KURA YA 'HAPANA' SCOTLAND NI USHINDI KWA TUME YA JAJI WARIOBA NA WANANCHI.
Kumekuwepo na upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya makada wa ndani ya chama Chetu (CCM) juu ya nini ni maana ya matokeo ya kura ya "hapana" Scotland. Tumewasikia na kuwasoma makada hao kwenye media, lakini pia tunazidi kuwasoma kwenye mitandao ya kijamii, na kuna kila dalili Kwamba Orodha hii itazidi kuongezeka. Mbali ya kupotosha umma juu ya tafsiri ya matokeo ya kura ya Scotland, pia mbinu zinaandaliwa kupotosha umma zaidi Kwamba kura ya hapana Scotland ni Anguko au pigo takatifu la rasimu ya tume ya warioba, hasa Kwamba maoni Yale hayakutokana na wananchi. Lakini uongo huu hauna mileage ya kutosha, Vinginevyo:
1. Serikali ya CCM isingefunga tovuti ya tume kuzuia umma usione yaliyomo. Kwani Kama ni kweli Kwamba content ya utafiti na uchambuzi wa tume ungekuwa na mapungufu ambayo CCM inayasema, Jambo la busara lingekuwa ni kuachia umma uone hiyo content Ili uwe ni ushahidi wa CCM kwa wananchi juu jinsi gani maoni yake hayakuwa ya wananchi Bali ya tume. Hilo halijafanyika, na halitafanyika kwa sababu ni upotoshaji na CCM inajua Hilo.
2. Ushahidi mwingine Kwamba CCM ni waongo na tuhuma zao Kwamba maoni ya rasimu ya tume hayakuwa ya wananchi Bali ni ya kina mzee warioba ni Kwamba - Makada wa CCM wameshindwa kwenda kuisemea tume kwa wananchi au kuichapisha na kuisambaza kwa umma ili ujionee wenyewe Kwamba yaliyomo sio yake waliyoyasema Mbele ya tume. Pia Hilo, CCM haijafanya na haitafanya kwa sababu inajua Fika Kwamba chama hakisemi Ukweli.
Ni kwa mantiki hii, baadhi yetu ambao ingawa ni wanachama hai wa CCM tutaendelea Kupinga wale wote ambao wanahatarisha uhai wa muungano na taifa letu kwa ujumla kwa kuweka maslahi ya chama Mbele ya maslahi ya taifa. Mwendelezo wa kupotosha umma juu ya uhalali wa rasimu iliyowasilishwa na tume ya jaji warioba hautavumiliwa.
Baada ya kusema hayo, sasa niingie moja kwa moja kwenye mada - kujadili kwanini kura ya maoni ya Scotland ni Ushindi kwa tume ya warioba na wananchi.
Moja ya hadidu za rejea kwa tume ya mabadiliko ya katiba ilikuwa ni kulinda na kuboresha muungano, sio kuudhoofisha na kuvunja muungano. Tume ilitekeleza Hilo kwa uadilifu mkubwa, na nitoe Mifano michache:
1. Sura ya kwanza inaelekeza kuwepo kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
2. Sura ya tano inaelekeza Kwamba uraia ni wa nchi moja, nao sio mwingine Bali uraia mmoja wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hivi karibuni, viongozi wa CCM wamekuwa wakizunguka na hoja Kwamba "kura ya Scotland ni ushahidi Kwamba muungano ni Jambo muhimu kuliko utengano". Wengine wamekuwa wakikejeli rasimu ya tume Kwamba inalenga kuvunja muungano. Lakini Kama tulivyokwisha ona, hakuna Ukweli juu ya Madai haya.
Makada wa CCM wanasema Kwamba 55% ya kura ya hapana Scotland maana yake ni Kwamba muungano ni suala muhimu. Lakini hoja ya msingi ambayo baadhi yetu tumekuwa tukiwasilisha haipingani na Hilo. Hoja Hapa sio juu ya umuhimu wa muungano, kwani tangia Shule ya msingi, sote tunajua Kwamba "umoja ni Nguvu, utengano ni udhaifu". Lakini baada ya kupevuka akili na kuondokana na utoto, tume jifunza kitu kingine muhimu zaidi, nacho ni Kwamba - pamoja na Ukweli Kwamba umoja ni Nguvu, utengano ni udhaifu, nguvu haiwezi kupatikana katika mazingira ya kutegeana na kunyonyana. Ikitokea Hali hii ya kutegeana na bado tukasema Kwamba eti umoja huo ni Nguvu, Huko ni kujidanganya.
