Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,186
- 10,924
Wakati uchaguzi wa Marekani unakaribia kumekuwepo na habari nyingi kuhusiana na mazungumzo ya kurudisha uhusiano baina ya Saudi Arabia na taifa la Israel.
Uhusiano huo umeshindikana kwa miaka yote hiyo tangu kuundwa kwa taifa la Israel mnamo mwaka 1948.Hii imetokana na tawala zote za Saudi Arabia kushikamana na maazimio ya kutokufanya mahusiano bila uhuru wa Palestina.
Kwa upande wao Marekani na Israel wamekuwa wakishinikiza jambo hilo kwa mbinu mbali mbali.Kwa mujibu wa vyombo vya propaganda vya kimarekani na Israel ni kuwa pindi makubaliano hayo yakifanikiwa basi Saudi Arabia itakuwa ndiye kinara wa eneo lote la mashariki ya kati.
Upande wa Saudi Arabia kwa mujibu wa vyombo hivyo ni kuwa inataka ihakikishiwa usalama wake katika hali ya machafuka kama yale yaliyoitwa Arab Spring na pia iruhusiwe kumiliki kinu cha nyuklia kwa matumizi ya kiraia kama kile cha UAE na vile vile iweze kununua aina ya silaha hasa ndege za kivita ambazo bado wamewekewa vikwazo na Marekani kuuziwa.
Kuvionesha kwamba vitu hivyo ni vya thamani kubwa imeelezwa kuwa kuna upinzani ndani ya mabunge ya Marekani kuiruhusua Saudia kupata wanachokitaka.
Mapema wiki hii kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas aliitwa na Saudi Arabia ili kujadili kile wanachokitaka iwe katika masharti ya Saudi Arabia katika mazungumzo ya kurudisha uhusiano na Israel.
Kiongozi huyo wa kipalestina alitaka utawala wake uruhusiwe kuwa na mamlaka kamili katika maeneo ambayo makubaliano ya miaka ya nyuma walipatiwa uhuru wa namna fulani ambao sasa wameona wameshang'anywa.
Vile vile ametaka Israel isitishe ubomoaji na ujenzi unaofanyika kila siku kwenye maeneo ya wapalestina.