Screw Wahisani and those who can't act without 'em! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Screw Wahisani and those who can't act without 'em!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 29, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Festo Polea (Mwananchi)


  SERIKALI ipo katika mazungumzo na wahisani ili kuweza kupanua barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kwa kiwango cha njia mbili zitakazosaidia kurahisisha usafiri na kuondokana na ajali zisizo za lazima.

  Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Ruvu mkoani Pwani, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu iliyopo Ruvu Darajani.  Alisema ajali nyingi zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembamba wa barabara hiyo kama inavyofikiriwa, bali zinatokana na uzembe wa madereva ambapo wengi wao wameonekana wakiendesha kwa kukiuka kanuni za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupita kiasi, kulewa na madereva wengine hupitiwa na usingizi wakiwa waneendesha magari.
  Dk Kawambwa amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea ajali mbaya katika eneo la Kibamba Darajani jijini Dar es Salaam, ambako watu 10 akiwamo mama mjamzito aliyepasuka tumbo, walifariki dunia papo hapo baada ya lori la mafuta kuiangukia daladala.
  “Wembamba wa eneo ilipotokea ajali ya juzi na kuua watu wote kwenye daladala ni changamoto kwa serikali kutanua barabara hiyo, lakini ajali zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembbama wa barabara, kwani ajali zinazotokea katika eneo hilo zinatokana na uzembe wa madereva,’’ alisema Dk Kawambwa.
  Akizungumzia kuhusiana na mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu na utaanzia kutanua eneo la Mwenge hadi Tegeta kwa ngazi ya njia mbili za kuingia na kutoka ili kusaidia kuondokana na msongamano wa magari katika barabara hiyo.
  “Tunajua tutapata changamoto kubwa kwa wananchi waliojenga kandokando ya barabara hizo tunazotaka kuzitanua, lakini tutajitahidi kwenda na wakati kwa kuendelea na ujenzi huo huku mazungumzo na wananchi hao katika maeneo mengine ambayo yatakuwa bado hatujayafikia yakiendelea ili kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa kwa kiwango cha njia mbili,’’ alisema Dk Kawambwa.  Pia Dk Kawambwa alisema ili kuondokana na tatizo kubwa la msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam, kupitia mradi wa kutanua barabara 10 za jiji hilo la Dar es Salaam utafanyika kwa lengo la kurahisisha usafiri katikati ya jiji hilo.

  Alisema mradi huo utafanya kazi kwa kutumia barabara tofauti na zilizo zoeleka katika usafiri wa daladala kama barabara ya Morogoro na Mandela.  “Tunatarajia kutumia njia nyingine na hazitamlazimisha dereva kutumia barabara moja ya Morogoro ili afike Posta ama Ubungo bali ataweza kupita ya kutokea Kigogo na kumuwezesha kufika ubungo ama Posta hiyo ikiwa ni malengo ya kuondokana na msongamano wa foleni katika barabara hizo.  Aliongeza kuwa mradi huo pia utasaidia kuondoa mrundikano wa malori kuwa katika foleni moja na magari madogo hasa katika barabara ya Jangwani, ambapo imeonekana malori yakiitumia pamoja na magari mengine madogo ambapo mradi huo ukianza malori na magari mengine hayatakuwa katika barabara moja.

  My Take:
  Read the heading! halafu kama ajali hazitokani na wembamba wa barabara kwanini mnataka kuzipanua? HIvi hawa wahisani wametushikia nini kwenye vichwa vyetu kiasi kwamba hatuwezi kufikiri mpango mzuri wa maendeleo au kufanya mambo ambayo tunajua tuna uwezo wa kuyafanya pasipo wao?

  Nimesoma juzi ati mamlaka ya maji taka huko Mbeya na wenyewe wanasubiri fedha za Wahisani ili kusaidia kujenga vyoo vya kisasa katika shule mbalimbali mkoani humo. Gharama ya mradi wote huo ni kama shilingi milioni 300 hivi!
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  ...and screw 'em tripo9 times!
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa nini hawazungumzi na wahisani kuhusu shule zetu za msingi na sekondari, mahakama zetu za mwanzo, vituo vyetu vya polisi, zahanati zetu, mambo ni mabaya zaidi huko kuliko hiyo barabara wanayotaka kuipanua.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Lazma kuwe na mkakati wa kupata fedha na kupanga miradi yetu wenyewe. Rasilimali mnawapa wageni kwa bei chee mnategema mtatoa wapi pesa ya kujenga barabara? Tena barabara zenyewe wanajenga wachina, wanachuma tena kidogo mlichonacho na kuwaachia barabara substandards. Tizameni Sam Nujoma, zege lilianza kubomoka kabla hata mradi haujakabidhiwa...!

  Upuuzi mtupu!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  lakini kuna uwezekano wa sisi watanzania kufanya kitu bila kutegemea wahisani na tukakifanya vizuri, kwa wakati na kwa ufanisi?
   
 6. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sidhani, tumekuwa "Aid addicts". Mpaka watoto wanajua mzungu=misaada siku hizi.
   
