Sasa ni rasmi January Makamba Waziri wa ovyo kuwahi kutokea kwenye sekta ya Nishati

Mr Dumila

JF-Expert Member
Jun 3, 2016
272
537
Habari wanabodi naandika hapa nikiwa Na masikitiko makubwa Na huyu Waziri aliyepewa wizara nyeti kabisa

Kwanza niweke wazi sijawahi mchukia Ila niliamini ni Waziri mzuri kutokana alivyofanya mambo mazuri akiwa Waziri wa Mazingira .
Ila toka amepewa wizara ya Nishati madudu yamekuwa makubwa zaidi haswa upandaji wa mafuta huku akijisifu kupunguza kodi wakati mafuta yanapanda

Sasa Hili suala la umeme ndio limenifanya nimuone Waziri wa hovyo kuwahi kutokea sababu umeme umekuwa unakatika saana haswa Sisi wa mikoani kuwahi kutokea toka miaka 60 ya uhuru

Hali ya kuwa alitupa siku 10 suala la mgao Na ukatikaji wa umeme wa hovyo utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kama si kuisha. Ila cha ajabu ndio Kwanza spidi imeongezeka

Mfano hapa Dumila iliyopo Kilosa mkoa wa Morogoro yaani umeme unaweza katika hata Wiki mfululizo Na Tanesco Wapo Tu hata ukilalamika Hakuna lolote Na huku mtandaoni nimelalamika vya kutosha wanaishia kukuona takataka Na hata wakikujibu wanakwambia tunafanyia Kazi Ila hakuna lolote lile zaidi ya meseji zao za kukop na kupaste

Sasa binafsi naona kabisa hii wizara imemshinda Na haswa aliposema bungeni kuwa Waziri Kalemani alipewa miaka minne ndipo akafanya vizur hivyo naye tumpe Muda HIVI ANAJIELEWA KWELI?

Kwa nini asingeendelea mwenzake alipoishia au Na yeye kaanza upya ili tuamiani ile dhana ya Mzee wa 10%

MAKAMBA HII WIZARA IMESHAKUSHINDA IACHE KWA AMANI KABLA HAIJAKUHARIBIA ZAIDI ila yote Kwa yote TANESCO Rudisheni umeme Dumila
 
Uliamini ile kauli ya mgao wa umeme Tanzania utakwisha baada ya siku kumi?! over my dead body. Waziri wa Nishati ni much know sana mdomoni lakini sio kwenye utendaji.

Makamba amelegea haswa, anapewa kero zinazoihusu wizara yake anajibu kama tatizo ni uwaziri au urais wa Samia, huyu jamaa anaficha udhaifu wake kwenye kivuli cha Rais, sasa wacha wote waangushiwe jumba bovu.
 
Wananchi ni mfano wa mwanamke bikra akikutana na mwanaume, atalalamika siku ya kwanza kuwa ni maumivu, siku ya pili atalalanika kiasi maumivu kwa mbali huku akianza kuizoea ile hali, siku ya tatu ataanza kuizoea kuizoea kabisa huku maumivu yakitoweka na siku ya nne anakua kashasahau kabisa na maisha yanaendelea kama kawaida huku akifurahia kabisa.

Mkuu ni hvi serikali huwa hawajali kulialia kwa wananchi wanajua kuwa tutazoea tu hii hali. Watu walilalamika masuala ya tozo kwenye miamala ya simu. Sasa hv kimya, bei za vifurushi kupanda sasa hv kimya, mfumuko wa bei kwnye bidhaa ila sasa hv kimyaa. WASHAZOEA NA MAISHA YANAENDELEA.
 
Ila toka amepewa wizara ya Nishati madudu yamekuwa makubwa zaidi haswa upandaji wa mafuta huku akijisifu kupunguza kodi wakati mafuta yanapanda
You are not serious dude! Hata kama ni chuki hii yako imezidi, yaani unamlaumu Waziri wa Nishati kwa kupanda bei ya mafuta.? Unajua bei ya mafuta kwa sasa kwenye soko la Dunia?
 
Waziri wa Nishati ni much know sana mdomoni lakini sio kwenye utendaji.
Alitakiwa apewe wizara ya sanaa na utamaduni anaweza sana kupiga poyoyo, mtu alikuwa mwandishi wa Hotuba wa Kikwete leo anaenda kuwa waziri wa Nishati wizara ambayo utendaji ndo Roho ya wizara. Huyu hafai ni bora hata wasimamishe mgomba hiyo wizara, Makamba hamna kitu pale!
 
Makamba ni mbunge wa CCM na kachaguliwa kuwa waziri na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM - Sisi twasema CCM ni walewale, sasa kama mna ugomvi bac malizaneni huko kwa huko sisi hautuhusu.
 
Back
Top Bottom