Avatar
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 11,128
- 11,938
Kwa mara ya mwanzo kabisa na baada ya jitihada za miaka mingi wanasayansi wamefanikiwa kuipata sauti ya kizuu kiitwacho Nesyamun cha kiongozi wa kidini aliyeishi nchini Misri miaka inayokisiwa 3000 kabla ya kuzaliwa Yesu rehema na amani ziwe juu yake.
Kulingana na maandishi yaliyopatikana kwenye kaburi lake kuja kusikilizwa tena kwa sauti yake hapo mbeleni baada ya kifo chake ilikuwa moja ya ndoto za kiongozi huyo.
Mafanikio hayo kama yalivyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari yamepatikana kutokana na juhudi na ushirikiano wa wanasayansi kutoka vyuo vikuu kadhaa kama vilet Royal Holloway, University of London, na chuo kikuu cha York na Leeds Museum Habari hizi zimechapishwa kwa mara ya mwanzo katika jarida la kisayansi lilitoka Alhamis iliyopita.
View attachment 1332484
Nisomapo habari hizi nafikiria hali itakavyokuwa hapo miaka michache ijayo tutakapoanza kuzisikia sauti za mitume kama vile Yesu a.s na atakapozikanusha baadhi ya imani zetu juu yake.
Habari za Yesu tunazipata kwenye maandiko tuu,yeye alifufuka na hakuna tunapoweza kupata mifupa au mabaki yake.Sasa si mpaka upate mwili was Yesu au mifupa yake?
huwezi maana mwili wake haupo , ipo sanda yake tu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Tunachofanya ni kutumia akili zetu na kuthibitisha kwamba sisi si walemavu wa kufikiri.Hivyo hatua ndogo waliyofikia sisi tunaenda mbali kufikiria mafanikio kamili na hii ni moja ya njia za kivumbuzi.Iwapo hao wanasayansi wanasoma hii michango yetu basi inaweza ikawatia moyo au wakaitumia kutafuta matokeo yaliyobora.Hapo na sisi itakuwa tumechangia kwenye jambo la maana kwa manufaa ya binadamu na kizazi kijacho.Mbona taarifa halisi haiendani na taarifa unayoitoa wewe??
- Unajua sauti ni nini?
- Kama unajua sauti ni nini utasikiliza vipi maneno ya sauti ya mtu aliyekufa?
Taarifa inasema wanasayansi kwa kutumia mabaki ya vocal cord ya mummy wame print 3D vocal cord ambayo itatoa sauti sawa na sauti ya huyo mummy. Hayo mengine umeyatoa wap??View attachment 1334219
Sent using Jamii Forums mobile app
Kila kitu kina sababu zake.Kwanini ziwe biblia za mapadri au maofisi kwao?
Sio wazungu wote wana pesa nyingi kiasi hichoWazungu wameshakosa kitu cha kufanya.
Wakati sisi tunawaza wapi tutapata pesa wao wanawaza pesa walizonazo wazipeleke wapi.
Unforgetable
Sasa nimekuelewa, sasa kama ndio ulimaanisha hivyo mbona hiyo technology tunayo toka miaka ya 1800's ... Niko hapa nasikiliza wimbo wa Lemi Ongala "Kifo" [emoji1][emoji1]na na Lemi alishaukata kitambo sana.Tunachofanya ni kutumia akili zetu na kuthibitisha kwamba sisi si walemavu wa kufikiri.Hivyo hatua ndogo waliyofikia sisi tunaenda mbali kufikiria mafanikio kamili na hii ni moja ya njia za kivumbuzi.Iwapo hao wanasayansi wanasoma hii michango yetu basi inaweza ikawatia moyo au wakaitumia kutafuta matokeo yaliyobora.Hapo na sisi itakuwa tumechangia kwenye jambo la maana kwa manufaa ya binadamu na kizazi kijacho.
Umeelewa Mazo....