Sehemu 1: Uumbaji Mpaka Gharika

Sehemu 1: Uumbaji Mpaka Gharika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
MAKALA KUTOKA KATIKA

attachment.php




Sehemu 1: Uumbaji Mpaka Gharika

Mbingu na dunia zilitoka wapi? Jua, mwezi na nyota, na vitu vingi duniani, vilitokea namna gani? Biblia inatoa jibu la kweli inaposema viliumbwa na Mungu. Basi, kitabu chetu kinaanza na hadithi za Biblia juu ya uumbaji.

Tunajifunza kwamba, watu wa roho ndio walioumbwa kwanza na Mungu, wakawa kidogo kama yeye. Hao ni malaika. Lakini dunia iliumbwa kwa ajili ya watu kama sisi. Halafu Mungu akaumba mwanamume na mwanamke walioitwa Adamu na Hawa, akawaweka katika bustani nzuri. Lakini hawakumtii Mungu, wakaipoteza haki ya kuendelea kuishi.

Jumla ya miaka kutoka kuumbwa Adamu mpaka Gharika kuu, ni 1,656. Wakati huo waliishi watu wengi wabaya. Huko mbinguni, walikuwako watu wa roho wasioonekana, Shetani na malaika zake wabaya. Hapa duniani, walikuwako Kaini (Kaina) na watu wengine wengi wabaya, na watu wakubwa mno. Lakini walikuwako pia watu wazuri duniani—Habili, Henoko na Nuhu. Tutasoma habari za watu hao wote katika Sehemu ya 1 tujue yaliyotendeka.



 

Attachments

  • tembo.jpg
    tembo.jpg
    29.4 KB · Views: 978
Hadithi ya 2: Bustani Nzuri

TAZAMA dunia hii! Kila kitu ni kizuri sana! Tazama majani na miti, maua na wanyama wote. Unaweza kumjua tembo na simba hapa?
attachment.php



Bustani hii nzuri ilitokea namna gani? Na tuone Mungu alivyotuwekea dunia tayari.

Kwanza, Mungu aliumba majani mabichi yaifunike nchi. Alifanya namna zote za mimea na miti midogo. Mimea hiyo inapamba dunia. Zaidi ya hivyo, mimea mingi inatupa chakula kitamu sana.

Tena Mungu aliumba samaki waogelee katika maji na ndege waruke katika anga. Aliumba mbwa na paka na farasi; wanyama wakubwa na wadogo. Ni wanyama gani wanaokaa karibu na nyumba yenu? Je! si vizuri kufurahi kwa vile Mungu alitufanyia vyote hivyo?

Halafu, Mungu alifanya sehemu moja ya dunia kuwa ya pekee sana. Aliiita bustani ya Edeni. Ilikuwa nzuri sana. Kila kitu ndani kilikuwa kizuri. Mungu alitaka dunia nzima iwe kama bustani nzuri hii.
Lakini tazama tena picha hii ya bustani. Je! unajua kitu ambacho Mungu aliona hakipo? Tuone.
Mwanzo 1:11-25; 2:8, 9.


 
Hadithi ya 3: Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

UNAONA tofauti gani katika picha hii? Kuna watu. Mwanamume na mwanamke wa kwanza. Nani aliwaumba? Ni Mungu. Unajua jina lake? Ni Yehova. Mwanamume na mwanamke waliitwa Adamu na Hawa.

attachment.php


Yehova Mungu aliumba Adamu hivi. Alichukua mavumbi akafanya mwili mzuri wa mwanamume. Kisha akapuliza katika pua, Adamu akawa hai.
Yehova Mungu alimpa Adamu kazi ya kuwapa wanyama wote majina. Labda Adamu aliwatazama wanyama muda mrefu ili aweze kuwachagulia wote majina bora. Adamu alipokuwa akiwapa wanyama majina, aliona jambo fulani. Unajua ni jambo gani?
Wanyama wote walikuwa na wenzao. Tembo baba na mama walikuwapo, hata simba baba na mama. Lakini Adamu hakuwa na mwenzake. Basi Yehova akampa Adamu usingizi mzito, akachukua ubavu wake mmoja. Kwa ubavu huo, Yehova alimfanyia Adamu mke.
Adamu akafurahi! Wazia Hawa alivyofurahi alipowekwa katika bustani hiyo nzuri! Wangeweza kuzaa watoto wakae pamoja kwa furaha.
Yehova alitaka Adamu na Hawa wakae milele. Alitaka waifanye dunia nzima iwe nzuri kama bustani hii ya Edeni. Adamu na Hawa walifurahia sana hilo! Wewe ungependa kuifanya dunia iwe bustani nzuri? Lakini furaha ya Adamu na Hawa haikuendelea. Na tuone kwa nini.
Zaburi 83:18; Mwanzo 1:26-31; 2:7-25.

 

Attachments

  • Adamu na Hawa.jpg
    Adamu na Hawa.jpg
    24.6 KB · Views: 563
Hadithi ya 4: Sababu Walipoteza Makao Yao

TAZAMA yanayotendeka sasa. Adamu na Hawa wanafukuzwa katika bustani nzuri ya Edeni. Unajua sababu?


