Sehemu ya msitu wa mlima Kilimanjaro inaungua moto!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Sehemu ya msitu wa mlima Kilimanjaro inaungua moto muda huu.

Habari kamili itakuja

Source ITV habari!

====

Wazima moto nchini Tanzania wanapambana kujaribu kuudhibiti moto unaouteketeza mlima mrefu zaidi barani Afrika, mlima Kilimanjaro. Kulingana na shirika la mbuga za kitaifa Tanzania TANAPA moto huo ulianza Jumapili.

"Moto huo bado unaendelea na wazima moto kutoka TANAPA, taasisi zengine za serikali na wakaazi wa eneo hilo wanaendelea na juhudi za kuudhibiti moto huo," alisema Pascal Shelutete afisa wa TANAPA. Shelutete hakutoa taarifa zaidi.

Hapo Jumapili Shirika hilo la mbuga za kitaifa lilichapisha picha ambayo haionekani vizuri kwenye mtandao wa Twitter ikisema ni moto unaouteketeza mlima Kilimanjaro.

Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 6,000 sawa na futi 20,000 kutoka usawa wa bahari. Karibu watalii 50,000 wanaukwea mlima huo kila mwaka.
 
Hii ni kweli kabisa mkuu Mimi nko maeneo ya shanty town naona ishara ya moto tokea saa kumi na mbili majira ya jioni leo.
 
Back
Top Bottom