Sauti ya "kike" inanisumbua usingizini

Sauti ya "kike" inanisumbua usingizini

Wiyelelee

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Posts
1,071
Reaction score
348
Jamani, nimeone niliseme hapa ili muweze kunisaidia kutokana na tatizo ambalo lilianza mwaka jana mwezi wa 11. Nimevumilia lakini niliseme tu hapa.

Nikiwa nimelala usiku, ikifika muda wa saa kumi hivi, inanijia sauti "nyororo na yenye kuvutia sana" inaita "Wiyelele, Wiyelele". Sauti hiyo inaning'ongoneza kwenye sikio langu la kulia nikiwa nimelala. Sauti hii ni nzuri sana na imekuwa ikijirudia mara tatu kwa wiki tena muda na wakati huo huo.

Nionavyo mimi, ni sauti ya mwanamke au msichana mzuri sana ambaye ambae simjui. Picha yake ilinijia usingizini siku moja kwenye ndoto na ni mzuri sana. Ni sauti inayoniita kwa kunibembeleza... natamani niedelee kuisikiliza jamani. Nahisi sauti hii imeona shida ninazozipata.

Kila niskikiapo sauti hii basi siku hiyo nakuwa na raha na amani sana. Sijajua bado maana yake ni nini. Hata hivyo, sio sauti ya mke wangu lahasha! Kwanini istokee siku hizi? Bado nafikiri na sipati majibu. Najitahidi kusali sana ili isije, lakini, kama ni sauti mbaya, mbona ikitokea nakua na furaha sana siku hiyo?
 
Akikuita tena itika umwambie akusubirie muondoke wote ukajipatie furaha ya kudumu.
 
baadae atakuwa anatokea na sura na usishangae ukajikuta unaota unafanya nae mapenzi, yani huyo ni jini mahaba huwezi ona madhara yake sasa, na kwasababbu umeshakubali kuwa unakuwa unafuraha ukiitwa ndo baasi unampa nafasi
Kama ni jini mbona siku nikiitwa nakuwa na furaha sana?
 
baadae atakuwa anatokea na sura na usishangae ukajikuta unaota unafanya nae mapenzi, yani huyo ni jini mahaba huwezi ona madhara yake sasa, na kwasababbu umeshakubali kuwa unakuwa unafuraha ukiitwa ndo baasi unampa nafasi

Sasa naomba msaada, nifanye siku ikitokea tena? Huwenda ikawa jini kweli...
 
Kwani umesahau kama ulishawahi kumtoa mimmba msichana in short huo mzimu wa binti yako.UTAJIBEBA MWAKA HUU.

Kikikikiki, we ndo unaota kweli. Sijawahi hata kidogo rafiki yangu.
 
Safari imekamilika. Wanakuandalia VIZA kabisa.
 
nikwambie!
hakuna cha jini mahaba wala nini! umemchukia sana mkeo kiasi cha kuamini kuna mwanamke mwingine mzuri anayekufaa umemtengeneza kichwani kwako na hiyo ni akili yako tu inarudisha kile unachowaza mchana kutwa!
 
Jini mahaba anakunyemelea

sio anamnyemelea hilo ni jini mahaba kamili
anachotakiwa ni kuchukua hatua na kukutana na watumishi wa Mungu ili aweze kufunguliwa
maana huwa yanakuwa kizuizi hasa pale unapofika wakati wa wewe kutaka kuanzisha mahusiano na mwanamke mwingine


zingatia mapema kweupe kabla haijwa ndivyo sivyo
 
Wale watu uliyo watapeli wanaanza kukutega kwa sauti za kike, ukiitika tu imekula kwako.
 
Thats devils trick wake up and take serious prayers ndg yangu! Kumbuka kazi kubwa ya Ibilisi ni kuleta destruction hiyo ni njia ya kukamilisha mission yake ambayo itaambatana na kuharibu ndoa yako! Wake up stand firm kutana na watumishi wa Mungu uweze kufanyiwa effective prayers na wewe mwenyewe uweze kusimama thabiti katika maombi!
Hakikisha hutengenezi loop hole yoyote ktika ndoa yako ya kumuwezesha shetani kupata mpenyo wa kuleta uharibifu meaning that you have to pray sana for your marriage.
 
Weyelele, maisha ni kitendawili na pia ni safari ndefu yenye mambo mengi tunayoyajua na tusoyajua.

*Kitendo cha wewe kuja kutafuta ushauri/suluhu ya tatizo lako hapa JF, inaonyesha ni jinsi gani umeona kuwa sio tukio la kawaida kunong'onezwa na mwanamke (sielewi ni ukiwa usingizini au ukiwa macho na pia sielewi ni maono au ni ndoto.

*Jambo la kutisha ni wewe kuwa curious kutaka ama kujua zaidi ni sauti ya nani na pengine kujenga uhusiano nae/kumfuata (maana unadai ni mzuri).
*Nadhani una mke (unaonekana usingejali kama ukipata mwingine mzuri zaidi.

TATIZO lako umelileta hapa na kila mchangiaji analeta anavyojua yeye ama kwa kudhani au kwa experiences zao. lakini nadhani itakuwa ni vigumu zaidi mwisho wa haya kujua ushauri mzuri ni upi. mimi ningesema hivi:

1. Tatizo lako inawezekana ni psychological au ni Spiritual. Spiritual issues lazima zitafutiwe solution yake iwe spiritually. na pia psychological issues zipelekewe wenye utaalam huo.

2. Matatizo ambayo ni spiritually based yanaombewa. Na labda niseme kuwa mimi ni mtu wa kanisa, na nimeona watu wengi wakiombewa na kupona kabisa (Tatizo ni kujua mwoombeaji ambae amesimama na akakusaidia tatizo hilo. Maana uzoefu unaonyesha kuwa mambo kama haya huwa hayaji na moja (Utaanza kusikia sauti, mara unakuja ona ndoa imevunjika, mara watoto wanaumwa tuuu, mara hupati pesa nk.

3. Suala lingine nikuwa unaweza wewe mwenyewe kujiombea na kusimama na Mungu. Hii inahitaji mtu msoma neno na anaetenda kuzingatia neno la Mungu (Righteous person). Hilo unalikemea dakika chache tu, na hutasikia tena.

4. baya zaidi inaonekana katika maelezo yako kuwa umefikia kujenga uhusiano na hilo(shetani - it doesnt matter its name).

5. The minute you try to have a conversation with demonic agents you will be setting yourself to fail. Break that relationship as soon as you can and start your deliverance battle.
 
Back
Top Bottom