Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Kwa mara ya mwanzo kabisa na baada ya jitihada za miaka mingi wanasayansi wamefanikiwa kuipata sauti ya kizuu kiitwacho Nesyamun cha kiongozi wa kidini aliyeishi nchini Misri miaka inayokisiwa 3000 kabla ya kuzaliwa Yesu rehema na amani ziwe juu yake.
Kulingana na maandishi yaliyopatikana kwenye kaburi lake kuja kusikilizwa tena kwa sauti yake hapo mbeleni baada ya kifo chake ilikuwa moja ya ndoto za kiongozi huyo.
Mafanikio hayo kama yalivyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari yamepatikana kutokana na juhudi na ushirikiano wa wanasayansi kutoka vyuo vikuu kadhaa kama vilet Royal Holloway, University of London, na chuo kikuu cha York na Leeds Museum Habari hizi zimechapishwa kwa mara ya mwanzo katika jarida la kisayansi lilitoka Alhamis iliyopita.
Nisomapo habari hizi nafikiria hali itakavyokuwa hapo miaka michache ijayo tutakapoanza kuzisikia sauti za mitume kama vile Yesu a.s na atakapozikanusha baadhi ya imani zetu juu yake.