attachment.php



Walifanya jambo baya sana. Yehova anawaadhibu. Unajua jambo baya ambalo Adamu na Hawa walifanya?
Ni jambo ambalo Mungu aliwakataza. Mungu aliwaambia wale chakula cha miti ya bustani. Lakini si cha mti ambao Mungu aliwakataza, ili wasife. Huo ulikuwa mti wake peke yake. Tunajua ni makosa kuchukua kitu cha mtu mwingine, sivyo? Basi, kulitokea nini?
Siku moja Hawa alipokuwa peke yake katika bustani, nyoka alisema naye. Ajabu! Akamwambia Hawa ale tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. Yehova hakuumba nyoka waseme. Mtu fulani alifanya nyoka aseme. Ni nani?
Si Adamu. Ni mmoja wa watu ambao Yehova alikuwa ameumba zamani kabla ya dunia. Ni malaika ambao hatuwezi kuona. Malaika huyo mmoja akawa na kiburi sana. Alianza kuwaza kwamba ingefaa atawale kama Mungu. Alitaka watu wamtii yeye kuliko Yehova. Huyo ndiye malaika aliyemfanya nyoka aseme.
Malaika huyo alimdanganya Hawa. Alipomwambia watafanana na Mungu wakila tunda hilo, Hawa aliamini. Hawa akala, hata Adamu. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu. Ndiyo sababu walipoteza makao yao mazuri.
Lakini siku moja Mungu ataifanya dunia nzima iwe nzuri kama bustani ya Edeni. Tutajifunza namna wewe unaweza kushiriki kuifanya hivyo. Lakini sasa, tuchunguze yaliyowapata Adamu na Hawa.
Mwanzo 2:16, 17; 3:1-13, 24; Ufunuo 12:9.

 

Attachments

  • makao yao.jpg
    makao yao.jpg
    17.2 KB · Views: 462
Hadithi ya 5: Maisha ya Taabu Yanaanza

NJE ya bustani ya Edeni, Adamu na Hawa walipata taabu nyingi. Iliwapasa kufanya kazi kwa bidii wajipatie chakula. Mahali pa miti mizuri ya matunda, waliona miiba mingi inamea kuwazunguka. Ndivyo ilivyokuwa Adamu na Hawa walipokataa kumtii Mungu, wasiwe tena rafiki zake.
attachment.php




Zaidi ya hayo, Adamu na Hawa walianza kufa. Kumbuka, Mungu aliwaonya hivyo, ikiwa wangekula tunda la mti fulani. Walianza kufa siku ile ile waliyokula. Walikuwa wapumbavu sana kukataa kumsikiliza Mungu!
Watoto wote wa Adamu na Hawa walizaliwa Mungu akisha kuwafukuza wazazi wao katika bustani ya Edeni. Kwa hiyo, watoto pia wangezeeka na kufa.
Kama Adamu na Hawa wangemtii Yehova, wao na watoto wangekaa kwa furaha. Wote wangeweza kukaa duniani milele kwa furaha. Hakuna ambaye angezeeka, awe mgonjwa na kufa.
Mungu anataka watu wakae milele kwa furaha, Naye anaahidi kwamba siku moja watakaa hivyo. Dunia nzima itakuwa nzuri, hata watu wote watakuwa wenye afya. Kila mtu duniani atakuwa rafiki mzuri wa kila mtu mwingine na Mungu.

attachment.php


Lakini Hawa hakuwa tena rafiki ya Mungu. Haikuwa rahisi kwake kuzaa watoto wake. Alipata maumivu. Kukataa kumtii Yehova kulimletea huzuni nyingi, sivyo?
Adamu na Hawa wakazaa wana na binti wengi. Mwana wao wa kwanza alipozaliwa, walimwita jina Kaini. Walimwita mwana wao wa pili Habili. Walipatwa na nini? Unajua?
Mwanzo 3:16-23; 4:1, 2; Ufunuo 21:3, 4.

 

Attachments

  • maisha ya tabu.jpg
    maisha ya tabu.jpg
    9.4 KB · Views: 456
  • Yanaanza.jpg
    Yanaanza.jpg
    13.2 KB · Views: 458
Mkuu MziziMkavu, Heri ya mwaka mpya 2013 colleague,
sasa hii kitu si tuihamishe kule Habari na hoja mchanganyiko?

ahsante kutukumbusha mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Hadithi ya 6: Mwana Mzuri na Mbaya

TAZAMA Kaini na Habili sasa. Wote wawili wamekuwa wakubwa. Kaini amekuwa mkulima. Anakuza nafaka na matunda na mboga.

attachment.php


Habili amekuwa mwenye kufuga kondoo. Anapenda kuchunga kondoo wadogo. Wamekuwa kondoo wakubwa, na upesi Habili ana kundi zima la kondoo wa kuchunga.
Siku moja Kaini na Habili wanamletea Mungu zawadi. Kaini analeta chakula alichokuza. Na Habili analeta kondoo bora zaidi. Yehova anapendezwa na Habili na zawadi yake. Hapendezwi na Kaini na zawadi yake. Unajua sababu?
Si kwa sababu zawadi ya Habili ni bora kuliko ya Kaini tu. Habili ni mtu mzuri. Anampenda Yehova na ndugu yake. Kaini ni mbaya; hapendi ndugu yake.
Basi Mungu anamwambia Kaini kwamba ni lazima ageuze njia zake. Kaini anakataa. Anakasirika sana kwa sababu Mungu amempenda Habili kuliko yeye. Kwa hiyo Kaini anamwambia Habili hivi, ‘twende kule shambani.’ Halafu, wakiwa huko peke yao, Kaini anampiga Habili ndugu yake. Anampiga sana na kumwua. Kaini alifanya vibaya sana, sivyo?

attachment.php



Ijapo Habili alikufa, Mungu anamkumbuka. Habili alikuwa mtu mzuri, naye Yehova hasahau mtu kama huyo. Kwa hiyo, siku moja Yehova Mungu atamfufua Habili. Wakati huo Habili hatakufa tena. Atakaa milele hapa duniani. Je! itakuwa vizuri kujua watu kama Habili?
Lakini Mungu hapendi watu kama Kaini. Kaini alipokwisha kumwua ndugu yake, Mungu alimpa adhabu ya kumfukuzia mbali na jamaa yake. Kaini alipoondoka kukaa sehemu nyingine ya dunia, alichukua mmoja wa dada zake, akawa mke wake.
Kisha Kaini na mke wake wakaanza kuzaa watoto. Wana na binti wengine wa Adamu na Hawa waliolewa, nao wakazaa watoto. Upesi kukawa watu wengi duniani. Na tujifunze habari zao.
Mwanzo 4:2-26; 1 Yohana 3:11, 12; Yohana 11:25.

