.

Hapa pia kwenye barabara kuna zile sehemu za watembea kwa miguu (walking lanes) na baiskeli hazipo kwenye barabara nyingi. Hongera barabara mpya inayoenda coco beach kupitia daraja la tanzanite hii ipo, na unaona jinsi watu wanafurika jioni kutembea na kufanya mazoezi.
Hii inapaswa kuwepo kwenye barabara zote, ili kuwa na mji wa watu wenye afya.

3. Beach - nia aibu mji wa pwani lakini hamna fukwe ya maana, kupata "beach experience" mpaka watalii waende zanzibar au diani mombasa au...
kulipaswa kuwa na mkakati maalum kuhakilisha fukwe za visiwa vya dar na Kigamboni zinawekwa safi na kuwa zinavutia. Kuhakikisha kuna usalama na usafiri wa uhakika kufikia visiwa

4. Vivutio/vitu vya kufanya - ni mji wa ajabu ambao wageni wakija wanaishia kwenda zanzibar kwasababu hauna kitu cha kuona au kutembelea. Nashauri kwa wangeboresha makumbusho, wakaongeza labda makumusho ya Mwl. Nyerere.
Pia wakaenda kuchukua yule dinosar (mabaki ya mjusi wa kale) ujerumani n.k. Pia nashauri
  • kuwe na city tour ya kueleweka (wataaam wa utalii wanaweza kuandaa hii na kuwa na maguide waliosajiliwa kuifanya au kuwafunza madereva taxi) bahati mbaya kwasasa mji wa zamani wa historia wote umebomolewa.
  • Kuwe labda na "Cruise trip" zenye party+dinner+ music za kila usiku dar to bwagamoyo kama sehwmu ya utalii
  • Sehemu za utamaduni (cultural center) na ngoma za makabila maarufu ya Tanzania kama maasai, sukuma, zaramo n.k.
  • sehemu za sanaa mbali mbali - theatres kwajaili ya sanaa zinazovutia sio mpaka ufaransa ndio wadhamini kupitia Alliance France.
  • Slum tour- hivi slums ni wapi au mji wote tu maana haujapangwa???
  • Dar view center - hapa wanapswa kujenga jengo refu au hata lile lililopo (psssf twin tower au lile bandari) liwe lina sehemu ya watu kupanda mpaka top floor yenye uwazi wa kuangalia mji kama ilivyo dubai burj khalifa au hata KiCC ya majirani.

5. Animal shelter/zoo - mfano mzuri ile wameanzisha Kilimanjaro inaitwa Serval watu wanaenda kulisha wanyama au kama Giraffe Center Nairobi.
Kuna zoo ipo kigamboni ila inahitaji mamboresho makubwa ilivyo haivutii kabisa.

6. Usafiri wa umma - mwendo kasi inajitahidi na muendelezo wake unaendelea kujengwa hapa hamna tatizo.

Pia kama jiji inabidi kufikiria kuanzisha light train/metro za mjini hizi hubeba watu wengi kwa wakati mmoja na huwa na ufanisi sana...au wazo la barabara ya kasi ya wote ya kulipia kama ilivyo Express way ya majirani...kwa ukuaji wa dar maiaka 30 ijayo msongomano utakuwa mbaya zaidi.
Pengine kuhusu malori yanayotoka bandarini wangedfikiria kutengeneza barabara maalum ya malori kutoka nje ya jiji itakayotokea kibaha au chalinze punguza msongomano.

7. Nyumba/housing - hapa kuna tatizo kubwa la nchi nzima limeanzia kwa kutokupima ardhi hivyo hamna mipango....

Serikali ikiamua aidha kwakutumia wawekezaji binafsi au yenyewe kama ilivyofanya magomeni kota, kuna uwezekano wa kuboresha jiji kwa kujenga makazi ya kisasa ya bei nafuu. Hii itapunguza hata foleni...hakuna haja mtu anafanya kazi mjini anaishi Bunju....fikiria kama Sinza, magomeni, kinondoni kungekuwa na majumba ya makazi ya kutosha ambapo watu wanaishi kwa kununua au kupanga. Kwasasa miradi inayofanywa na NHC ni ghali mno kuliko hata US kwahiyo haina mantiki kununua ni kama "luxury" sio kwaajili ya kuondoa tatizo.
Wanaweza kuanzisha mradi kama huu wa magomeni kuvunja nyumba zilizopo na kujenga za kisasa kwa utaratibu maalum wa kulipa fidia...maeneo kama tandale, manzese, magomeni, mwananyamala, n.k
View attachment 2395053
View attachment 2395051


Ili jiji livutie na pia lijipange kwa ukuaji wake na ongezeko la watu lazima liwe na mipango na uwekezaji wa kutosha, lakwetu pengine mipango ipo inafanyiwa kazi naamini halija achwa tu. Ni muhimu kwenda na kazi maana ongezeko la watu ni kubwa sana...lakini kwasasa ndio maana halivutii tena watalii wa nje labda watalii wa ndani (kutoka mikoani) lakini pia wakazi hawalifurahii kwa kukosa vitu vya msingi vya miji ya kisasa. Hili wanaweza wasilione mpaka waende sehemu zingine.
Ushauri wako una hadhi ya nyota tano
 
Okay itategemea na interests zako. Ila me naweza kukushauri kama unapenda nature, tembelea sehemu hizi:

1. Pugu Natural Forest (Ushoroba) Hii ipo opposite na Minaki Secondary, kwahiyo daladala ni kama 2000/= jumla kutokea Ubungo.
Hapo utaweza kufanya hiking, camping, kuendesha boat, etc.
Gharama jiandae kuanzia 20k hadi 80k kutegemea na huduma.
View attachment 2390959

2. Vikindu forest reserve. Hii ipo opposite na kiwanda cha juice cha Bakhresa kipo Mbagala kwa mbele nimepasahau jina.
Activities ni sawa kabisa na Pugu hapo namba 1 ila ni cheaper na kasoro hiking hawana milima.

View attachment 2390964

Me kwa hizo mbili ndio recommend kama mtu wa kurelax mfano na bebe au friends.

Beaches, Malls, na sehemu zingine watakupa wadau.
Ushoroba is the best kwakweli, kama unahitaji kurelax pazuri
 
Back
Top Bottom