Saudi Arabia kuona Hamas wanashinda ndio wanajitokeza kutetea "two state solution"

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,192
10,926
Kwa muda mrefu nchi ya Saudi Arabia imekuwa kimya tangu pale vita vianze rasmi kati ya Hamas na jeshi kubwa la Israel.

Takriban mwezi tangu vita vianze waliitisha mkutano wa mataifa kadhaa ya kiarabu na kiislamu uliofanyika mjini Riyadh.Katika mkutano huo hakuna chochote cha maana kilichojadiliwa wala azimio la maana lilliofikiwa.Kikubwa kilichotokana na mkutano huo ni kutoa wajumbe waliokwenda China kuishtaki Israel kwa nchi hiyo.

Kwa ujumla ujumbe ule ulipuuzwa sana na China na hata watu walioupokea walikuwa ni maafisa wa ngazi za chini katika wizara ya mambo ya nje.

Baada ya kashfa ile Saudi Arabia imekuwa kimya sana tena katikati ya mauji mabaya yaliyousthtua ulimwengu mzima.Ilikuwa kama kwamba walikuwa wamekubali Israel iwamalize Hamas na kuua kiasi inachotaka cha wapalestina ili hatimae mpango wake wa kurudisha uhusiano na taifa hilo haramu ufanikiwe.

Miezi mitatu mbele na wakati Hamas wamesimama wenyewe kujitetea kwa mafanikio ndipo Saudi Arabia imesikika ikisema eti hawatarejesha uhusiano na Israel mpaka hapo mpango wa kuwepo kwa taifa la Palestina sambajmba na Israel utakapowekwa wazi.

1706072508146.png
Saudi Arabia 'rules out' normalisation with Israel without state for Palestinians
 
Mkuu fahamu Saudia ni kama koloni la Marekani! Hakuna cho chote ambacho Saudia inaweza kuamua bila US kukubali!
Sasa US nao wanaanza kuishauri Israel ikubaliane na Two state solution! Kwa hiyo si ajabu Saudi kuanza kujitutumua na kutoa kauri hizo!
 
Kwa muda mrefu nchi ya Saudi Arabia imekuwa kimya tangu pale vita vianze rasmi kati ya Hamas na jeshi kubwa la Israel.
Takriban mwezi tangu vita vianze waliitisha mkutano wa mataifa kadhaa ya kiarabu na kiislamu uliofanyika mjini Riyadh.Katika mkutano huo hakuna chochote cha maana kilichojadiliwa wala azimio la maana lilliofikiwa.Kikubwa kilichotokana na mkutano huo ni kutoa wajumbe waliokwenda China kuishtaki Israel kwa nchi hiyo.
Kwa ujumla ujumbe ule ulipuuzwa sana na China na hata watu walioupokea walikuwa ni maafisa wa ngazi za chini katika wizara ya mambo ya nje.
Baada ya kashfa ile Saudi Arabia imekuwa kimya sana tena katikati ya mauji mabaya yaliyousthtua ulimwengu mzima.Ilikuwa kama kwamba walikuwa wamekubali Israel iwamalize Hamas na kuua kiasi inachotaka cha wapalestina ili hatimae mpango wake wa kurudisha uhusiano na taifa hilo haramu ufanikiwe,.
Miezi mitatu mbele na wakati Hamas wamesimama wenyewe kujitetea kwa mafanikio ndipo Saudi Arabia imesikika ikisema eti hawatarejesha uhusiano na Israel mpaka hapo mpango wa kuwepo kwa taifa la Palestina sambajmba na Israel utakapowekwa wazi.
View attachment 2881099
Saudi Arabia 'rules out' normalisation with Israel without state for Palestinians
Hamas wanashinda nini?
 
Kwa hadhi yake mbele ya Palestina Hakukutakiwa tamko.Kilichotakiwa ni vitendo kama vya Houth
Unajua kwa nini kipindi cha Makkah Mtume Muhammad ( Peace be upon him) hakupigana na wala kuamrisha UMMA kupigana pamoja na mateso yote ila Jambo hilo likatokea Madina tena baada ya muda kupita ?

Saudi anaweza kupambana na Israeli plus washirika wake ?

Vita sio kitu kizuri unaweza kuambulia hasara bila kupata chochote ulichokusudiwq ikiwa umeupiga hesabu mbaya na kukurupuka je hizo hasara zitalipwa vipi ?
 
Mahesabu katika vita haviendani na uzembe wala woga.
Inategemea na kiwango cha uchokozi unaochokozwa.Kuna sehemu hata ukihisi utashindwa inabidi upigane ili ufe kishujaa.
Kwa hapa anachofanya Saudi Arabia na sababu zote zitakazotolewa haziendani na shida iliyojitokeza Palestina na hasa Gaza.
Kila siku watu wanauliwa kwa kasi ya 200/day na husemi kitu wala humzuii anayefanya mauaji hayo.
Houth wanazuia meli zinazokwenda na kurudi Israel na imetikisa kiasi kile.Saudia hata akisema hauuzi mafuta kwa Israel na hatoi ushirikiano nayo basi ingesaidia zaidi.
 
Kama umeshindwa kuona ushindi huo basi hujawahi kusikia habari za teknolojia inayosifiwa nayo Israel na wala hujaona wingi wa vifaru na ndege za kivita ilivyonavyo.
Kashangilie huo ushindi wa hamas kwenye mashimo ya panya ila nakupa pole usije kulia humu free palestine
 
Hebu tuambie na wewe ni ushindi upi unaoshangilia wa Israel kwa Hamas.
Kumbe kupigwa hospitali kila siku na kuuliwa watu na kufukua makaburi kutafuta mateka unaona ndio ushindi!
 
Unajua kwa nini kipindi cha Makkah Mtume Muhammad ( Peace be upon him) hakupigana na wala kuamrisha UMMA kupigana pamoja na mateso yote ila Jambo hilo likatokea Madina tena baada ya muda kupita ?

Saudi anaweza kupambana na Israeli plus washirika wake ?

Vita sio kitu kizuri unaweza kuambulia hasara bila kupata chochote ulichokusudiwq ikiwa umeupiga hesabu mbaya na kukurupuka je hizo hasara zitalipwa vipi ?
Msome Mfalme Faisal aliwaadhibu Marekani kwa njia ipi nyakati za mgogoro kama huu!

Nikusaidie, aliwaadhibu kwa kuwawekea vikwazo, kutoruhusu mafuta kwenda kwao.
 
Hebu tuambie na wewe ni ushindi upi unaoshangilia wa Israel kwa Hamas.
Kumbe kupigwa hospitali kila siku na kuuliwa watu na kufukua makaburi kutafuta mateka unaona ndio ushindi!
Pole humo mahospitalini magaidi wanarushia rocket lazima wapigwe humo
 
Back
Top Bottom