 

Attachments

  • mwana mbaya.jpg
    mwana mbaya.jpg
    18.3 KB · Views: 452
  • mwanamzuri.jpg
    mwanamzuri.jpg
    11.3 KB · Views: 439
Hadithi ya 7: Mtu Hodari

attachment.php



WATU walipoanza kuongezeka duniani, wengi wao wakafanya mabaya kama Kaini. Lakini mtu mmoja alikuwa tofauti. Ni huyu anayeitwa Henoko. Henoko alikuwa mtu hodari. Watu wote karibu yake walikuwa wakifanya mabaya, lakini Henoko aliendelea kumtumikia Mungu.
Unajua sababu wakati huo watu walifanya mabaya mengi sana? Kumbuka, Nani alifanya Adamu na Hawa wakatae kumtii Mungu kisha wakala tunda ambalo Mungu aliwakataza? Ni malaika mbaya. Biblia inamwita Shetani. Anataka kumfanya kila mtu awe mbaya.


attachment.php



Siku moja Yehova Mungu alimwagiza Henoko awaambie watu jambo fulani ambalo hawakutaka kulisikia. Ni hili: ‘Siku moja Mungu atawaharibu watu wote wabaya.’ Labda watu hao walikasirika sana kwa kusikia hayo. Labda hata walitaka kumwua Henoko. Hivyo ilimpasa Henoko awe hodari sana ili awaambie watu hao jambo ambalo Mungu alikusudia kufanya.
Mungu hakumwacha Henoko akae muda mrefu kati ya watu hao wabaya. Henoko alikaa miaka 365 tu. Kwa nini twasema “miaka 365 tu”? Kwa sababu watu wa siku hizo walikuwa wenye nguvu nyingi kuliko watu wa sasa. Nao walikaa muda mrefu zaidi. Methusela mwana wa Henoko alikaa miaka 969!

attachment.php



Basi, Henoko alipokufa, watu walizidi kuwa wabaya sana. Biblia yasema kwamba ‘kila jambo walilowaza lilikuwa baya wakati wote,’ na kwamba ‘dunia ikajaa jeuri.’
Unajua sababu moja kwa nini kulikuwako matata mengi sana duniani siku hizo? Shetani alipata njia mpya ya kufanya watu watende mabaya. Tutajifunza hayo katika hadithi inayofuata.
Mwanzo 5:21-24, 27; 6:5; Waebrania 11:5; Yuda 14, 15.


 

Attachments

  • mtu hodari.jpg
    mtu hodari.jpg
    5.5 KB · Views: 418
  • mtu wa hodari mbaya.jpg
    mtu wa hodari mbaya.jpg
    13.8 KB · Views: 433
  • mtu wa hodari mbaya zaidi.jpg
    mtu wa hodari mbaya zaidi.jpg
    18.1 KB · Views: 419
[h=1]Hadithi ya 8: Watu Wakubwa Mno Duniani[/h]IKIWA mtu angekuwa akikaribia kwako naye ni mrefu sana kama dari ya nyumba yenu, ungeona namna gani? Mtu huyo angekuwa mkubwa mno! Wakati mmoja kulikuwa watu wakubwa mno duniani. Biblia inaonyesha kwamba baba zao ni malaika waliotoka mbinguni. Lakini ilikuwa namna gani?
08.jpg

Kumbuka, Shetani malaika mbaya alikuwa akifanya matata. Hata alikuwa akigeuza malaika wa Mungu wawe wabaya. Mwishowe, malaika wengine walianza kumsikiliza Shetani. Waliacha kufanya kazi waliyopewa na Mungu huko mbinguni. Wakaja duniani na kujivika miili ya kibinadamu. Unajua sababu?
Biblia yasema wana hao wa Mungu waliona wanawake wazuri duniani wakataka kukaa pamoja nao. Kwa hiyo, wakaja duniani kuoa wanawake hao. Biblia inasema hilo lilikuwa kosa, kwa sababu Mungu aliumba malaika wakae mbinguni.
Malaika hao na wake zao walipozaa watoto, watoto hao walikuwa tofauti. Kwanza labda hawakuonekana tofauti sana lakini walizidi kuwa wakubwa na nguvu sana, mpaka wakawa wakubwa mno.
Watu hao walikuwa wabaya. Na kwa vile walivyokuwa wakubwa mno na nguvu sana, waliumiza watu. Walijaribu kumlazimisha kila mtu awe mbaya kama wao.
Henoko alikuwa amekufa, lakini sasa kulikuwako mtu mmoja duniani aliyekuwa mzuri. Mtu huyo ni Nuhu. Sikuzote alifanya mapenzi ya Mungu.
Wakati mmoja Mungu alimwambia Nuhu kwamba wakati wake umefika wa kuharibu watu wote wabaya. Lakini Mungu alitaka kumwokoa Nuhu, jamaa yake na wanyama fulani wengi. Na tuone namna Mungu alivyofanya hivyo.
Mwanzo 6:1-8; Yuda 6.
 