Katika hoja zao za upotoshaji juu ya matokeo ya kura ya Scotland, makada wa CCM wanaendelea kujadili Kwamba - kura hii ni fundisho kwa Zanzibar ambayo inataka kujitenga. Makada hawa wanaenda Mbali na kusema Kwamba - kura hii ni ushahidi juu ya "ubora wa serikali Mbili", Huku Wakisema Kwamba eti hata England haina serikali yake nje ya muungano wa UK, ingawa Scotland wanayo serikali Yao Kama Zanzibar. Kwa mantiki hi, wanahitimisha Kwamba muungano wa UK ni sawa na muungano wa Tanzania, hivyo hakuna mabadiliko yanayohitajika.
Kwa manufaa ya muungano na taifa kwa ujumla, ni muhimu tukasahihisha upotoshaji huu unaofanywa na makada kadhaa wa CCM mapema Kabla ya Hali haijawa Mbaya zaidi.
Tuanze kwa kuangalia hotuba ya waziri mkuu wa UK, David Cameroon ambayo aliitoa muda mchache baada ya matokeo ya kura ya maoni kutangazwa. David Cameroon alisema hivi:
"Just at the people of Scotland will have more power over their affairs, so it follows that the people of England, wales and Northern Ireland must have a bigger say over theirs".
Tafsiri isiyo Rasmi ni Kwamba:
"Kama ambavyo Scotland itakavyokuwa na mamlaka zaidi juu ya mambo Yao, Vivyo hivyo watafuata Watu wa England, Wales na Northern Ireland kuwa na kauli juu ya mambo Yao".
Hapa tunaona Kwamba makada wa CCM hawasemi Ukweli juu ya mabadiliko yanayokuja UK kufuatia kura ya maoni Scotland. Makada wa CCM hawasemi Ukweli Kwamba kwa kauli hii, sasa serikali ya England itajitenga au itajivua koti la muungano. Swali linalofuata ni je:
Kauli hii ya David Cameroon inapishana vipi na kazi ya tume ya mabadiliko ya katiba pamoja na matamshi mbalimbali ya mzee wetu jaji warioba ambae alifanya kazi yake kwa uadilifu na uzalendo mkubwa?
Kama alivyofanya Jaji warioba, David Cameroon ametambua Kwamba haiwezekani kuwepo kwa muungano imara iwapo muungano huo Unatoa Nguvu au mamlaka zaidi kwa mshirika mmoja wa muungano. Kuendekeza Hali hiyo ni kujenga chuki, uhasama baina ya pande Mbili za muungano, na hatimaye kuvunja muungano.
Katika hotuba yake, pia David Cameroon Alitamka Kwamba:
"I have long believed that a crucial part missing from this national discussion is England. We have heard the voice of Scotland and now the millions of voices of England must not be ignored".
Tafsiri isiyo Rasmi ni Kwamba:
"Kwa muda mrefu, nimekuwa nikiamini Kwamba suala muhimu linalokosekana Katika mjadala wa kitaifa, ni suala la England". Tumesokia sauti za wa-Scotland na sasa sauti za mamiloni na waingereza haziwezi kupuuzwa"
Katika Hilo pia, jaji warioba na tume yake waliweka bayana Kwamba kuna manung'uniko mengi ya wananchi juu ya Mfumo wa muungano wa serikali Mbili. Jaji warioba Alisema Kwamba kwa upande wa Zanzibar, yapo malalamiko makuu matatu, na kwa upande wa Tanzania bara, yapo malalamiko makuu manne. Jaji warioba akaonya Kwamba iwapo watawala watayazibia masikio malalamiko haya, matokeo yake itakuwa ni kuzidi kuudhoofika kwa muungano. Muhimu Hapa pia ni Kwamba, Kama alivyofanya David Cameroon kutaja jina la England na umuhimu wake kujivua koti la muungano, jaji warioba pia nae alijadili haja ya kuizindua Tanganyika pamoja na umuhimu wake wa kujivua koti la muungano. Kwa maana nyingine, kwa manufaa ya muungano, Kama ilivyokuwa muhimu kwa sauti za mamiloni wa Uingereza Kuanza kusikilizwa, Vivyo hivyo ni kwa sauti za mamilioni ya watanganyika.
