ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,685
Wenje si kazi yake. Acheni ujinga
acha upuuzi wako wewe.....Kwani wale masalia hawakuwa wakijiita namna hiyo? Tena mpaka leo yule binti kinara wao anaendelea kuamini hivyo. lengo lako tumeshalifahamu, wala husumbui tena
Wenje usipokee simu zao.
Me naona mna mnyanyasa tuu wenje kwanza si jukumu lake kufatilia mikopo! Alaf swala la ukahaba hivi ni kweli litatuliwa na wenje kama sio nyie wenyewe?
Sasa hapa mnamuonea! Labda muombe awasaidie kufatilia tuu na hilo linawezekana kabisa!
hana haja ya kuombwa, hiyo ndiyo kazi yake jimboni. Ni wajibu wake pasi na shaka. Sisi ndio tumemchagua kwa makubaliano kwamba atawakilisha kero zetu serikalini km inavyotueleza falsafa 'social contract theory'.
kazi yake ninini?, wanafunzi kutoka jimboni kwake wamepata matatizo yeye yuko karibu na serikali, achukue hoja zao aziwakilishe panapohusika. Linapokuja swala la kamanda mwenzetu kuzembea tusimtetee.
hawa watoto wa siku hizi wameanza kudelegate migomo ili wapate boom. Wenje ndo akagome? Aafu mbona wakati wa uchaguzi vyuo vilikuwa vimefungwa? Waliopo hapo chuoni ni walioanza chuo 2010/2011 sasa kura walilinda wapi wakati hata chuo walikuwa hawajaanza? Huyu atakuwa ni chagulani na wenzake.! Madogo acheni uoga wa kipumbavu kafateni hela zenu management mpaka bodi hadi waone ofisi chungu! Mmekaa mwanza mnasubiri wenje ndo aje dar kufuatilia boom la wanachuo! These are jokes bhana.
Kwa hiyo nyie hamna wawakilishi huko chuoni? Mmeshatuma muwakilishi wa kwenda kuonana na wenje aka kataa?
wawakilishi wapo ambao ni SAUTSO iliyoko chini ya raisi wake MALISA ambaye ni katibu mwenezi tawi la SAUT CDM. Uongozi wote wa SAUTSO walichaguliwa wakiaminiwa kwamba ni wapambanaji wa CDM ila muda wote wamefunga ofc zao.
hayo si yangu, hizi ni taarifa za wanafunzi toka jimbo la Wenje na zimeandikwa kwenye gazeti la SAUTI HURU.
SAUTI HURU ni gazeti dada la wanazi wa ssm na jambo leo>< uliyetoa thread yawezekana una malengo yako>< achana na weje watz tunaona kazi yake mjengoni<>
Wenje shughulikia madai ya wanafunzi hawa. Achana na watu wanaokukingia kifua humu, jaribu kufuatilia suala hili. Nakumbuka SAUT ilikua chachu ya ushindi wako.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mt. Augustine-Mwanza wamemtupia lawama mbunge wao mh. Wenje kwa kile kinachoelezwa kwamba amewatelekeza.
Ikumbukwe kwamba Mh Wenje wanafunzi wa SAUT ambao idadi yao ni zaidi ya 15000 ndio waliomwezesha kiasi kikubwa kupata ushindi. Pia ni hawa hawa wanafunzi ndio walikesha kwenye vituo kulinda kura zisichakachuliwe.
Chanzo cha kumtupia lawama mbunge wao Wenje ni kutokana na wanafunzi wenzao 215 hadi sasa semister imeisha hawajapata pesa zao za kujikimu kutoka bodi ya mikopo.
Inaelezwa kwamba uzembe mkubwa kutoka uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi SAUTSO inayojipambanua kwamba ni makamanda wapiganaji wameshindwa kufuatilia pesa za wanafunzi hawa kitendo kilichopelekea wawasiliane moja kwa moja na Wenje kupata msaada zaidi.
Lakini hadi sasa si Wenje ambaye amewapa taarifa juu ya hatima yao huku wakidai muda mwingine wakimpigia simu hapokei.Imefikia baadhi yao kuacha chuo, wengine wameanza kujiuza miili yao ili wapate pesa za kujikimu.
Jamii ya SAUT ni kubwa jamani...na kwa ukubwa wake nafikiri inahitaji attention ya mtu kama MBUNGE...