Hadithi ya 9: Nuhu Ajenga Safina

attachment.php



NUHU alikuwa na mke na wana watatu. Wana hao ni Shemu, Hamu na Yafeti. Kila mmoja wao alikuwa na mke. Kwa hiyo, jamaa ya Nuhu ilikuwa yenye watu nane.
Mungu akamwagiza Nuhu afanye jambo geni. Alimwambia ajenge safina kubwa. Safina hiyo ilikuwa kubwa kama meli, lakini ilionekana kama sanduku kubwa, refu. ‘Fanya iwe urefu wa vyumba vitatu kwenda juu,’ Mungu akasema, ‘uweke vyumba ndani yake.’ Vyumba hivyo vilikuwa vya Nuhu na jamaa yake, wanyama, na chakula chao.
Tena Mungu akamwambia Nuhu aikaze safina hiyo ili maji yasiweze kuingia. Mungu akasema: ‘Nitaleta gharika kubwa iharibu ulimwengu mzima. Kila mtu nje ya safina atakufa.
Nuhu na wanawe walimtii Yehova wakaanza kujenga safina. Lakini watu wengine walikuwa wakicheka tu. Walizidi kuwa wabaya.

attachment.php

Kujenga safina kulichukua muda mrefu kwa sababu ilikuwa kubwa mno. Baada ya miaka mingi, ikamalizika. Kisha Mungu akamwambia Nuhu aingize wanyama katika safina. Tena Mungu alimwambia Nuhu aingize namna zote mbalimbali za ndege. Nuhu akafanya kama Mungu alivyosema.
Kisha, Nuhu na jamaa yake wakaingia katika safina. Ndipo Mungu akaufunga mlango. Nuhu na jamaa yake walingoja humo ndani. Je! kweli gharika ingekuja kama vile Mungu alivyosema?
Mwanzo 6:9-22; 7:1-9.

 

Attachments

  • Nabii Nuhu A.S..jpg
    Nabii Nuhu A.S..jpg
    14.7 KB · Views: 425
  • wanyama.jpg
    wanyama.jpg
    14 KB · Views: 419
[h=1]Hadithi ya 10: Gharika Kuu[/h]NJE ya safina, watu walikaa kama zamani. Bado hawakuamini kwamba Gharika ingekuja. Walicheka wee, wakacheka sana. Lakini upesi waliacha kucheka.
10a.jpg

Mara moja maji yakaanza kuanguka. Yalimwagika kutoka angani kama vile unapomwaga maji kutoka ndoo. Nuhu alikuwa amesema kweli! Lakini sasa ilikuwa kuchelewa mno ye yote kuingia katika safina. Yehova alikuwa amefunga mlango sana.
Upesi mabonde yote yakafunikwa. Maji yakawa kama mito mikubwa. Yakaangusha miti na kupindua-pindua mawe makubwa, na kufanya kelele nyingi. Watu waliogopa. Wakapanda sehemu zilizoinuka zaidi. Afadhali wangemsikiliza Nuhu na kuingia katika safina mlango ulipokuwa bado kufungwa! Lakini sasa walichelewa mno.
Maji yakazidi kupanda juu sana. Siku 40 mchana na usiku maji yalimwagika kutoka angani. Yalifika hata kwenye vilele vya milima. Upesi hata vilele vya milima mirefu zaidi vilifunikwa kwa maji. Kama Mungu alivyokuwa amesema, watu na wanyama wote waliokuwa nje ya safina wakafa. Lakini kila aliyekuwa ndani alikuwa salama.
Nuhu na wanawe walikuwa wamefanya kazi nzuri ya kujenga safina. Maji yaliinua safina juu, ikaelea juu ya maji. Kisha siku moja, mvua ilipoacha kunya, jua lilianza kung'aa. Lo! maono gani! Kila mahali palikuwa bahari kuu moja. Safina peke yake ndiyo ilionekana ikielea juu ya maji.
10.jpg

Wale watu wakubwa mno walipotea. Hawakuonekana tena waumize watu. Wote pamoja na mama zao na watu wengine wabaya, walikuwa wamekufa. Namna gani baba zao?
Baba zao hawakuwa wanadamu kama sisi. Ni malaika waliokuwa wameshuka wakae duniani. Basi Gharika ilipokuja, hawakufa pamoja na watu wengine. Walivua miili ya kibinadamu wakarudi mbinguni wakiwa malaika. Lakini hawakuruhusiwa tena katika jamaa ya malaika wa Mungu. Wakawa malaika wa Shetani. Katika Biblia wanaitwa mashetani.
Basi Mungu alileta upepo, nayo maji ya Gharika yakaanza kupunguka. Miezi mitano ilipopita, safina hiyo ilisimama juu ya mlima. Zilipopita siku nyingi zaidi, wale waliokuwa katika safina walitazama nje wakaona vilele vya milima. Maji hayo yakazidi kupunguka.
Kisha Nuhu akamtoa kunguru katika safina. Kwa sababu hakuona mahali pa kusimama, alikuwa akiruka-ruka akienda na kurudi. Alizidi kufanya hivyo akirudi kila wakati, akisimama juu ya safina.
10b.jpg

Nuhu alitaka kuona kama maji yamekauka duniani. Basi baada ya hapo alimtoa njiwa kutoka safina. Lakini njiwa huyo pia alirudi kwa sababu hakuona mahali pa kukaa. Nuhu alimtuma tena mara ya pili, akarudi akiwa na jani la mzeituni katika mdomo wake. Ndipo Nuhu alijua kwamba maji hayo yamekauka. Kisha Nuhu alimtuma tena njiwa mara ya tatu, mwishowe aliona mahali pakavu pa kukaa.
Ndipo Mungu akasema na Nuhu. Akamwambia: ‘Toka katika safina. Chukua jamaa yako yote na wanyama.' Walikuwa wamekaa ndani ya safina muda wa zaidi ya mwaka mmoja. Tunafikiri wote walifurahi sana kutoka nje tena wakiwa hai!
Mwanzo 7:10-24; 8:1-17; 1 Petro 3:19, 20.


 
[h=1]Sehemu 2: Gharika Mpaka Kukombolewa Katika Misri[/h]Watu wanane peke yao ndio waliookoka Gharika, lakini baadaye wakaongezeka kuwa maelfu mengi. Kisha, ilipopita miaka 352 baada ya Gharika, Abrahamu akazaliwa. Tunajifuzna namna Mungu alivyotimiza ahadi yake kwa kumpa Abrahamu mwana anayeitwa Isaka. Kisha, kati ya wana wawili wa Isaka, Yakobo alichaguliwa na Mungu.
Yakobo alikuwa na jamaa kubwa ya wana 12 na binti fulani. Wana 10 wa Yakobo walimchukia ndugu yao mdogo Yusufu wakamwuza utumwani huko misri. Baadaye, Yusufu akawa mtawala mkuu wa Misri. Njaa kuu ilipotokea, Yusufu aliwajaribu ndugu zake aone kama wamegeuza moyo. Halafu, jamaa yote ya Yakobo, yaani, Waisraeli, wakahamia Misri. Hayo yalitokea miaka 290 baada ya kuzaliwa Abrahamu.
Kwa miaka 215 iliyofuata Waisraeli walikaa huko Misri. Yusufu alipokufa, wakawa watumwa huko. Mwishowe, Musa akazaliwa, naye Mungu akamtumia awakomboe Waisraeli kutoka Misri. Kwa jumla, miaka 857 ya historia inazungumzwa katika Sehemu ya 2.
25.jpg

 
Hadithi ya 11: Upinde wa Mvua wa Kwanza

UNAJUA jambo la kwanza ambalo Nuhu alifanya wakati yeye na jamaa yake walipotoka katika safina? Alimtolea Mungu zawadi. Unaweza kumwona akifanya hivyo katika picha iliyo chini. Nuhu alitoa zawadi hiyo ya wanyama ili amshukuru Mungu kwa kuokoa jamaa yake katika gharika kuu.
11a.jpg

Unadhani Yehova alipendezwa na zawadi hiyo? Ndiyo. Alimwahidi Nuhu kwamba hangeuharibu ulimwengu tena kwa gharika.
Upesi nchi yote ikakauka, Nuhu na jamaa yake wakaanza kuishi tena nje ya safina. Mungu akawabarikia na kuwaambia: ‘Zaeni watoto wengi. Mwongezeke mpaka watu waishi pote duniani.'
Lakini baadaye, labda watu wangeogopa kwamba gharika kama hiyo ingetokea tena. Basi Mungu alitoa kitu cha kukumbusha watu ahadi yake kwamba hataifunika tena dunia yote kwa maji. Unajua ni kitu gani? Upinde wa mvua.
11.jpg

Umepata kuuona? Unaona mmoja katika picha hii?
Mungu aliahidi hivi: ‘Watu wote na wanyama hawataharibiwa tena kwa gharika. Ninaweka upinde wangu wa mvua katika mawingu. Upinde wa mvua utakapoonekana, nitauona nikumbuke ahadi yangu.'
Basi unapoona upinde wa mvua, unakukumbusha nini? Ahadi ya Mungu kwamba hatauharibu ulimwengu tena kwa gharika kuu.
Mwanzo 8:18-22; 9:9-17.


ETAENDELEA BAADAE............
 
Hadithi ya 12: Watu Wanajenga Mnara Mkubwa

IKAPITA miaka mingi. Wana wa Nuhu wakazaa watoto wengi. Watoto wao walikua na kuzaa watoto zaidi. Upesi kukawa na watu wengi duniani.
Mmoja wa watu hao alikuwa kijukuu wa Nuhu jina lake Nimrodi. Alikuwa mtu mbaya aliyewinda na kuua wanyama na hata wanadamu. Nimrodi pia alijifanya mfalme atawale watu wengine. Mungu hakumpenda Nimrodi.

Wakati huo watu wote walisema lugha moja. Nimrodi alitaka awakusanye wote ili awatawale. Unajua alilofanya? Aliwaambia watu wajenge mji na ndani yake mnara mkubwa. Watazame katika picha hii wakitengeneza matofali.

Yehova Mungu hakupendezwa na jengo hilo. Mungu alitaka watu watawanyike na kukaa pote duniani. Lakini wao walisema: ‘Njoni! Tujenge mji na mnara mrefu sana ufike mbinguni. Ndipo tutasifiwa sana!’ Watu hao walitaka wajiheshimu kuliko Mungu.

Kwa hiyo Mungu aliwaachisha kujenga mnara. Unajua namna alivyofanya? Aliwafanya waanze kusema lugha mbalimbali mara moja. Wajenzi hao hawakufahamiana tena. Ndiyo sababu mji wao ukaitwa Babeli, au Babiloni, maana yake “Mchafuko.”
Basi watu hao walianza kuondoka Babeli. Vikundi vya watu waliosema lugha moja vilikwenda kukaa pamoja sehemu nyingine za dunia.
Mwanzo 10:1, 8-10; 11:1-9.
12.jpg



Hadithi ya 13: Ibrahimu—Rafiki ya Mungu

MAHALI pamoja ambapo watu walikaa baada ya Gharika ni Uru. Pakawa mji wa maana wenye nyumba nzuri. Lakini watu wa huko waliabudu miungu ya uongo. Ndivyo walivyofanya hata katika Babeli. Watu wa Uru na Babeli hawakuwa kama Nuhu na Shemu mwanawe, waliozidi kumtumikia Yehova.
Mwishowe, ilipopita miaka 350 tangu gharika, Nuhu mwaminifu akafa. Ilipopita miaka miwili mtu unayemwona katika picha hii alizaliwa. Alikuwa mtu wa pekee sana kwa Mungu. Jina lake ni Ibrahimu. Alikaa pamoja na jamaa yake katika mji huo wa Uru.
13.jpg


Siku moja Yehova alimwambia Ibrahimu (Abrahamu): ‘Ondoka Uru, wewe na ukoo wako, uende kwenye nchi ambayo nitakuonyesha.’ Je! Ibrahimu alimtii Mungu na kuacha starehe zote za Uru? Ndiyo. Ibrahimu alijulikana kuwa rafiki ya Mungu kwa sababu alimtii Mungu sikuzote.

