Scotland Independence

Scotland Independence

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Baada ya uchaguzi mkuu nchini Uingereza, Scotland imejinyakulia vitu 48 ambavyo ni ushindi mkubwa kwa Scotland, First Minister of Scotland amesema kwamba, Scotland inajiamulia wenyewe own future na sio bunge la Westminster.

Nani alijua kwamba muungano wa United Kingdom wa miaka 300 na ushee utaweza kufikia hatua ya kuvunjika? Kuna kila ishara huko mbeleni Scotland na Northern Ireland zitadai uhuru.

Kwa nini Wazanzibar iwe ni uhaini? Zanzibar ina kila sababu nayo ya kudai uhuru wake kutoka Tanganyika.

Hivi siku Zanzibar ikaamua kujitenga kutoka Tanganyika na kuwa nchi inayojitegemea kwa kila kitu, ni nani atakayepoteza zaidi?

Au ndiyo mtaanza tena kudai fidia ya mabilioni kwa kisingizio Tanganyika iliwadhulumu tangu mlipoungana mwaka 1964? Ila Wazanzibar wakati fulani mpunguze ulalamishi aisee! Mbona mnafaidika zaidi na Muungano kuliko hata sisi Watanganyika!

Binafsi naunga mkono hoja ya kupunguza au kuondoa kabisa kile kinachoitwa "Kero za Muungano" ila siyo kujitenga kabisa na ndugu zenu wa damu wa Tanganyika. Nahisi mtaathirika zaidi kuliko kunufaika na huko kujitenga mnakotaka.
 
Maadam muungano wa England, Scotland na Northern Ireland kuunda United Kingdom umedumu kwa miaka 300!. Then nasi tusubiri angalau baada ya miaka 100 ndio tuanze kiwazia haya.

Muungano wao ni federations kama ilivyo USA lakini muungano wetu ni union fused together as one, it can't break.
Pole.
P
 
Nahisi itakuwa uzuri zaidi tukiungana na Sudani ya Kusini pia sio na kijinchi kidogo kama Zanzibar tu!
 
Hivi siku Zanzibar ikaamua kujitenga kutoka Tanganyika na kuwa nchi inayojitegemea kwa kila kitu, ni nani atakayepoteza zaidi?

Au ndiyo mtaanza tena kudai fidia ya mabilioni kwa kisingizio Tanganyika iliwadhulumu tangu mlipoungana mwaka 1964? Ila Wazanzibar wakati fulani mpunguze ulalamishi aisee! Mbona mnafaidika zaidi na Muungano kuliko hata sisi Watanganyika!

Binafsi naunga mkono hoja ya kupunguza au kuondoa kabisa kile kinachoitwa "Kero za Muungano" ila siyo kujitenga kabisa na ndugu zenu wa damu wa Tanganyika. Nahisi mtaathirika zaidi kuliko kunufaika na huko kujitenga mnakotaka.
Ukiijuwa uzuri mipaka ya bahari ya nchi hizi mbili ndio utajuwa nani ataathirika zaidi ukivunjika Muungano!
 
Zanzibar ni tofauti na scotland.Zanzibar wanadai uhuru shughuli zao zote na makazi ya wadai uhuru yakiwa tanzania bara!!!!!

soko la samaki wanategemea ferry la tanzania bara
 
Ukiijuwa uzuri mipaka ya bahari ya nchi hizi mbili ndio utajuwa nani ataathirika zaidi ukivunjika Muungano!

Tutawaachia visiwa vyenu viwili tu, cha Pemba na Unguja! Hayo maeneo mengine sijui yaliyotolewa na Muingereza kwa Sultan! Yatabakia daima kuwa ni ndoto ya asubuhi. Haitokuja itokee tukawapa kirahisi tu!
 
Naunga mkono Zanzibar iwe huru tena. Nina swali moja. Unaweza kuniwekea ramani ya Zanzibar inayoonesha mpaka wake na Tanganyika? Kila mara nikiukiza hiki swali sipati majibu ya kueleweka. Nimejaribu kugoogle napo siipati.

Latham Island ni mali ya Tanganyika au Zanzibar?
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia ukanda wa pwani wote ni Zanziba

Kwa hapa Der mpaka wa Zanzibar na Tanganyika upo kimara maana yake ni kwamba 90% ya jiji la Dar ni eneo la Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 1886 (Angro German agreement) 10 Miles coastal strip in Mainland ilikuwa mali ya Sultan wa Zanzibar ikiwa pamoja na Lamu,Pate n.k.Piga hesabu 10 inaishia wapi?Laki Ujerumani alinunua hizo 10 Miles kutoka kwa Sultan wa Zanzibar hiyo ni Angro German agreement 1890.Waambieni wasifute history Kama wanavyojidanganya wanasiasa mtasababisha matatizo hasa kwa kizazi kisichojua historia yao Kama wewe.
 
Nahisi itakuwa uzuri zaidi tukiungana na Sudani ya Kusini pia sio na kijinchi kidogo kama Zanzibar tu!
Mkuu Ikipendaroho, exactly hiki ndicho kinakwenda kufanyika kwenye mtangamano wa Africa Mashariki, tumeanza na customs union, tuko kwenye common market, tunakwenda kwenye free labour migration, free movement, hakuna kutumia passport, tunakuja muungano wa sarafu na kumalizia kwa political federation tunakuwa nchi moja masikini Zanzibar itakuwa kama Lindi!.
P
 
Mwaka 1886 (Angro German agreement) 10 Miles coastal strip in Mainland ilikuwa mali ya Sultan wa Zanzibar ikiwa pamoja na Lamu,Pate n.k.Piga hesabu 10 inaishia wapi?Laki Ujerumani alinunua hizo 10 Miles kutoka kwa Sultan wa Zanzibar hiyo ni Angro German agreement 1890.Waambieni wasifute history Kama wanavyojidanganya wanasiasa mtasababisha matatizo hasa kwa kizazi kisichojua historia yao Kama wewe.
Yes Wajerumani walinunua hiyo 10 miles costal stripe toka kwa Waingereza kwa kubadilishana na kisiwa cha Hellingoland. Jina jingine la hiyo treat inaitwa Hellingoland Treaty.
P
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom