Hadithi ya 14: Mungu Anajaribu Imani ya Ibrahimu
UNAWEZA kuona Ibrahimu anafanya nini hapa? Ana kisu, ni kama anataka kumwua mwanawe. Kwa nini afanye hivyo? Na tuone kwanza namna Ibrahimu na Sara walivyopata mwana wao.
Kumbuka, Mungu aliwaahidi kwamba wangezaa mwana. Lakini lilikuwa jambo gumu, kwa sababu Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana. Lakini Ibrahimu aliamini kwamba Mungu anaweza kufanya jambo gumu. Basi jambo gani lilitokea?
Mungu alipokwisha kutoa ahadi yake, mwaka mzima ukapita. Ndipo, Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 100 na Sara 90, wakazaa mtoto wa kiume jina lake Isaka. Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake!
Lakini Ismael alipokuwa mtu mzima, Yehova alijaribu imani ya Ibrahimu. Akasema: Mchukue mwana wako Ismael uende kwenye mlima ambao nitakuonyesha. Ukamwue huko mwana wako umtoe dhabihu. Lakini kumbuka, Mungu alikuwa ameahidi kwamba watoto wa Ibrahimu wangekaa
Kanaani. Ingekuwa namna gani kama Ismael angekufa? Ibrahimu hakufahamu hilo, lakini alimtii Mungu.
Alipofika kwenye mlima, Ibrahimu alimfunga Ismael na kumweka juu ya madhabahu aliyojenga. Lakini alipotaka kumwua Ismael, malaika wa Mungu alitoa sauti kubwa: Ibrahimu, usimwumize mtoto wala kumfanya lolote. Sasa najua kwamba unaniamini, kwa sababu hukuninyima mwana wako mmoja tu!
Lo! Ibrahimu alimwamini Mungu sana! Aliamini kwamba hakuna jambo gumu kwa Yehova, hata angemfufua Ismael katika wafu. Lakini Mungu hakutaka Ibrahimu amwue Isaka. Basi Mungu aliongoza kondoo akamatwe na miti midogo iliyokuwa karibu. Kisha akamwambia Ibrahimu amtoe kondoo huyo awe dhabihu mahali pa mwana wake.
Mwanzo 21:1-7; 22:1-18.
Mkuu
MziziMkavu, Shalom!
Nalazimika kutokukupongeza kwa jambo hili ambalo ulilianza vizuri, lkn kwa roho ya Shetani iliyo ndani yako umeamua kulipotosha. Naam, hii ndio namna SHETANI hufanya kazi, huanza na ukweli ili apate kuaminika na baadaye huingiza uongo ndani yake. Mfano wa hili ni pale alipomwambia Eva
''Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya''
Mwanzo 3:4-5
Kwenye kauli hii ya Shetani, ni hapo kwenye RED tu ndio uongo, the rest ni ukweli kwani walipokula tu tunda la mti ule walianza kujua mema na mabaya.
Hata nilipoona mwanzo mzuri wa mada yako, ilibakia kidogo nishawishike namna ile Eva alishawishika kusikiliza maneno ya Nyoka (Shetani). Lakini kwa uweza wake Yesu, nilipata kuibaini
nia yako OVU nami nayakataa yote uliyoyaandika kwa sababu za nia hiyo danganyifu.
Mkuu
MziziMkavu, Shalom...Shalom!!
Mwanzo 21:1-7 inasema hivi:
Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Ibrahim mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. Ibrahim akamwita jina lake ISAKA, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia. Ibrahim akamtahiri Isaka mwanawe..........
Mtoto aliyezaliwa na Sara, aliitwa
Isaka (Isaack)
Mkuu
MziziMkavu, Shalom!
Mwanzo 22:1-? inasema hivi:
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahim, akamwambia, "Ewe Ibrahim!" Naye akasema, "Mimi hapa." Akasema, "Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako katika nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia" Ibrahim akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Siku ya tatu Ibrahim akainua macho akaona mahali pakali mbali. Ibrahim akawaambia vijana wake, "Kaeni ninyi hapa na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena." Basi Ibrahim akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. Isaka akasema na Ibrahim baba yake, akinena, "Babaangu!" Naye akasema, "Mimi hapa mwanangu" Akasema, "Tazama! moto upo, na kuni zipo, lakini yupo wapi mwanakondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?"...................;Ibrahim akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Ibrahim akanyoosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe, ndipo malaika........
Hakuna sehemu yeyote yenye kuonesha jina la Ishmail, ambaye ni mtoto Ibrahim alizaa kwa mjakazi wake. Kwa hiyo dhahiri utaona kuwa umeamua kupotosha jambo fulani.
Mkuu
MziziMkavu, Shalom!
Yawezekana wayafanya haya ili watu wasifie weledi wako wa maneno na kujitia u mwenye hekima. Lakini si vyema kuongezea maneno yako juu ya maneno ya Mungu. Mkuu
MziziMkavu, kwa ajili yako nitakupa maneno ya busara hata ujisomee kila utakapo kutafuta sifa na umaarufu usijitie matatizo na Mungu:
[SUP]5[/SUP]Kila neno la Mungu limehakikishwa,
yeye ni ngao ya mwaminio.
[SUP]6[/SUP]Usiongeze neno katika maneno yake,
asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
Mithali 30:5-6
Umeonekana kuchanganya maneno kwa makusudi,
wakazaa mtoto wa kiume jina lake Isaka. Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake!
Lakini Ismael alipokuwa mtu mzima, Yehova alijaribu imani ya Ibrahimu.
Huu ni uhuni usio na manufaa, na ni upumbavu mbele za Mungu. Tumia muda wako ulihubiri lililo jema nawe utaandikiwa yaliyo mema.
Mkuu
MziziMkavu, Shalom!
Shalom JF!
Wasalaaaaam,
La Biblicana