Moto unawaka usiku huu msitu wa Mlima Kilimanjaro

Nature

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
758
2,027
Kwa wale wakazi wa Mji wa Moshi na maeneo ya Jirani kuanzia saa 2:30 usiku huu ukiangalia Upande wa kaskazini ulipo mlima Kilimanjaro unaonekana Moto mkubwa. Unaoambatana na Moshi mwingi.

Kama hali itaendelea bivi basi itabidi Mamlaka husika zijiandae kwa ajili ya kuzima moto huo mapema kabla hauja sambaa na kuleta uharibifu zaidi.

Hiyo unaona kama taa inawaka kwa juu ni Moto na kadiri muda unavyoenda ndivyo unazidi kusambaa eneo kubwa.

IMG20221021213545.jpg


======

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umezuka katika mlima Kilimanjaro, karibu na eneo la Karanga Camp lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka na jitihada ya kuuzima zinaendelea.

Moto huo ulianza kuonekana jana Ijumaa Oktoba 21, 2022 usiku kutokea Moshi Mjini, ambapo Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), William Mwakilema aliyezungumza na Mwananchi leo Oktoba 22, amesema vikosi vinaelekea kuuzima moto huo.

Taarifa zinaeleza moto huo unawaka ukanda wa Moorland, ambao mimea yake ikishika moto huwa ni mkali na tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) na Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) wametuma vikosi kwenda kuukabili.

Kamishina wa Uhifadhi kanda ya Kaskazini, Betrita James amesema baada ya kupata taarifa za kuonekana kwa moto huo, menejimenti ya Kinapa ilianza mara kazi ya kukusanya nguvu kazi na vifaa, na tayari timu zimeelekea eneo hilo.

Mbali na timu hiyo, video ambazo zimesambaa katika makundi mbalimbali ya Whatsapp zinawaonyesha baadhi ya waongoza watalii (Guides) na wapagazi (porters), wakijaribu kuzima moto huo kwa kutumia majani ya miti.

Mmoja wa waongoza watalii mwenye uzoefu na njia hiyo, Geness Shirima, amesema kwa kadri alivyojulishwa, moto huo uko karibu na Karanga Camp na Askari wa Kinapa na wadau wengine walikuwa wakielekea huko kushiriki kazi ya kuuzima.

“Ukitoka kituo cha Mweka ndio unaenda Millennium au High Camp halafu ndio Karanga yaani iko kwenye zone (ukanda) moja. Ni eneo liko juu kama urefu wa karibu meta 4,000 hivi kutoka usawa wa bahari.

“Mfano kama chakula cha wageni kinapandishwa huwa kinapelekwa Karanga camp kwa sababu ndio kituo ambacho ni kabla ya kwenda kituo cha mwisho kwenda Summit (kileleni) pale ndio wageni wanapelekewaga chakula fresh”

Amesema moto huo unaonekana kutokea njia ya Mweka kuelekea ukanda wa Moorland wenye vichaka.

“Ndio maana huu moto unakamata kwa kasi sana ni kama umewasha petrol,” amesitiza.

Oktoba 2020, moto mwingine ulizuka katika mlima huo katika ukanda wa nyasi na vichaka na kuteketeza vibanda 15 vya kulala wageni katika mlima Kilimanjaro pamoja na mifumo ya umeme wa jua na miundombinu ya maji taka.
 
Hakuna majanga hapo, huchomwa kwaajili ya uoto mpya. Hata Serengeti wanachoma kila mwaka.
Uoto wa Hifadhi ya Kilimanjaro siyo sawa na Serengeti...
Huko KLM ni Misitu na Miti mirefu ndyo inateketea...

Na kwa Theluji iliyo kileleni hauwezi kuwasha moto kwa ajili ya uoto mpya....

Grow Up.
 
Kwa wale wakazi wa Mji wa moshi na maeneo ya Jirani kuanzia saa 2:30 usiku huu ukiangalia Upande wa kaskazini ulipo mlima kilimanjaro unaonekana Moto mkubwa. Unaoambatana na Moshi mwingi

Kama hali itaendelea bivi basi itabidi Mamlaka husika zijiandae kwa ajili ya kuzima moto huo mapema kabla hauja sambaa na kuleta uharibifu zaidi.
Mwaka Jana pia hiyo Hali ilijitokeza ila ukuifuqatilia kwa ukaribu utabaini ni uzembe na mazingira yakupiga Hela saivi watu wanajitaftia tuu mazingira wafaidike ni tofauti sana na miaka ya nyuma kidogo
 
Back
Top Bottom