Sauti za marehemu zaanza kusikilizwa

Sauti za marehemu zaanza kusikilizwa

Kwa mara ya mwanzo kabisa na baada ya jitihada za miaka mingi wanasayansi wamefanikiwa kuipata sauti ya kizuu kiitwacho Nesyamun cha kiongozi wa kidini aliyeishi nchini Misri miaka inayokisiwa 3000 kabla ya kuzaliwa Yesu rehema na amani ziwe juu yake.

Kulingana na maandishi yaliyopatikana kwenye kaburi lake kuja kusikilizwa tena kwa sauti yake hapo mbeleni baada ya kifo chake ilikuwa moja ya ndoto za kiongozi huyo.

Mafanikio hayo kama yalivyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari yamepatikana kutokana na juhudi na ushirikiano wa wanasayansi kutoka vyuo vikuu kadhaa kama vilet Royal Holloway, University of London, na chuo kikuu cha York na Leeds Museum Habari hizi zimechapishwa kwa mara ya mwanzo katika jarida la kisayansi lilitoka Alhamis iliyopita.
View attachment 1332484
Nisomapo habari hizi nafikiria hali itakavyokuwa hapo miaka michache ijayo tutakapoanza kuzisikia sauti za mitume kama vile Yesu a.s na atakapozikanusha baadhi ya imani zetu juu yake.

Vyuo vikuu vyetu [emoji22] ajabu ajabu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hivyo hivyo.Na zaidi nyuzi za kutoa sauti kwenye koromeo ziwe hazikuharibika pamoja na kupitiwa na karne nyingi tangu kuondoka kwake duniani.Hili kwa Mwenyezi Mungu anapotaka kuthibitisha uwezo wake na huruma zake kwa viumbe wake ili kutoa nafasi ya kila mmoja kuelekea peponi zaidi kuliko motoni,hilo ni rahisi sana kwake na yaelekea ndio mpango wake huko mbeleni.Hii sauti ya kizuu cha Misri ni hatua tu kuelekea huko.
Hiyo mifupa au mabaki ya Yesu utayapata wapu?
* 2 Kor 4:3,4
Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
 
Vyuo vikuu vyetu [emoji22] ajabu ajabu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyuo vikuu vyetu tujikaze basi!. Sisi tuanze kuscan vivuli vya watu waliokufa zamani.Mimi nadhani hili la sura litakuwa jepesi pia iwapo sauti imeanza kuonesha njia.Si tayari tuna kamera za majumbani na mabarabarani ambapo pakitokea uhalifu huwa tunakimbilia kuangalia rekodi ya picha mpaka tunamfikia tunayemshuku.
Vyuo vikuu vya Tanzania vingeanzisha mradi wa kuscan picha za eneo fulani walipopita watu fulani tunaowajuwa angalau miaka 20 iliyopita na nataraji tutawaona.Baada kufanikiwa hili tutatengeneza super scanner la kuangalia nyuma zaidi mpaka tuwafikie Mitume rehema na amani ziwashukie.
 
Natamani nimsikie mfalme Suleiman,mtu mwenye busara kuliko wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo litakuwa lugha sasa.Sijui alikuwa akizungumza lugha gani.Na Jee lugha hiyo bado ina watu wanaoifahamu.Ama iwapo ni maswahaba wa Mtume Muhammad rehema na amani zimshukie si tatizo kwani wanaofahamu kiarabu wapo wengi duniani.
 
Maana yake ni kuwa waliokufa zamani hapo baadae tunaweza tukawasikia walivyokuwa wakizungumza wakati wa uhai wao.Mambo yakikaa vizuri hata mitume tutawasikia mawaidha yao.
Hakutakuwa na kudanganyana tena.
Kitu gani ambacho watakiweka ktk vyombo vyao ambavyo itafanya wasikie hiyo sauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazungu wameshakosa kitu cha kufanya.

Wakati sisi tunawaza wapi tutapata pesa wao wanawaza pesa walizonazo wazipeleke wapi.

Unforgetable
Ni kweli tulisoma kwenye social policy, kuna watu wanapesa lakina hakuna ardhi ya kutosha kuwekeza. Wakati sisi tuna ardhi lakini hatuna pesa ya kuwekeza.
 
Tatizo litakuwa lugha sasa.Sijui alikuwa akizungumza lugha gani.Na Jee lugha hiyo bado ina watu wanaoifahamu.Ama iwapo ni maswahaba wa Mtume Muhammad rehema na amani zimshukie si tatizo kwani wanaofahamu kiarabu wapo wengi duniani.
Hapo ndio shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana yake ni kuwa waliokufa zamani hapo baadae tunaweza tukawasikia walivyokuwa wakizungumza wakati wa uhai wao.Mambo yakikaa vizuri hata mitume tutawasikia mawaidha yao.
Hakutakuwa na kudanganyana tena.
Hapa ndo utadanganywa mpaka ufurahi, dunia kuna mambo inaandaa nahisi ili kuendeleeza usimamizi
 
Mbona taarifa halisi haiendani na taarifa unayoitoa wewe??
- Unajua sauti ni nini?
- Kama unajua sauti ni nini utasikiliza vipi maneno ya sauti ya mtu aliyekufa?

Taarifa inasema wanasayansi kwa kutumia mabaki ya vocal cord ya mummy wame print 3D vocal cord ambayo itatoa sauti sawa na sauti ya huyo mummy. Hayo mengine umeyatoa wap??
Screenshot_2020-01-25-14-36-03-1.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho kifaa kije huku ili ninunue niwe nasikiliza sauti ya mama yangu na baba yangu waliofariki, nitafukua makaburi ya mababu nisikilize sauti na lugha zao za awali, ili siku ukipewa kesi ya uhamiaji haramu unasikiliza sauti za mababu unaondoa utata
 
Ndio hivyo hivyo.Na zaidi nyuzi za kutoa sauti kwenye koromeo ziwe hazikuharibika pamoja na kupitiwa na karne nyingi tangu kuondoka kwake duniani.Hili kwa Mwenyezi Mungu anapotaka kuthibitisha uwezo wake na huruma zake kwa viumbe wake ili kutoa nafasi ya kila mmoja kuelekea peponi zaidi kuliko motoni,hilo ni rahisi sana kwake na yaelekea ndio mpango wake huko mbeleni.Hii sauti ya kizuu cha Misri ni hatua tu kuelekea huko.
Kwa hiyo kwenye miili yetu kuna kifaa cha kutunza Sauti?
 
Back
Top Bottom