Wengine wa jamaa ya Ibrahimu walimfuata alipoondoka Uru. Tera baba yake alimfuata. Hata Lutu mpwa wake. Na pia Sara mke wa Ibrahimu. Halafu wote wakafika Harani, na huko Tera akafa. Walikuwa mbali sana na Uru.

Muda kidogo Ibrahimu na jamaa yake wakaondoka Harani kuja Kanaani. Yehova akasema: “Hii ndiyo nchi nitakayowapa watoto wako.’ Ibrahimu alikaa Kanaani katika hema.

Mungu alianza kumsaidia Ibrahimu hata akawa na kondoo na wanyama wengine wengi na mamia ya watumishi. Lakini yeye pamoja na Sara hawakuwa na watoto wowote.
Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 99, Yehova alimwahidi hivi: ‘Utakuwa baba ya mataifa mengi.’ Lakini watoto wangezaliwa namna gani, maana Ibrahimu na Sara ni wazee mno?
Mwanzo 11:27-32; 12:1-7; 17:1-8, 15-17; 18:9-19.
 
Hadithi ya 14: Mungu Anajaribu Imani ya Ibrahimu

UNAWEZA kuona Ibrahimu anafanya nini hapa? Ana kisu, ni kama anataka kumwua mwanawe. Kwa nini afanye hivyo? Na tuone kwanza namna Ibrahimu na Sara walivyopata mwana wao.
14.jpg


Kumbuka, Mungu aliwaahidi kwamba wangezaa mwana. Lakini lilikuwa jambo gumu, kwa sababu Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana. Lakini Ibrahimu aliamini kwamba Mungu anaweza kufanya jambo gumu. Basi jambo gani lilitokea?
Mungu alipokwisha kutoa ahadi yake, mwaka mzima ukapita. Ndipo, Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 100 na Sara 90, wakazaa mtoto wa kiume jina lake Isaka. Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake!

Lakini
Ismael alipokuwa mtu mzima, Yehova alijaribu imani ya Ibrahimu. Akasema: ‘Mchukue mwana wako Ismael uende kwenye mlima ambao nitakuonyesha. Ukamwue huko mwana wako umtoe dhabihu.’ Lakini kumbuka, Mungu alikuwa ameahidi kwamba watoto wa Ibrahimu wangekaa

Kanaani. Ingekuwa namna gani kama
Ismael angekufa? Ibrahimu hakufahamu hilo, lakini alimtii Mungu.
Alipofika kwenye mlima, Ibrahimu alimfunga
Ismael na kumweka juu ya madhabahu aliyojenga. Lakini alipotaka kumwua Ismael, malaika wa Mungu alitoa sauti kubwa: ‘Ibrahimu, usimwumize mtoto wala kumfanya lolote. Sasa najua kwamba unaniamini, kwa sababu hukuninyima mwana wako mmoja tu!’
Lo! Ibrahimu alimwamini Mungu sana! Aliamini kwamba hakuna jambo gumu kwa Yehova, hata angemfufua
Ismael katika wafu. Lakini Mungu hakutaka Ibrahimu amwue Isaka. Basi Mungu aliongoza kondoo akamatwe na miti midogo iliyokuwa karibu. Kisha akamwambia Ibrahimu amtoe kondoo huyo awe dhabihu mahali pa mwana wake.
Mwanzo 21:1-7; 22:1-18.
 
[h=1]Hadithi ya 15: Mke wa Lutu Alitazama Nyuma[/h]LUTU na jamaa yake walikaa Kanaani pamoja na Ibrahimu. Siku moja Ibrahimu alimwambia Lutu hivi: ‘Hapa hapana nchi ya kufaa wanyama wetu wote. Tafadhali, tutengane. Ukienda huku, na mimi nitakwenda kule.'
Lutu akaitazama nchi. Akaona sehemu ya nchi iliyo nzuri sana yenye maji na majani mazuri mengi ya wanyama wake. Hiyo ilikuwa Wilaya ya Yordani. Basi Lutu alipeleka jamaa yake na wanyama huko. Mwishowe wakakaa katika mji wa Sodoma.
Watu wa Sodoma walikuwa wabaya sana. Lutu alisumbuliwa, maana alikuwa mtu mzuri. Hata Mungu alisumbuliwa. Mwishowe, Mungu alituma malaika wawili wakamwonye Lutu kwamba Mungu ataharibu Sodoma, na Gomora mji wa karibu, maana ni miji mibaya.
Malaika hao wakamwambia Lutu hivi: ‘Fanya haraka! Chukua mke wako na binti zako wawili mwondoke huku!' Malaika mmoja alisema: ‘Kimbieni mponye uhai wenu! Msitazame nyuma. Kimbieni kwenye milima msiuawe.'
Lutu na binti zake walitii, wakatoka Sodoma. Lakini mke wa Lutu hakutii. Walipokwisha kutembea mwendo fulani kutoka Sodoma, mke alisimama akatazama nyuma, akawa nguzo ya chumvi. Unaweza kumwona katika picha?
Tunaweza kujifunza somo zuri kwa hayo. Yanatuonyesha kwamba Mungu anaokoa wale wanaomtii, lakini wale wasiomtii watapoteza uhai wao.
Mwanzo 13:5-13; 18:20-33; 19:1-29; Luka 17:28-32; 2 Petro 2:6-8.
15.jpg




