Sasa tumefika mwanzo wa mwisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa tumefika mwanzo wa mwisho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Sep 6, 2010.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Hatuko mwanzo,wala hatuko mwisho,inawezekana tuko mwanzo wa mwisho.Hapa nazungumzia safari ya taifa hili la Tanzania kuelekea kwenye ukweli,kuelekea kwenye mwanga.Ukiona giza totolo limetanda kila kona ujue asubuhi inakaribia.Bila shaka Watanzaniawengi hawajawahi kuona mwanga,hawajawahi kuiona asubuhi,ni watu wachache ambao hawafiki hata nusu ya wananchi wote wanaoimiliki asubuhi na wanaoitawala nuru ya nchi hii,wakiamua leo hii mvua inyeshe wanaweza,lakini kwa muda mrefu sas wameamua jua liangaze,mazao yetu yananyauka,ngozi zetu zinangua,mama zetu wamekuwa wajane,wadogo zetu wamekuwa yatima.

  Lakini sasa angalau mwanga unaanza kuonekana,wale watu waliokufa wanaonyesha dalili za kufufuka,wakina mama sasa wanaanza kung'amua kuwa waume zao hawakufa bali walipelekwa utumwani,hapa ni pazuri kwa kuanzia.Yale yanayodaiwa kuwa ni maisha bora kwa kila mwana kaya sasa yameyeyuka,hayapo na wala hayakuwahi kuwepo,sasa wananchi wanatambua kuwa hakujawahi kuwepo na mipango yoyote ya kuwakomboa zaidi ya sanaa za maonyesho na mbwembwe za vin'ola vya watawala,vinginevyo utaongoleaje tabia ya watawala wetu kuiendesha kaya kwa press conference?

  Waziri mtanashati aliyevalia mavazi ya gharama hasa suti nadhifu ambazo zinapatikana London na Paris pekee,aliyependeza kisawasawa,ambaye mwonekano wake unaonyesha ana siha nzuri na bongo safi,anajitokeza mbele ya wandishi wa habari kuja kutoa majibu ya maswali magumu,mwisho wa mkutano hakuna alichokieleza zaidi ya majisifu na majigambo,"serikali yangu itawachukulia hatua kali wale wote watakaohatarisha amani na usalama wa taifa".Waandishi wanapotaka kumuuliza maswali anagoma,yuko bize na shughuli za serikali.Huyu ni mtu aliyepita skuli nyingi wao wanamwita Profesa,sawa lakini si kila Profesa ana bongo safi na pia huwezi kujua huo uprofesa aliupataje,si unajua katika kaya yetu chochote kinawezekana,wewe hujaona au hata kusikia vyeti vinauzwa au watu kofoji vyeti?.

  Hapa ndipo tulipofika na hatukufika kwa bahati mbaya,na wala hatukufika kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.Tumefika hapa kwa mapenzi ya watu wachache wateule na watoto wa mfalme wanaoishi mitaa ya ng'ambo ya DARE ES SALAAM.Hawa ni wateule weusi wenzetu kwa rangi na wageni kwa tabia na matendo yao,hawa tulikuwa nao enzi za kutafuta uhuru,tulikunywa na kula kwa pamoja,tuliishi wote kwenye nyumba za udongo,tulikunywa mvinyo na sifongo kwa pamoja,lakini wenzetu Mungu kawasaidia,wamebadili zile nafasi za wale tuliokuwa tunawapinga,ujamaa waliokuwa wanauhubiri haupo tena,sasa kila mtu na atakufa na chake.Usaliti!Usaliti!Usaliti mkubwa huu unaofanywa na ndugu zet wa damu tuliokuwa tunachunga wote ng'ombe na kukamata vindege kule Bagamoyo,Rombo,Kantalamba,Uvinza,Tundur na kwingineko.

  Nasema hapa tulipofikia ni pazuri,maana hamna ambaye sasa amelala,kila mtu najua usaliti huu mtakavitu,wanajua kuwa nchi hii inahitaji ukombozi wa pili ambao ni mgumu kuliko ule wa mara ya kwanza.Ukombozi wa kwanza tulikuwa tunagombana na na wale weupe wa ng'amboambao hatukuwa na nasaba nao,sasa tunagombana na ndugu zetu,walioshiba hasa na wenye miili ya watu wawili ndani ya mwili mmoja na walevi wa madaraka wa kupindukia ambao wako radhi kununua ndege mbovu ya rais kwa gharama ya wananchi kula nyasi.Nasema tulipofika ni pazuri sana kwa kuanzia harakati,kuwa nasubira nitakuambia,na nitakachokuambia tafathali sana wambie na wengine ila usiwambie nani kakuambia maana wakubwa hawachelewi kusema nina hatarisha amani ya nchi,waulize MwanaHalisi nini kiliwapata,wakati kwa upande wa wabaka uchumiwanatesa mitaani kwa sababu kuwakamata ni sawa na kuiangusha serikali,sasa ingawaje si sawasawa.

