Sauti......................... ........

Dena Amsi

R I P
Aug 17, 2010
13,082
4,260
Habari zenu wote......

Hapa nazungumzia sauti kwa wanaume (Msinipige mawe)
Napenda kupata maoni yenu may be mie nakosea
kufikiria hivyo.......................

Nimekuwa nikiona mwanaume mwenye sauti nzito (besi)
huwa wanakuwa na confidence sana katika kuzungumza
kuliko wale wenye sauti nyembamba kama ya wanawake
huwa hata hawapendi kuzungumza sana wanaona kama
hawaheshimiwi hivi wanakuwa hawajiamini sana kama hawa
wenye sauti nzito (nimekutana na mmoja jana) mwenye sauti
nyembamba alikuwa akiongea bila kujiamini kabisa.........
Nikamuuliza mbona unanielekeza kitu huku huna confidence
akasema huwa sipendi kuongea sana sauti yangu ina shida
sikutaka kumuuliza sana nilijua ni shida gani anayozungumzia

Wanaume mpo??? Hebu nipeni mauzoefu yenu tafadhali

DA
 
Uchokozi huo... Ukipigwa mie simo... Hivi hilo huwa ni tatizo au, na kama ndio huwa linasababishwa na nini?

Kuna mmoja alikuwepo jana tbc1 kile kipindi kinachohusu mambo ya kiswahili, akiongea utamhurumia sauti ya kike.
 
Mie na wewe nani mchokozi.........
mie nimeuliza nataka kujua tu
 
Mi nadhani inategemeana na mtu mwenyewe,wapo wenye sauti ndogo lakini wana roho ngumu na wako wenye sauti kubwa na ni waoga pia,ila wenye sauti kubwa huwa wakiongea wanapewa attention kutokana na sauti ndo mana.
Hivi baba wa taifa ana sauti ipi?
 
Mie na wewe nani mchokozi.........
mie nimeuliza nataka kujua tu
Sio uchokozi Dena, nilikuwa nimeketi na mtu akawa ananiuliza huyo ni mwanamke mwanaume? Mwanzoni nikamjibu mwanamke manake amevaa shati jeupe mikono mifupi kama blauzi ila walivosogeza kamera nkaona ana suruali na viatu vya kiume,..ikabidi nikanushe haraka kuwa sio mwanamke lol...

Afu sasa hana sura ngumu kivile na ndevu katoa zote... Mie nawashauri wanaume wenye sauti za kike wawe wanafuga ndevu ili kutuondolea utata bana...

DA si umeshatanguliza samahani hapo juu? Nisijetolewa kwa dirishani bure!
 
Sauti inaongeza kujiamini kwa kiasi kikubwa .
Mwenye sauti laini kama ya kike huwa anakuwa undercomfidence kutokana na kasumba ilyojengeka kuwa wanawake ni dhaifu sana.
 
Sikuona hicho kipindi haya ushauri umesomeka
 
Mi nadhani inategemeana na mtu mwenyewe,wapo wenye sauti ndogo lakini wana roho ngumu na wako wenye sauti kubwa na ni waoga pia,ila wenye sauti kubwa huwa wakiongea wanapewa attention kutokana na sauti ndo mana.
Hivi baba wa taifa ana sauti ipi?
Baba wa Taifa( rip ) sauti yake ilikuwa ya kawaida bana, akiwa anasisitiza jambo ndio inabadilika na kuwa nyepesi kidogo but pia huwezi kusema inafanana na ya kike...

Kuna wanaume wana sauti ya kwanza Excellent, yaani akiongea ukafumba macho utadhani uko na mwanamke!
 
Sauti inaongeza kujiamini kwa kiasi kikubwa .
Mwenye sauti laini kama ya kike huwa anakuwa undercomfidence kutokana na kasumba ilyojengeka kuwa wanawake ni dhaifu sana.

Mie hapo kwenye red tu ndo nimepaona
 
Baba wa Taifa( rip ) sauti yake ilikuwa ya kawaida bana, akiwa anasisitiza jambo ndio inabadilika na kuwa nyepesi kidogo but pia huwezi kusema inafanana na ya kike...

Kuna wanaume wana sauti ya kwanza Excellent, yaani akiongea ukafumba macho utadhani uko na mwanamke!

vp kuhusu wanawake wenye sauti za kiume?
 
Baba wa Taifa( rip ) sauti yake ilikuwa ya kawaida bana, akiwa anasisitiza jambo ndio inabadilika na kuwa nyepesi kidogo but pia huwezi kusema inafanana na ya kike...

Kuna wanaume wana sauti ya kwanza Excellent, yaani akiongea ukafumba macho utadhani uko na mwanamke!

Wewe ngoja utolewe baru ndo utaimba yesu ni bwana
 
Back
Top Bottom