[h=1]Hadithi ya 16: Isaka Anapata Mke Mzuri[/h]JE! UNAJUA mwanamke aliye katika picha hii? Jina lake ni Rebeka. Na mwanamume anayekutana naye ni Isaka. Atakuwa mke wake. Ilikuwa namna gani?
Ilikuwa hivi, Ibrahimu baba ya Isaka alitaka kumtafutia mwana wake mke mzuri. Hakutaka Isaka aoe mwanamke wa Kanaani, kwa sababu watu hao waliabudu miungu ya uongo. Ibrahimu akamwambia mtumishi wake: Nenda Harani, kwa ukoo wangu ukamtafutie Isaka, mwanangu, mke.'
Mara hiyo mtumishi wa Ibrahimu akachukua ngamia kumi akaanza safari ndefu. Alipofika karibu na ukoo wa Ibrahimu, alisimama penye kisima. Ilikuwa jioni, wakati wanawake wa mji wanapokuja kuteka maji katika kisima. Basi mtumishi wa Ibrahimu alimwomba Yehova hivi: ‘Mwanamke atakayeteka maji na kunipa mimi na ngamia, na awe ndiye umechagua kuwa mke wa Isaka.''
16.jpg

Upesi Rebeka akaja kuteka maji. Mtumishi huyo alipomwomba maji ya kunywa akampa. Kisha akaenda kuchota ya kutosha ngamia wenye kiu. Ilikuwa kazi ngumu maana ngamia wanakunywa maji mengi sana.
Rebeka alipomaliza, mtumishi wa Ibrahimu alimwuliza jina la baba yake. Akamwuliza hata kama angeweza kulala kwao usiku huo. Alijibu: ‘Baba yangu ni Betueli, kuna nafasi yako kukaa pamoja na sisi.' Mtumishi wa Ibrahimu alijua Betueli ni mwana wa Nahori ndugu ya Ibrahimu. Basi alipiga magoti akamshukuru Yehova kwa kumwelekeza kwenye ukoo wa Ibrahimu.
Usiku huo mtumishi wa Ibrahimu aliwaambia Betueli na Labani ndugu ya Rebeka sababu iliyompeleka huko. Wote wawili wakakubali Rebeka aende naye akaolewe na Isaka. Rebeka alijibu nini alipoulizwa? Alikubali. Halafu kesho yake wakapanda ngamia wakisafiri sana kurudi Kanaani.
Walipofika jioni, Rebeka akamwona mwanamume akitembea shambani. Ni Isaka. Alifurahi kumwona Rebeka. Sara mama yake alikuwa amekufa miaka mitatu iliyopita, naye alikuwa bado amehuzunika. Isaka sasa akampenda sana Rebeka, akawa na furaha tena.
Mwanzo 24:1-67.
 
Hadithi ya 17: Mapacha Waliokuwa Tofauti

17.jpg

WAVULANA wawili hapa ni tofauti sana, sivyo? Unajua majina yao? Yule mwindaji ni Esau, na yule anayechunga kondoo ni Yakobo.
Esau na Yakobo walikuwa mapacha wa Isaka na Rebeka. Isaka baba yao, alimpenda sana Esau, kwa sababu alikuwa mwindaji mzuri naye aliiletea jamaa chakula. Lakini Rebeka alimpenda sana Yakobo, kwa sababu alikuwa mtulivu, mwenye amani.
Ibrahimu babu yao alikuwa bado hai. Tunaweza kuwaza namna Yakobo alivyopenda kumsikiliza akisema habari za Yehova. Mwishowe Ibrahimu akafa akiwa mwenye miaka 175, mapacha hao walipokuwa wenye miaka 15.
Esau alipokuwa mwenye miaka 40 alioa wanawake wawili kutoka nchi ya Kanaani. Hilo lilihuzunisha sana Isaka na Rebeka, kwa sababu wanawake hao hawakumwabudu Yehova.
Ikawa siku moja Esau akamkasirikia sana Yakobo ndugu yake. Ulifika wakati Isaka alipotaka kumbariki mwanawe mkubwa. Kwa kuwa Esau alikuwa mkubwa kuliko Yakobo, Esau alitazamia kupokea baraka hiyo. Lakini Esau alikuwa amekwisha kumwuzia Yakobo haki hiyo ya kupokea baraka. Pia, wavulana hao wawili walipozaliwa Mungu alikuwa amesema kwamba Yakobo angepokea baraka hiyo. Na ndivyo ilivyokuwa. Isaka alimpa Yakobo mwanawe baraka hiyo.
17a.jpg

Baadaye, Esau alipojua hivyo akamkasirikia sana Yakobo. Alikasirika sana hata akasema angemwua Yakobo. Rebeka aliposikia hayo, alisumbuka sana. Basi akamwambia Isaka mume wake hivi: ‘ltakuwa vibaya sana ikiwa Yakobo pia anaoa mwanamke Mkanaani.’
Kisha Isaka akamwita Yakobo mwanawe akamwambia hivi: ‘Usioe mwanamke wa kutoka Kanaani. Nenda kwenye nyumba ya babu yako Betueli katika Harani. Oa mmoja wa binti za Labani mwanawe.’
Yakobo akamsikiliza baba yake, na mara hiyo akaanza safari yake ndefu kwenda kwa watu wake wa ukoo huko Harani.
Mwanzo 25:5-11, 20-34; 26:34, 35; 27:1-46; 28:1-5; Waebrania 12:16, 17.
 