  Katika vita ya kuzikomboa nchi zetu kutoka mikononi mwa mazanuni wa kikoloni bila shaka adui yetu alikuwa anaonekana hata kwa kumtazama kwa macho,tulifanikiwa kwa sababu lengo letu lilikuwa moja,tukawaondoa wakoloni ambao tulikuwa hatuwajui vizuri.Kama Halmashauri yako ya ubongo inafanya kazi kwa ushirikiano mzuri,si tu utakubaliana na mimi bali utaamini kuwa uhuru tuliupata hatuwezi kujivunia kwani matunda yake hayaonekani,maana tumeyasubiria sana,na sas ni jioni na tunaenda kulala bila ya hata kula.

  Kama haujui basi naomba kubaliana na mimi kuwa uhuru si kila mara ni mwisho wa utumwa,inawezekana sera ya assimilation na assimilado zimetuathiri kiasi kisichopimika,vinginevyo unazungumziaje tabia ya viongozi wengi wa bara hili lililoitwa bara la giza na wakoloni.BViongozi wetu wa bara hili ni walevi na walavi wa madaraka kwa kiasi kisichoelezeka.Inawezekana hatukufahamu kuwa wakati tunapata uhuru wazungu walikuwa wametuzidi akili,wakafanya kile ambacho ndicho kinatutesa hadi leo hii.

  Uhuru tulioupata una maana moja tu,kuwa wajanja wachache kujimilikisha madaraka na mali na kubadili nafasi za wazungu kufaidi neema za nchi.Ikulu sas zinakaliwa na weusi wenzetu kwa ranmgi na tofauti kwa matendo.Weusi haya ni hatari kulio weupe tuliowafukuza.Angalia sasa Ikulu zetu zimetekwa,zimekuwa sehemu zinazokaliwa na wachuzi au madalali wa soko huria au wajasiliamali kwa lugha tamu za kimagharibi.Watu tunaowaheshimu sana na pengine tunaowaamini sana kama ndugu zetu,ni haohao wanaotusaliti na kushirikiana na wanyang'anyi wa ng'ambo kupora rasilimali zetu.

  Baba wa taifa,Hayati Mwalimu Nyerere amewahi kusema kuwa ikilu ni sehemu takatifu,ambayo haina kitu zaidi ya kubeba matatizo ya watu,pia amepata kuwauliza vijana waliokuwa wanakimbilia ikulu,kuwa wanafuata nini Ikulu.Bila shaka sasa tunaona kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa anawajua vizuri vijana hawa(kwa sasa wazee0,na sisi pia tumeona kuwa vijana hawa walikuwa wanataka nini.Wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu mwaka 1995,pamoja na Kikwete kuonekana akimshinda Benjamini Mkapa,Baba wa Taifa aliingilia kati na kumwambia Kikwete kuwa alikuwa mdogo(sijui kiumri au kiakili)Uamuzi huo ulionekana kama ubabe,lakini sasa tunaona kuwa Nyerere kuwa alikuwa sahihi.

  Lakini kwa kutenda haki zaidi,pia tumeshuhudia jinsi chaguo la Nyerere,Mkapa alivyosaidia kuchonga jeneza la nchi kuelekea kwenye utumwa.PAMOJA NA KUIMARISHA UCHUMI,KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI NA KUONGEZA NIDHAMU YA KAZI SERIKALINI,zoezi lake la ubinafshaji mali za umma umeleta gharika kuu ndani ya nchi hii.Ubnafishaji wa mali umma unaweza usiwe tatizo maana tumeshuhudia nchi nyingine zoezi hili likienda vizuri,lakini zoezi hili kuliendesha ndani ya nchi yetu ni sawa na kuuza nchi kwani watendaji wengi wa serikali sio waaminifu hata chembe.

  Katika nchi ambayo watendaji wake hawajulikani wametokea wapi,wanachaguliwa kwa ujanjaujanja kutokana na kiasi cha pesa walizonazo,na wengine wanateuliwa kushika nyadhifa kubwa serikalini kutokana na michango yao waliyoitoa wakati wa uchaguzi,vinginevyo mtandao una maana gani au una faida gani kwa wananchi?Vi9nginevyo jiulize kwanini nchi za Asia kama vile China wamesonga mbele sana kimaendeleo wakati miaka ya 1970 tulikuwa almost at the same level,lakini kwa sasa hawa watu wako mbele sana kiasi kwamba hata watu wa maghariby wameanza kuogopa.Nchi kama China inasonga mbele kwa sababu ya uzalendo wa juu kabisa,mipango inayoendana a utekelezaji,elimu nusu masomo na nusu kazi na uaminifu wa ajabu kwa watendaji wa serikali.

