Elections 2010 Sasa Najiunga Na Chama Cha Siasa Rasmi

Mimi Watz wamenihisi nitamani tena kuishi 100+

Natangaza rasmi kujiunga na maswala ya kisiasa kuanzia siku niliyopiga kura yangu ya ukombozi. Naahidi kutokushinda tena kwenye jukwaa la mapenzi nimepata mwamko wa ajabu.
 
Nami nimgeni hapa JF na napenda kuwa mwanachama wa CHADEMA! Kwa kweli nimehamasika sana mwaka huu na napenda kazi ya kuelimisha wenzetu kuhusu mabadiliko ianze mapema zaidi ili ifikapo 2015 watu wengi zaidi wawe tayari kwa mabadiliko!!!
 
hongereni kwa kuona umuhimu wa kuifanyia kitu nchi yetu. Niweke angalizo kuwa hata CCM ilianzishwa kwa nia njema na taratibu ikaanza kuruhusu mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo na sasa sote ni mashahidi kuwq CCM is hijacked. Niwashauri tu kuwa moyo wa uzalendo ndio uwasukume kufanya hayo yote na mkithibitika kuwa vionfozi wazuri nitawasapoti. Pia mnaweza uliza namna ya kujiunga na chadema kupitia facebook za wahusika kama Dr. Slaa au Zitto. Pia sina hakika kama web ya chadema ina contact page!

Go and do something good for our country for you are a Tanzanian before you become a politicians.....all the best and be faithful!
A patriot.
 
Nimegundua siitendei haki CHADEMA na ndio maana wanatuonea. Nami natangaza rasmi nia ya kuchukua kadi ya uanachama wa CHADEMA baada ya ushabiki wa miaka 5
 
Nami pia! Nilidhani ktk maisha yangu sitakuwa mwanachama wa chama chochote, lakini natangaza rasmi kuwa sasa natafuta utaratibu wa kujiunga na CHADEMA!
 
safi kabisa,naomba unijulishe dar ofisi zao ziko wapi ili nikifika tu,kesho yake naenda kukamata kadi na kuwa mwanachana hai,nitaanza kampeni kijijini kwetu mwakani kwa ajili ya 2015.Watakoma sana Chama Cha Majambazi/mafisadi
 
safi kabisa,naomba unijulishe dar ofisi zao ziko wapi ili nikifika tu,kesho yake naenda kukamata kadi na kuwa mwanachana hai,nitaanza kampeni kijijini kwetu mwakani kwa ajili ya 2015.Watakoma sana Chama Cha Majambazi/mafisadi
Labda jaribu kupitia Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inaweza kuwa na maelekezo mazuri. Ukishindwa piga simu hizi za Mnyika 0754694553, 0784222222 atakujuza. Karibu Chadema mimi baada ya kukaa nje nikikipenda Chama hatimaye mwaka jana niliamua kujiunga baada ya kumsikia Mbowe akimwaga sera kwenye operation Sangara. Tulikuwa wengi tuliochukua kadi na tulipewa na Mbowe mwenyewe.
 
.....Hata mie bado nipo nipo tu, si mwanachama wa chama chochote cha siasa.......nilikuwa shabiki maandazi yaani nilikuwa nafuata upepo tu kama bendera.Hapa kweli watu mmeonyesha mwamko lakini jamani hebu muwe serious kufungua matawi mengi ya chadema hata huko vijijini hapo ndipo mtatambulika.
 
Kweli tujiunge uanachama tukichangie kwa hali na mali ili kuweza kuwa na mtandao kila kijiji kama ccm tukiweza hilo direct ticket to Ikulu.Kama safari hii tuko hivi halafu tunakaribia majimbo 30,sa embu fikiria tukijizatiti.Kujiunga haina masharti magumu tafadhali fika katika ofisi za chadema zilizo karibu nawe uchukue form na maelzo utapewa.Chadema ni ya watanzania.
 
Naunga mkono hoja na nashauri kwa kuwa ni chama cha NGUVU YA UMMA kama ilivyofanyika wakati wa kampeni wananchi wakishirikishwa naamini watachangia na wabunge wa CHADEMA ndo tegemeo la wananchi kwa sasa ndani ya BUNGE tusiwaangushe watanzania wote ndani ya majimbo yetu na yasiyo yetu. Wabunge na viongozi CHADEMA WAHAKIKISHE NDANI YA MIAKA 3 ANGALAU TUWE TUMEFIKA KILA KATA KUSHUKURU NA KUSIKILIZA MAONI YAO NA KUSAJIRI WANACHAMA. Ni ngumu ila inawezekana tukiunganisha nguvu zetu chini ya katibu wetu DR SLAA. My take TUKISHINDWA KUPANGA TUMEPANGA KUSHINDWA hasa kwa nchi iliyo jikatia tamaa kama Tz:yield::smile:
 
mimi nitajiunga na nataka pia nikafungue matawi mapya ya CHADEMA huko lushoto vijijini mapema sana, pia nitatembelea shule zote za kata za jimbo langu nianze kuwapa watu elimu ya uraia. nitaomba CHADEMA wanipe utaratibu wa jinsi ya kwenda kuanzisha matawi ya CHADEMA huko.
 
hata mimi ccm nilikuwa naichukia toka kipindi cha mageuzi nikawa mwana nccr baada ya kutuvuruga nikaacha na kurudi ccm lakini sasa kutokana hali hii nimeichana kadi ya ccm.Hapa nilipo nataka kadi ya chadema sijui nitapataje sasa hivi nipo belgium masomo
 
Nashukuru wananchi mnaoipenda Tz mnaamka nami nipo nanyi. Tovuti ya Chadema huwa hawajibu mfano nililodge request yangu mwezi juzi lakini mpaka leo sijajibiwa,najua wako bize siwezi laumu. My request: NATAKA KUPELEKA PROPOSAL KWA Dr.SLAA PALE UFIPA HQ ILI CHADEMA IWE NA TAWI MTANDAONI HAPA JF. Tuwe na kadi za Chadema lakini ni Tawi mtandao hapa Jf pia mwanachama yeyote wa tawi la kawaida anaweza kuwa mwanachama wetu,mtandao/internet itasaidia kufikia watu wengi,kupeana taarifa wenyewe bila watu kujua si watu wa tigo,zain wala voda watapata mawasiliano yetu! Hii munaionaje wasomi wanamageuzi? Jaman tupo wengi,ni tawi tosha,kumbuka jf voters wa dr.SLAA tulikuwa over 6700 tunatosha kuunda tawi hapa Jf au vipi?! Nawasilisha.
 
Mimi nina kadi ya CCM toka 1986. Niliipata mkoani Iringa. Sijawahi ilipia. Ni mwanachama mfu, kama Dr. Azaveli.

Sasa nataka kuwa active member wa Chadema.
 
hata mimi mwanzoni nilikuwa nccr ila nilirudi ccm baada ya mrema na wenzake kuvuruga mageuzi.Slaa nilikuwa naipenda ingawa nilikuwa ccm nikawa naangalia msimamo wake isije ikawa kama mrema.lakini sasa ninajiunga rasmi na chadema ila tatizo nipo belgium kimasomo kadi nitapata wapi au nasi tuanzishe tawi letu kama ccm uk
 
Back
Top Bottom