 7. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Babu, utapigwa ban!!Mbona unatufundisha matusi? :)
  Ila nakuelewa, wanaudhi, eh?
  And how contradicting, one minute anaomba msaada wa kupanua barabara kwa misingi ya kupunguza ajali, the next anasema ajali ni uzembe wa madereva!! This can only go unscrutinised in Tanzania!!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama kunahitajika miujiza kuweza kutimiza hili. Miaka zaidi ya 40 ya kujitawala sidhani kama tunashindwa. Kabarabara ka Sam Nujoma ka kilomita zisizozidi 4, tumempa mchina ajenge, katuzungusha kwelikweli kwa kuchelewesha kazi na bado katuachia kazi substandard, na barabara ipo Dar, the most commercialised city of our beloved Bongoland, sasa unaeza kuimagine magnitude ya tatizo.

  Sijui hali ya barabara ya Mandela itakueje.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I'm just sayin'...I'm not sayin'...but you know what I'm sayin.....
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Simple rule of becoming better off. Let's take an example of a poor person. Mtu masikini ana wezaji kuendesha maisha yake na vipesa vidogoa anavyo pata na at the same tiem akaendelea?

  1. Living within ones means. Tule kwa urefu wa kamba yetu. Matumizi ya serikali yaendani na hali halisi ya uchumi wetu.

  2. Saving and having surplus. Tukisha tumia pesa kwenye kuendesha shughuli mbali mbali za nchi pia tubakize kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.

  3. Fanya miradi yenye long term profit. Siyo lazima kuanza na kikubwa. Hii ina hitaji organization, planning, patience and vision.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  pse don't say it because I know what ur saying..
   
 12. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  My take:: Barabara zijengwe whether pesa zinatoka kwa walipa kodi wa tanzania au kwa wahisani, lakini ujenzi ufanyike ASAP na sio mambo ya upembuzi yakinifu (sp) blah blah.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Upembuzi yakinifu ni msemo tu ukionesha process za maandalizi ktk kukamilisha mradi wa kiinjinia. Ukisema uondoe upembuzi yakinifu hakuna engineering tena, and everything is a total waste.
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika hawa hata wakikaa kwenye vikao vya mabaraza la Mawaziri,Kamati tendaji ya makatibu wakuu,na vikao vya Halmashauri kama hata siku moja wanafikiria kusukuma mbele gurudumu la maendeleo bila kutegemea wahisani wamefika mahari mpaka wanaakili mgando kabisa wewe fikiri kwa mtaji wa nchi kama Tanzania ilivyo na utajiri wa rasirimali watu,na rasirimali za asili viiongozi wangekuwa wanawaza kujikita katika kukuza nyanja zote za uchumi ili angalau Tanzania ikawa kinara katika ukanda wa Afrika mashariki wakilingia amani na lugha moja inayotumika ,hawa watu kazi yao ni kuwaza saa ngapi visahani vya visambusa vitapita kwenye kikao wasokomeze kwenye makoo yao,nchi hii ilivyo na utajiri wa asili hakuna sababu ya kuchelewa kukuza pato la taifa na kuwa la kujitegemea
  Ndio maana inatakoe wata wahisani wanweza wakamdhihaki Raisi wetu kwa kumpelekea vizawadi vya baiskeli na matoroli na majembe ya mkono IKULU kwa sababu wanajua ndio hulka yake ya kupenda vimisaada,Raisi wa nchi nzuri yenye utajiri mkubwa kama hii hawezi kufanyiwa fedheha yakupelekewa kimasaada cha milioni 51 IKULU na yeye akafurahia kwa kujaribu kupanda kipikipiki kuwafurahisha kazi ambayo wangempa hata mkuu wa wilaya ya Ilala au Temeke au Kinondoni apokee lakini sio Raisi
  Wataadhiriwa kila siku kutokana na kuwa ombaomba kama wale wanosimama pale ubungo au salender
  Ebu viongozi badilikeni acheni mawazo mgando na hulka za kujipenda nyinyi zaidi ya nchii
  kukosa kwenu ubunifu muzalisha rundo zima la vijana wasio na kazi kwa maana hiyo ndio nguvu kazi ambao ingechakalika mungeacha kuomba baiskeli kutoka kwa wachina
  Du inatisha Raisi wetu kuomba baiskeli
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mpaka vifo vitokee ndio wanakumbuka barabara..Duu
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Ni maslahi binafsi ndo tanatuponza. Hakuna kitu kinachojengwa au kufanywa katika standard. Na hao wachina rushwa ndo iko mdomoni, akona ofisa wa serikali tu anatoa bahasha hata kabla hujasema shida yako. Its pathetic, ukiwa strict anawahi kwa bosi wako. Na huyu rais wetu nae, katuwekea foleni jumamosi tumeshindwa kwenda shamba, kisa anaenda kufungua machinjio. Hiyo si kazi ya waziri jamani! Aagh!
   
 17. M

  MC JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kikwete juzi kapokea MSAADA wa viatu na baiskeli kutoka Serikali ya watu wa China wenye thamani ya Shilingi Milioni 50. Sikuamini macho yangu...... Hii ndio TZ ya WaTZ
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,393
  Trophy Points: 280
  ,
  tusi kwa lugha nyingine sio tusi, hata neno nina, mayo, nyoko na mae, yya kufote ni mama kwa lugha za kibantu. Screw si ni ile ya kukazwa kwa csrew driver, tusi lipi?.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  are you serious?
   
Loading...