  Lakini kwa Afrika ni tofauti sana,uhuru ulikuwa una maana moja tu,kuhamisha neema walizokuwa wanapata wazungu kwa weusi wenzetu.Angalia wenzetu hawa walivyokuwa maharamia,wakiua watu wetu wasiokuwa na hatia,usishituke sana,vinginevyo unasemaje kuhusu ufisadi wa kutisha unaofanywa na watendaji wa serikali,angalia wakina mama wanavyopoteza maisha pamoja na vitoto vyao,huduma za afya ni duni,na watu wengine wanakufa kwa kukosa chakula katikati ya ardhi yenye rutuba.

  Sidhani kama wananchi waliowengi kama hawajui kinachofanywa na watendaji na wanasiasa wetu.Kwa maoni yangu wengi wanajua kuna kuna baadhi ya watu ambao zamani tuliwaita wenzetu jinsi wanavyoneemeka na kunawili kwa kutumia rasilimali za taifa.Wanachi wanatambua haya,tena ukiwakuta wanaongea kwenye vijiwe vyao,kama unapenda kuchekacheka na kutopenda kufikiri sana utawapuza lakini kama unapenda kufikiria,utaumia sana na utachukua hatua.

  Mwishojapo si kwa umuhimu ni kwamba Watanzania tuna nafasi moja tu ya kurekebisha makosa yetu hapo ifikapo Octoba 2010.Japo wengi hawaamini kuwa kuwa katika Afrika inaweza kubadilisha maisha,hakika tunaweza kusonga mbele kama tutawapigia kura watu makini na wanaokerwa na umasikini wetu.Ni nafasi yetu pekee kuonyesha ukomavu wetu na uzalendo wetuTuchague watu makini na si vyama,vyama vinapita lakini Tanzania itabaki milele.Tuchague viongozi kwa umakini mkubwa ili tuitimishe ngwe ya kwanza ambayo ni MWISHO WA MWANZO.
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena.
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kama ulikuwepo. Na waliouona huo mwanzo wa mwisho ni wale ambao kila siku walikuwa mwisho wa mambo yote - walalahoi, maskini wa kutupwa.

  Hawa ndio wanaosema - leo - kwamba SASA BASI.

  Kweli, hata mbwa wako ukimtesa sana, iko siku atakuja KUKUNG'ATA mkono wako!

  Wananchi wamenena. HAWADANGANYIKI!

  CCM kushinda kwa kishindo ni sawa na ndoto za Alinacha!

  Hahahaha!

  JK, nenda kapumzike baba. Nenda, nenda kwa amani. Nenda. Imechoka! Unahitaji kuijenga upya CCM yako, utuachie sisi Tanzania yetu!

  SASA tunairejesha Tanzania mikononi mwetu. SASA NI MWANZO WA MWISHO wa UTAWALA wa CCM!

  -> Mwana wa Haki
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Tuchukue hatua gani ili tuhakikishe nchi yetu inarudi kwa wananchi? Maana imeporwa na MAFISADI. Haitatosha kusimama pembeni na kuitazama CHADEMA.

  Kama sio wewe utafanya hiyo kazi basi ni nani? Nani atakukombolea taifa lako? Itabidi utoe mchango wako. Kama uko Tanzania nenda ofisi ya CHADEMA uwaambie uko tayari kufanya kazi za chama. Jiunge kama bado. Kuwa Katibu Mwenezi wao sehemu ulipo. Hata kama ni ofisini tu.
   
 5. A

  African Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika historia ya maendeleo ya dola mbali mbali ili kupiga hatu ni muhimu kwanza kuutambua ukweli na kuelekea mbele. Ni Bahati mbaya kwamba bara la Africa hususani kusini mwa jangwa la Sahara ... hasa Tanzania...it is taking too long for this nation (TZ) to discover reality and address it and make a step foward. Mfano mzuri ni kukubali kuwa ufisadi unalirudisha nyuma taifa na kupambana nao kwa dhati. Wote tunajua fika jitihada za serikali yetu kupambana na ufisadi ni danganya toto ( alex Stewart,EPA) zote hizi ni political show cases kwa wafadhili ili kubembeleza misaada. We all know that Japan made a quantum jump after investing massively in public education yet there is no will to adopt this historical best practice. We have to discover reality address it and move forward.
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Post nzuri sana Mwankuga. Ni vipi ujumbe huu mzuri utaweza kuwafikua wananchi wengine nje ya JF?
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwanahaki umenena vizuri lakini je umekwenda vijijini ukaangalia jinsi watu bado washabiki wa kofia,kanga na tshirt za CCM?
  Inabidi kujipanga kwelikweli...Na bado kuna watu huko vijijini hata baadhi ya mijini wanaaminishwa kwamba ukichagua upinzani ni vita!
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mbaya zaidi hata hawa wananchi wa Dar es salaam tunaoamini wana elimu tosha ya uraia (cha kusikitisha) bado hawajui chanzo cha umasikini wao kuwa ni uongozi dhaifu wa CCM na Serikali yake, jana nimepita vigunguti kukwepa foleni ya pale Tazara kuelekea airport niliyoyakuta huko ni balaa, wananchi wanataabika mno hata ukiangalia sura zao ni zimekata tamaa, lakini ni wachache sana wanaojua kwamba sera mbovu, utendaji mbovu na ubadhirifu wa mali za umma na gawiwo lisilo na usawa la pato la taifa ndiyo chanzo kikuu.