[h=1]Hadithi ya 18: Yakobo Anakwenda HaraniUNAWAJUA wanaume hawa ambao Yakobo anazungumza nao? Akiisha kusafiri siku nyingi, Yakobo alikutana nao penye kisima. Walikuwa wakichunga kondoo zao. Yakobo akauliza: ‘Mnatoka wapi?'
‘Harani,' wakasema.
‘Mnamjua Labani?' Yakobo akauliza.
‘Ndiyo,' wakajibu. ‘Tazama anakuja Raheli binti yake akiwa na kondoo zake.' Unamwona Raheli (Rakeli) yule anakuja kutoka mbali?
18.jpg

Yakobo alipomwona Raheli akiwa na kondoo za mjomba wake, alikwenda kuondoa jiwe katika kisima ili kondoo wanywe maji. Kisha Yakobo akambusu Raheli na kujijulisha kwake. Raheli alifurahi sana, akaenda nyumbani kumwambia Labani baba yake.
Labani alifurahi sana Yakobo akae naye. Yakobo alipoomba kumwoa Raheli, Labani alifurahi. Lakini, alimwomba Yakobo afanye kazi katika shamba lake miaka 7 ili apewe Raheli. Yakobo alifanya hivyo kwa sababu alimpenda sana Raheli. Lakini ulipofika wakati wa arusi, unajua ilivyokuwa?
Labani alimpa Yakobo Lea binti yake mkubwa badala ya Raheli. Yakobo alipokubali kumfanyia Labani kazi muda wa miaka mingine saba, Labani alimpa Raheli pia awe mke wake. Siku hizo Mungu aliruhusu wanaume wawe na wake wengi. Lakini sasa, kama Biblia inavyoonyesha, imempasa mwanamume awe na mke mmoja tu.
Mwanzo 29:1-30.



[/h]
 
[h=1]Hadithi ya 19: Yakobo Ana Jamaa Kubwa[/h]
19.jpg

EBU tazama jamaa hii kubwa. Hawa ni wana 12 wa Yakobo. Ana binti pia. Unajua majina ya watoto hao? Na tujifunze majina yao.
Lea alizaa Reubeni, Simeoni, Levi na Yuda. Raheli alipoona kwamba hakuzaa watoto, alihuzunika. Basi akampa Yakobo Bilha, mtumishi wake naye Bilha akazaa wana wawili walioitwa Dani na Naftali. Kisha Lea pia akampa Yakobo Zilpa mtumishi wake, naye Zilpa akazaa Gadi na Asheri. Mwishowe Lea akazaa wana wengine wawili, Isakari na Zebuloni.
Halafu Raheli alizaa mtoto. Akamwita jina Yusufu. Baadaye tutajifunza mengi juu ya Yusufu, kwa sababu akawa mtu mkubwa sana. Hao ndio wana 11 wa Yakobo alipokuwa anakaa na Labani baba ya Raheli.
Yakobo pia alikuwa na mabinti fulani, lakini Biblia inataja jina la mmoja tu, Dina.
Ukafika wakati ambapo Yakobo aliamua kumwacha Labani, arudi Kanaani. Akakusanya jamaa yake kubwa na kondoo wake wengi na ng'ombe, akaanza safari ndefu.
Muda kidogo Yakobo na jamaa yake waliporudi Kanaani, Raheli alizaa mwana mwingine. Alizaa walipokuwa katika safari. Raheli alipata taabu kisha akafa alipokuwa akizaa. Lakini mtoto huyo mchanga alipona. Yakobo akamwita jina Benyamini.
Tunataka tuyakumbuke majina ya wana 12 wa Yakobo kwa sababu taifa zima la Israeli lilitokana nao. Makabila 12 ya Israeli yanaitwa kwa majina ya wana 10 wa Yakobo na wana wawili wa Yusufu. Isaka alikaa miaka mingi baada ya kuzaliwa watoto hao wote wa kiume, na bila shaka alifurahi sana kuwa na wajukuu wengi sana. Lakini na tuone yaliyompata Dina, mjukuu wake.
Mwanzo 29:32-35; 30:1-26; 35:16-19; 37:35.


 
Hadithi ya 20: Dina Anaingia Katika Taabu UNAONA Dina anaenda kutembela nani? Ni wasichana wanaokaa Kanaani. Je! Yakobo baba yake atafurahia? Ili uweze kujibu ulizo hilo, jaribu kukumbuka Ibrahimu na Isaka walivyofikiria wanawake wa Kanaani.

attachment.php



Je! Ibrahimu alitaka Isaka aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Je! Isaka na Rebeka walitaka Yakobo aoe msichana wa Kanaani? Sivyo. Unajua sababu yake?
Ni kwa sababu watu hao wa Kanaani waliabudu miungu ya uongo. Hawakufaa kuwa waume na wake, nao hawakufaa kuwa

rafiki wa kushirikiana nao. Basi tunaweza kuwa na hakika kwamba Yakobo hangependezwa na urafiki wa binti yake pamoja na wasichana hao Wakanaani.
Bila shaka, Dina aliingia katika taabu. Je! unamwona mwanamume huyo Mkanaani katika picha anayemtazama Dina? Ni

Shekemu. Siku moja Dian alipokuwa akitembelea, Shekemu alimchukua na kumlazimisha alale naye. Hilo lilikuwa kosa, kwa sababu ni wanaume na wanawake waliooana tu ndio wanaotakiwa kulala pamoja. Ubaya huo ambao Shekemu alimtendea Dina uliongoza kwenye taabu nyingi zaidi.

Ndugu zake Dina waliposikia yaliyotokea, walikasirika sana. Simeoni na Levi, walikasirika sana hata wakachukua panga wakaingia mjini na kuwafikia wanaume hao ghafula. Wao na ndugu zao wakamwua Shekemu na wanaume wengine wote.

Yakobo alikasirika kwa sababu wanawe walifanya ubaya huo.
Taabu yote hiyo ilianza namna gani? Ni kwa sababu Dina alifanya urafiki na watu ambao hawakutii sheria za Mungu. Hatutaki tufanye urafiki na watu kama hao, sivyo?
Mwanzo 34:1-31.



 

Attachments

  • DINA.jpg
    DINA.jpg
    54.8 KB · Views: 167
Back
Top Bottom