Sawa Mungu akatuchoma moto wa Milele. Je ninyi watakatifu mtakao Baki mtakuwa na furaha Gani wapendwa wenu wakiwa wanachomwa moto wa Milele??

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
11,250
Reaction score
24,084
Mods Uzi huu uachwe ujitegemee tafadhari.🫷

Awali ya yote Mimi mpango wa kwenda mbinguni ni kama haupo maana kila nikipiga tathimini Bado najiona Sina sifa hizo
Kwanza Zaka sitoi,sadaka nishakataa kuipeleka kanisani.

Ukija namna ya kuishi napo Bado na pwaya maana uko zako unawaza kuchuma nyanya zako mara mdada kaumbika anapita mbele yako Tyr hapo natamani (naingia dhambini) so kwa kifupi yapo mengi na mengi ambayo nikijifanyia tathimini najiona Bado sitatoboa kuingia yerusalemu mpya.

Sasa mtuambie ninyi watakatifu mtakao Uingia mji ule!.......

Ikiwa tu hapa Duniani tunapopoteza wapendwa wetu huwa tunakuwa na msongo wa mawazo wengine huzimia na wengine hujihisi upweke usio Isha.


Wengine Bado hadi Leo hawajapona mioyo Yao baada kuondokewa Baba,mama ndg na jamaa zao

Vipi wewe mtakatifu wa Bwana utakuwa na furaha Gani iwapo familia yako yote itachomwa moto ?

Mke/mme na watoto pamoja na wazazi wako wadogo zako na wakubwa zote wamechomwa moto utakuwa na furaha Gani?

Kama mtaishi kwa raha huku watoto wenu wanachomwa moto huko jehanamu sasa sijui akili yenu itakuwaje vile.

 
Mungu ni wetu sote, wenye haki na wasio haki. Kutoa sadaka kanisani si kigezo cha kwenda mbinguni, wala kushiriki ibada kila siku si tiketi ya kupokea uzima wa milele. Neno la mungu linatumbia kwamba sote tutaokolewa kwa imani si matendo. Unapoishi pasipo roho wa Mungu ni vigumu kwako kuenenda katika haki. Wala amri zake si mzigo mzito, ni kumkiri na kumpokea yeye moyoni mwako kwa imani utayashinda yote katika ulimwengu.
 
Moto wa milele utaunguza nini wakati mwili wa mtu huzikwa ardhini na kuoza? Na hapa kwenye picha naona watu wako motoni (na miili yao) sasa sijui hawakuzikwa hawa!?
 
Wewe unarahisha sana
 
"Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli."

Ufunuo 21:4-5
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…