Tunachojifunza kutoka kwa David Cameroon na Jaji Warioba ni Kwamba wadau wakubwa Katika suala la Mfumo wa Utawala ni wananchi, sio viongozi au Wanasiasa.
Katika hotuba yake ya kukabidhi rasimu ya pili pale viwanja vya karimjee, jaji warioba alisema Kwamba - "kuendelea kwa serikali Mbili kulihitaji ukarabati mkubwa ambao haiwezekani kufanyika."
Kauli hii ya jaji warioba haipishani na waziri mkuu wa zamani wa UK, Gordon Brown aliyoitoa mwezi Juni mwaka huu wa 2014. Gordon brown alisema Kwamba:
"Westminster's claim to undivided authority over the county? dead and buried".
Tafsiri isiyo Rasmi ni Kwamba:
"Madai ya Westminster juu ya mamlaka ya nchi yasiyogawanyika? Madai hayo yamekufa na kuzikwa".
Hapa tufahamu Kwamba Gordon Brown na David Cameroon ni viongozi wa vyama viwili Vikubwa vyenye upinzani mkubwa sana nchini UK, lakini Katika suala muhimu Kama Mfumo bora wa muungano wenye maslahi kwa taifa na muungano wenyewe, wameona Kwamba kuna haja ya kuweka pembeni itikadi za vyama, hasa iwapo suala husika wadau wake wakubwa ni wananchi. Gordon Brown amewahi kunukuliwa akisema Kwamba yeye sio Mpenzi wa Dhana ya shirikisho la Britain, lakini Mfumo huo sasa ni "necessary & inevitable". Huu Ndio uongozi! Kwanini Tanzania Tunakosa viongozi wa aina hii? Moja ya sofa kubwa ya uongozi ni uwezo wa kuingoza mabadiliko. Sisi viongozi wetu wanaogopa kuongoza mabadiliko. Je tutafika? Kwa Tanzania, kitendo cha ukawa kuwa nyuma ya maoni ya wananchi kwa mtindo ule ule wa UK, baadhi ya makada wa CCM wanafanya mzaha Katika suala nyeti Kama hili na kuendelea kuchakachua rasimu ya wananchi Kule Dodoma.
Kuna haja ya kuacha kupotosha wananchi juu ya nini maana ya kura ya maoni Scotland. No vote in Scotland haikumaanisha No Change. Kwa maana nyingine Rahisi - the ni vote has preserved the union, but has not preserved the status quo. Nitafafanua:
Katika kampeni za Gordon Brown juu ya "no vote" to Scotland's independence, tulisikia kampeni hizi zikiambatana na ahadi nyingi juu ya mabadiliko makubwa ya Mfumo wa Utawala wa nchi iwapo Scotland watakataa kujitenga na Uingereza. Brown alienda Mbali zaidi na kusema Kwamba - England, Wales, na Northern Ireland pia zitapewa mamlaka zao Kama Scotland. Haya hayasemwi na makada wa CCM wanaotumia matokeo ya kura Scotland kuhalalisha "No Change in Status Quo" in Tanzania. Kwa kufanya hivyo, pengine hawajui Kwamba ni kuingiza muungano wetu kwenye Giza nene.
Tukiendelea kujenga hoja kwanini kura ya hapana Scotland ni Ushindi kwa tume ya warioba na wananchi, Ahadi Za akina Gordon Brown zilizolenga kulinda muungano wa UK zinafanana sana na kazi iliyofanywa na tume ya warioba. Kwa mfano, kina Gordon Brown waliahidi Kuanza mchakato wa kuleta shirikisho la UK. Walienda Mbali na kusema Kwamba watafanya mabadiliko makubwa Kama vile kuzuia wabunge wa Scotland kutoshiriki kwenye bunge la westminster - kwenye mijadala na maamuzi juu ya mambo ya England kwa vile hayawahusu. Msimamo huu ulitokana pia na chama cha Conservatives chini ya David Cameroon ambacho kilidai madaraka Kama hayo kwa England (yani England nao kuingia kwenye bunge la Scotland). Kwetu Tanzania, ilitakiwa CCM iwe na msimamo sawa na ukawa Kama ilivyopendekeza tume, kwa maslahi ya muungano na taifa kwa ujumla.
Hoja za tume ya jaji warioba na kina Gordon Brown Wakati wa kampeni za "no vote to Scotland's independence zinafanana sana kuhusiana na washirika wa muungano kuwa na serikali zao, mabunge Yao, kuwa na mamlaka nje ya muungano. Kwa maana nyingine, Pendekezo la viongozi wa UK linafanana na lile la tume ya warioba juu ya shirikisho la serikali Tatu ambapo Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na serikali zake na mabunge yake juu ya masuala Yao ambayo hayataingiliana na masuala ya muungano Kama ilivyo sasa chini ya serikali Mbili.Hata ziboreshwe kwa miaka Mia moja, bila ya serikali Tatu, muungano utazidi kudhoofika.
Kuna umuhimu wa makada husika wa CCM kuacha kupotosha umma, na hii itakuwa kwa faida ya chama kwani wananchi wa Leo ni waelewa, sio wale wa miaka 50 iliyopita. Dhana ya kwenda kwa Wakati ndani ya chama ni lazima iendane na Dhati ya kuzingatia mahitaji ya Wakati uliopo, kwa mfano shirikisho la serikali Tatu.
Wanapojadili matokeo ya kura ya maoni Scotland, makada husika wa CCM wana haja pia ya kujadili kwanini matokeo ya Scotland yamekuwa hivyo, na hii pia ni faida kwa chama, hasa kuanzisha utamaduni wa kusimamia masuala ya kitaifa Kama wenzetu UK Katika masuala nyeti Kama haya ya Mfumo wa Muungano badala ya kuweka maslahi ya chama Mbele, huku muungano na taifa kwa ujumla vikiwekwa Katika hatari ya kusambaratika.
Kujadili Ushindi wa UK kwenye kura ya maoni Scotland bila ya kichambua na kujadili sababu za Ushindi wa kura hiyo haiwezi kukisaidia hata chama (CCM) Katika mikakati yake ya Ushindi na kutumikia wananchi. Kwa mfano, kujadili Ushindi bila uchambuzi wa sababu za Ushindi Ni sawa na chama kujadili Ushindi wake kwa mfano kwenye jimbo la uchaguzi au kata ya udiwani bila ya kujali kuchambua au kutathmini sababu juu ya kwanini chama kimeshinda kiti husika. Vile vile ni sawa na chama kuanguka kiti cha ubunge au udiwani na kuacha kujadili sababu za kuanguka Huko kwa manufaa ya kujipanga Mbeleni. Sidhani Kama CCM imepungukiwa hivyo kifikra, kwahiyo nadhani nitakuwa sahihi kusema Kwamba CCM Inaacha kujadili sababu za matokeo ya hapana Kule Scotland, kwa makusudi Kabisa, na kwa sababu hazina maslahi kwa muungano na taifa Bali CCM peke yake.
Tanzania nchi ya Watu wote bila ya kujalisha itikadi zao za vyama. Kati ya watanzania milioni 45, wanachama wa CCM hawazidi milioni tano, ambayo ni sawa na asilimia isiyozidi kumi na moja (11%) ya watanzania wote. Ni sababu hizi Ndio zinafanya baadhi yetu Kama wanachama wa CCM kuwa waangalifu Katika kuweka misimamo baina ya Ile yenye maslahi ya chama na Ile yenye maslahi ya muungano na taifa kwa ujumla. Tunaamini Kwamba hivyo Ndio tutaweza kuendelea kuwepo Katika siasa za nchi yetu hata Kama itatokea tukapoteza uchaguzi ngazi ya urais. Vinginevyo kuweka maslahi ya chama kwa kukandamiza maslahi ya taifa hakutatuwezesha kuongoza kwa ridhaa ya wananchi (the 90% ya watanzania ambao sio wana CCM), badala yake tutakuwa tukiongoza kwa hila na vitisho, masuala ambayo hata baba wa taifa aliyakemea Katika vitabu vyake vya "tanu na Raia" na "tujisahihishe" (1962).
Kuna haja ya makada wa CCM Kujifunza kutoka kwa vyama vya siasa UK, hasa kwa kuangalia mfano jinsi gani UK inaelekea kwenye Mfumo wa shirikisho kwa manufaa ya wananchi wa UK Kama tulivyojadili. Ni muhimu ieleweke Kwamba
matokeo ya kura ya hapana Scotland ni ahadi waliyopewa na vyama vyote Vikuu vya Uingereza juu ya mamlaka zaidi, mabadiliko makubwa ya kikatiba Kukidhi haja ya devolution kwa washirika wote wa muungano, na muhimu zaidi, safari ya kwenda kwenye "federation of the United Kingdom" na vision ya shirikisho (federalism). Kama wapo wasiokubali juu ya haya, basi watafute Nyaraka inayoitwa "a pledge for Scottish Voters". Nyaraka hii ilitiwa Saini na viongozi wote wakuu wa vyama vya siasa England: Cameroon (Conservatives), Ed Millband (Labour), na Nick Clegg (Liberal democrats), bila ya kujadili itikadi Zao za vyama. Nyaraka hii ilikuwa ni ahadi kwa wananchi wa Scotland Kabla ya kura ya maoni Kwamba wakipiga kura ya hapana na kubakia kwenye muungano, watapewa more executive powers juu ya Utawala wao wa ndani. Pia waliahidiwa Kwamba watakuwa na kauli ya mwisho (mamlaka) ya kuamua juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya jamii - elimu, afya, Ajira n.k, Katika jurisdiction Yao.
Mbali ya Hilo, Scotland pia walipewa ahadi ya kuwa na mamlaka (baadhi ya ahadi zikiwa tayari zinatekelezwa kwenye baadhi ya kodi) mamlaka ya kuamua masuala Mbali Mbali yanayohusiana na kodi na matumizi Yao - kibajeti (fiscal autonomy). Kwa mfano, suala la income tax, capital gains tax, VAT etc. Muda sio mrefu, Mfumo wa kibajeti UK utabadilika kufuatia kura ya hapana Scotland kwani hata northern Ireland and Wales (washirika Wengine wa muungano wa UK), nao wanaelekea kwenye fiscal autonomy.
Ni hitimishe kwa kusisitiza Kwamba:
"no vote" haina maana "no change" in Scotland. Kwa maana nyingine, the vote has preserved the "union", but has not preserved the "status quo".
Kwa tathmini ya tume ya jaji warioba, baada ya kuwasikiliza wananchi, tume iliona Kwamba ni dhahiri Pendekezo la kuifanya Zanzibar isionekane Kama kwa kuificha Tanganyika lisingekubika kwenye kura ya maoni. Kama ilivyo kwa tume ya warioba, viongozi wa UK waliona Hilo kwa Scotland zaidi ya miaka kumi iliyopita, na kuamua kuachana na siasa za vyama na bada yake kuweka maslahi ya taifa Mbele ili kulinda muungano. Hivyo ndivyo historia itamwandika mzee warioba. Lakini legacy yake itatokana na kuzinduliwa kwa Tanganyika, suala ambalo tofauti na miaka 50 iliyopita ambapo lilikuwa haliwezekani, Leo mtazamo umegeuka kuwa, kuzinduka kwa Tanganyika ni suala la muda tu, kwani, contrary to popular belief ndani ya CCM, rasimu ya tatu ya katiba ambayo ni Kinyume na Sheria ya mabadiliko ya katiba 2011, rasimu hii Ndio itakuwa kichocheo cha uzinduzi wa Tanganyika.
Tanzania kwanza, Tanganyika Kabla.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Cc
MwanaDiwani,
chama,
Nape Nnauye,
Mwigulu Nchemba,
ZeMarcopolo