Sasa vita mpya CHADEMA, CCM

Sasa vita mpya CHADEMA, CCM

mambo ya uchunguzi chadema hawatayaweza wao waendelee tu na tarifa zao za udaku na vikatuni.
 
nakubaliana na wewe ila point yangu ni kuwa wanaposoma huo udaku hawatoki bure ila kuna kitu wanapata, mfano hiyo habari iliyoandikwa kuhusu mkutano wa mbowe huko songea hata kama umeandikwa na gazeti la udaku kama unavyoamini,huoni kwamba msomaji atakuwa keshasoma hotuba yote ya mbowe na kuona ubaya wa serikali?

Hiyo ni kweli.
 
Magamba bwana.....lazima jasho liwatoke najua maovu mliyoyafanya ndio maana wanagwaya kuwa na uwazi.Nimefurahishwa sana na maneno ya kamanda mbowe ya kuwa haogopi mtu awe rais,polisi,jeshi bali anawaheshimu,pia ya kwamba wamemwongeea charge.Kanyaga twende kamanda Mbowe..hatuwezi kuwa watumwa katika nchi yetu,nami naongezea kwa kusema siogopi kufa iwe kwa kunyongwa,kupigwa risasi,kufungwa kifungo cha maisha,kwani hata walio madarakani akiwemo Jk na wengine lazima wafe ila hatujui ni njia gani lakini kufa ni lazima,hakuna nafsi itakayodumu milele katika uso huu wa dunia.
 
Ingekuwa laani zinagawiwa kama karanga!!!

hivi wewe unafikiri mbowe angeuawa kwenye mkutano huo wa kampeni,amani ya nchi ingekuwa hatarini.Fikiria beyond kidogo,usimwangalie mbowe angalia wanaomfuata,acha uvivu wa kufikiri wewe.
 
mziki wa Bilicanas au wawapi tena Mkuu. yote yatapita na CCM itabaki madarakani kwa gharama yeyote ile tupo. hakuna hakuna hakuna kama CCM Tanzania

Ndio maana mnaua watu,mnateka watu,mnalipua mabomu...kumbe ndio gharama unazozisema,hata Gaddafi alifanya haya haya leo hii yuko wapi?
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...

Nakerwa na mijitu isiyoshughulisha ubongo,haya maneno ni nukuu aliyosema Mh.Mbowe sasa
hapa udaku upo wapi,?!!!kwani lazima uchangie hata kama unajidhalilisha?!!!!
 
Akili za bavicha hizi!!!

Uwezo wako wa kufikiri sio mkubwa,kama mnaona kama chama cha demokrasia na maendeleo ni tishio,si muue viongozi wote sasa halafu ushuhudie nini kitatokea,ucwe mvivu wa kuhangaisha ubongo wako,jaribu hata kukifuta tu ucheki movie yake.
 
Wakati wao CCM wakimtesa mtu mmoja mmoja kwa kung'oa kucha na meno bila ganzi GIZANI, sisi CHADEMA tunauambia umati wa MUNGU haki yao HADHARANI. Nina hakika kile CCM hawataki watanzania wajue, sisi CHADEMA tutajitahidi kuwaambia na kweli wataelewa.
 
Back
Top Bottom