  Ni kweli lazima kusimama kweli kweli maana makamba akienda hapo wote hao wanatoka vibandani kwao wanamshangilia na juu ya vibanda nyao wameweka bendera za CCM juu. tuna kazi bado lakini we have to move forward so far so good
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mwankuga peleka hii article Mwananchi au mwanahalisi watu wengi wanufaike na busara zako,kweli mzee umenena
   
 10. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu, wala si vijijini tu hata hapa mjini wapo ambao hata uwaambie nini inakuwa kana kwamba unampigia mbuzi gitaa. Wati wanaichukulia status quo kama ndio hali halisi na halali na wanaopinga wanapinga kisiasa tu! It is very frustrating!
   
 11. D

  Dopas JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwanza nampongeza Mwakuga kwa post nzuri iliyojaa uchungu alionao kwa nchi yetu.

  Pili nakuunga mkono mageuzi1992 kwa mchango wako.

  Kwa ujumla tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha wetu wetu. Ila sio rahisi kuwaambia wasichukue hizo khanga na kofia za CCM, wazichukue tu ila wajue wa kumpa kura.

  Pia sisi sote wakati na baada ya kupiga kura tuhakikishe haki inatendeka. Kupambana kufa ili kuepuka kura zetu zisiibwe.
   
 12. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,453
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Kwa ujumla tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha wetu wetu. Ila sio rahisi kuwaambia wasichukue hizo khanga na kofia za CCM, wazichukue tu ila wajue wa kumpa kura.

  Elimu ya kupiga kura haijatolewa,wapiga kura walio wengi mijini na vijijini hawaelewi hilo zoezi la kupiga kura vizuri,Ni bahati mbaya kwa wale walioelemika baadhi yao hawajiandikishi kupiga kura,na waliojiandikisha hawajitokezi kupiga kura,wamekata tamaa.Kura ya maoni huko nchi jirani Kenya kuhusu katiba mpya wananchi walipewa elimu ya zoezi hilo na walijitokeza kwa wingi.Labda itungwe sheria ya kumtaka mtanzania mwenye sifa za kupiga kura lazima ajiandikishe na apige kura,zipo nchi zinafanya hivyo Uswizi na nyingine.
  Vitambulisho vya uraia ni muhimu katika uandikishaji na upigaji kura.Lakini kwa makusudi au kutojua umuhimu wa vyeti vya uraia tunatimiza miaka 50 ya uhuru bila vitambulisho vya uraia.Sasa CCM mnaomba miaka mingine mitano ya nini?kama miaka 50 mlishindwa haya mambo ya msingi kura tuwape za nini?Nenda likizo angalau miaka 10 mjifunze a, e, i ,o, u ya kutawala nchi.
   
 13. m

  mjukuu2009 Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu post yako imetulia,
  Mimi naona ata vijijini watu wamesha elimika watu wana tambua matatizo yana yowakabili ni kwa sababu yakuwa na uongozi mbovu ndio mana ata hao viongozi wa ccm wakienda uko wanazomewa au wanakumbana na watu waliojipanga barabarani kutaka kuelezea matatizo yao.
  kusema vijijini awajaelimika kabisa ni sera ya ccm ili wakiiba kura waseme vijijini amna watu awatambui upinzani.
  EEHEE MUNGU TUONDOLE AYA MAJAMBAZI YA MALI NA DEMOKRASIA YETU,WEWE CCM TUACHIE SASA UMESHATUNYONYA VYAKUTOSHA,EWE KUPE TUACHIE SASA AMNA TENA DAMU.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kuhusu elimu ya mpiga kura huwezi kuitoa kwa upeo maana tume ya uchaguzi wanachuja mno taarifa za kuwapelekea wananchi.
  CCM kila mahali kama GESTAPO
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ninaomba ruhusa nii copy na kuanza kuizungusha kwa email kwa wadau. Kwa jinsi hii itafika mbali sana.
   
Loading...