Hapo zamani za kale.........

Hapo zamani za kale.........

idiomer

Senior Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
179
Reaction score
203
Hapo zamani za kale palikuwa na kijiji kimoja kizuri sanaa. Kijiji hicho kilikuwa na vitu vizuri kama dhahabu, gesi, maji safi na na mali nyingi msituni. Basi kiongozi mmoja mzalendo akapewa kazi ya kuongoza jahazi.

Wakaenda vizuri kumbuka kabla ya hapo waliongozwa na watu kutoka katika vijiji vingine. Basi hilo jambo liliwakera. Basi wakapambana kupata kiongozi mzawa.
Hakika kiongozi wa kwanza alikuwa mwema mzalendo na mpenda watu, mkarimu na mcheshi.
Wakaenda siku miezi miaka basi ikafika muda yeye mwenyewe akaomba ufanyike uchaguzi na mwingine aongoze jahazi akaja wa pili naye alikua mzalendo na aliwapa uhuru wenzake kufanya mambo mengi. Basi matajiri wakawepo. Akaja watatu akaona ni vema kubinafsisha mali za watu kuwa za umma. Wakaona ni vema ikawa asubuhi ikawa usiku siku zikaenda.

Akaja wa nne yeye alipenda sana raha na kuwakaribisha wale waliokuwepo kabla ya wazawa kuchukua uongozi. Miaka ikaenda watu wakawa na fedha na kusema nitakupiga nikulipe. Ukwasi ukawa mkubwa sana kwa baadhi ya wanakijiji.

Akaja kiongozi mmoja akaona si vyema maskini kunyanyaswa akawabana matajiri sanaaa kukawa kama hawapo wengine wakakimbia kijiji hicho. Bahati mbaya kiongozi huyo alifariki akiwa hajamaliza malengo yake.

Akaja mwingine ambaye alirithi basi kama ilivyo desturi mali za kurithi hazina uchungu. Huyo kiongozi akafanya maisha ya mwanzo yakarudi watu walijisifu tena nanga mwenye hela kama mimi. Ufahari wa majumba, magari na fedha ukawa mkubwa. Mtu anatoa fedha kuchangia serikali basi watu wakawa na sauti kuliko serikali kijiji kikaanza kujawa na migawanyiko kwani maskini walichukizwa na uongozi huo. Nguvu za kupinga mambo ukawa mkubwa .

Basi kijiji hicho kikawa na sintofahamu badala ya kufanya maendeleo wakawa wanapambana kutatua migawanyiko.

Kijiji hicho kila aliyepinga dhuluma aliona cha mtema kuni. Basi kumbuka kiongozi aliyepita alikamata wale walio kuwa na ukwasi kwa dhuluma. Ila alivyofariki walitoka kizuizini . Baasi mambo yakageuka na sasa wale waliotetea haki wakawa kizuizini na wengine kuuawa.

Je una maoni gani dhidi ya kijiji hicho ? Je kinafanana na kijiji utakacho?
 
Apumzike kwa amani huyo kiongozi aliekufa kabla ya malengo yake kukamilika.
 
Back
Top Bottom