Second selection Kidato cha Tano 2015/2016

Second selection Kidato cha Tano 2015/2016

jamani wakuu! mimi nimechaguliwa kimamba secondary comb PCB je? kama kuna mtu anayeijua anipe taarifa na jinsi ya kupata join instruction! msaada wenu wakuu
 
Jaman Wadau Naomba Mniangalizie Hili Jina Kama Amebadilishiwa Shule Emanuel Ngoko Shule Aliyopo Sas Inaitwa Ileje ,msaada Wakuu
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA
WANAFUNZI WALIOBADILISHIWA SHULE, TAHASUSI NA
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA
PILI 2015
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya uchaguzi
wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili 2015 ambapo
wanafunzi 4775 (Wavulana 3,211 na Wasichana 1,564) wamechaguliwa . Aidha,
wanafunzi wote 305 walioomba kubadilisha shule na tahasusi (sanaa kwenda
sayansi) wamebadilishiwa. Uchaguzi na mabadiliko hayo umezingatia nafasi
zilizopatikana baada ya baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa awamu ya kwanza
kushindwa kuripoti. Wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe
14/09/2015 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 28/09/2015.
Kwa tangazo hili Wakuu wa shule mnatakiwa kuwaruhusu kuondoka/
kuwapokea wanafunzi waliopangwa au kubadilishiwa shule/tahasusi bila
pingamizi lolote. Wazazi/Walezi mnashauriwa kuwasaidia wanafunzi ambao
wamebadilishiwa shule. Aidha, wanafunzi ambao wameridhika na tahasusi
wanazosoma kabla ya tangazo hili wasilazimishwe kuondoka.
Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI
11 SEPTEMBA, 2015

walisema ni wanafunzi zaidi ya elfu 9 nashangaa kuona wamechaguliwa elfu 4? Duu kweli hi ndo Tz
 
Back
Top Bottom