Elections 2010 Sasa Najiunga Na Chama Cha Siasa Rasmi

mimi nimeshajiunga uanachama wa CHADEMA na nimehamasisha wamama wengine kama 4 na wameshajiunga tuko A towm maeneo ya kijenge na sitaishia hapo wandugu zangu huko mto wa mbu ndio wananisikitisha sana wanamuona EL kama mungu fulani hivi na huko nako nitaanza za chini chini mpaka kieleweke.
Tutafutane tuunganishe nguvu hii...! Nami natamani kupata support ya kuunganisha nguvu ili tuing'oe kisiki fulani, bado naogopa kukitaja lakini lazima niombee kwa Mungu na kuiwekea mikakati hiyo...! Please, I need your support especially to convince women...!
 
tunakuomba INVISIBLE popote ulipo utufungulie Jukwaa letu la CHADEMA, mimi pia nitajiunga na Chadema Katikati ya mwezi huu.
 
Naunga mkono hoja, vidole viwili salamu na ishara yetu daima!!
 
Wajameni, Profession yangu hainiruhusu kuwa na kadi ya chama cha siasa lakini I am sorry nitajiunga na Chadema tu.

Hakuna Marefu Yasiyokuwa na Ncha
 
Uchaguzi wa mwaka 2010 umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu.

Baada ya kuishi miaka 30(umri wangu) katika maisha ya mazoea na kukata tamaa, sasa nina amini nchi hii kuna watu wanaoweza kuwaamsha Watanzania na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiutawala yanayoweza kuleta uwiano wenye usawa kimaisha katika jamii.

Jamii nyingi za Watanzania hasa vijijini ni masikini, na wengi wanadhani kuwa Mungu aliwaumba kuwa masikini na hawajui kazi ya viongozi wa kisiasa.

Ki ufupi ni kwamba ninatangaza kupitia jamii forums kuwa Ninajiunga na Chadema Rasmi.

2005 nilikipigia kura nikiwa namtambua Mbowe(Freeman).
Zito kabwe nilianza kumsikia kwenye sakata la Amina Chifupa (marehemu) kupitia magazeti ya Udaku.

Nilishtuka pale nilipojua kuwa kumbe hata Professa Gwiji la Siasa za Kimataifa, Mwesiga Baregu naye pia ni mwanachama wa chama hiki makini.

Heshima kwa Mzee Mtei.

Heshima kwa Wibroa Slaa (PhD)

Heshima kwa mwana harakati Tundu Lisu

Heshima kwa Mpiganaji Rastafarai Chacha Zakayo Wangwe (Mungu Amlaze mahala pema)

Heshima kwa Damu ya Nyerere (Vincent Nyerere, Leticia).

Watanzania Wenzangu.

Hakuna haja ya kupigana. Hakuna haja ya kutamani kufa.

Ukombozi wa chi hii upo karibu.

Matokeo ya Mwaka 2010 nimeyavulia kofia.

Sasa Tuanze na Operation Nyangumi. Twende Vijijini. Tukawaamshe

Du! mkuu umenikuana kidogo hapo juu ulipoweka baadhi ya majina miongoni mwao wakiwa MACHAMPION WA CHADEMA, lakini kuna jina moja umelisahu, JAJI MSTAAFU, BOB MAKANI ame play big part katika maendeleo ya CHADEMA.
 
mimi nilikuwa mwanachama wa NCCR- Mageuzi lakini sijalipia kadi ya pata miaka kumi hivi! hivyo uanachama wangu ulishakufa, basi nami sina budi kutangaza rasmi kujiunga na CHADEMA, wala sioni taabu nitatembea kifua mbele kwa sababu ya kazi waliofanya akina Mbowe, Slaa, Zito, Mdee na wengineo, Wadau nifahamisheni ofisi za CHADEMA Segerea ziko wapi!

Sasa tunapaswa kukikuza chama zaidi ili tuweze kuchukua nchi ifikapo mwaka 2015,
wakati CCm wanatibu majeraha ya makundi Chadema imarisha chama. Naunga Mkono Operation Nyangumi!
 
Tutafutane tuunganishe nguvu hii...! Nami natamani kupata support ya kuunganisha nguvu ili tuing'oe kisiki fulani, bado naogopa kukitaja lakini lazima niombee kwa Mungu na kuiwekea mikakati hiyo...! Please, I need your support especially to convince women...!

Jimbo langu wamepitisha mbunge wa CCM bila kupingwa wakati ni masikini wa kutupwa??

Naomba uhai.

2015 nagombea mwenyewe. Kwa tiketi ya Chadema

Nimekulia huko. Wananijua mtoto wao.
 
Nafikiri tupo wengi sana ambao tulikuwa mashabiki wa CHADEMA na sasa tutakuwa wanachama halisi. Mimi na nyumba yangu (familia yangu) ni miongoni mwao na nina uchungu sana na kuikomboa Ruvuma, hasa wilaya ya Mbinga. Hiyo operation nitaomba ikaanzie huko. Hakika nimefurahishwa sana na watu wa kigoma, Mbeya, mwanza, Dar n.k. Hii ni dalili njema katika nchi hii.
 
Karibuni sana wanaharakati,wapiganaji naomba muwe waalimu kwa wanachi hasa mikoa masikini kuliko(Iringa(V),Dodoma,Singida ,Pwani,Morogoro,Lindi n.k Watu wanaona umasikini ni haki yao we need a great Change. Vijana amkeni. Ila nilisikitaka sana niliposikia Vijana wa UDOM wamechanga hela za mkopo(Tirdo) Tsh 1,000,000) kumuwezesha Mr Kikwete kuchukua fomu ya urahisi. Nyie watu wa UDOM mlikuwa hamna uhakika kuwa mtasomaa,naamini wengi ni wwatoto wa wkulima tena wengine ni waalimu wa Crsh Program mishahara ya 165,000 inawapa vibuli ee? Tuwasaidie wazazi tuliowaacha vjjini waliokata tamaa. U dom kunahitaji mabadiliko. Thts y sisi wasomi tunawasiwasi na vyeti vyenu na elimu inayotolewa hapo . Wanaharakati tufanye oparesheni pasua pale UDOM.
 
Uchaguzi wa mwaka 2010 umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu.

Baada ya kuishi miaka 30(umri wangu) katika maisha ya mazoea na kukata tamaa, sasa nina amini nchi hii kuna watu wanaoweza kuwaamsha Watanzania na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiutawala yanayoweza kuleta uwiano wenye usawa kimaisha katika jamii.

Jamii nyingi za Watanzania hasa vijijini ni masikini, na wengi wanadhani kuwa Mungu aliwaumba kuwa masikini na hawajui kazi ya viongozi wa kisiasa.

Ki ufupi ni kwamba ninatangaza kupitia jamii forums kuwa Ninajiunga na Chadema Rasmi.

2005 nilikipigia kura nikiwa namtambua Mbowe(Freeman).
Zito kabwe nilianza kumsikia kwenye sakata la Amina Chifupa (marehemu) kupitia magazeti ya Udaku.

Nilishtuka pale nilipojua kuwa kumbe hata Professa Gwiji la Siasa za Kimataifa, Mwesiga Baregu naye pia ni mwanachama wa chama hiki makini.

Heshima kwa Mzee Mtei.

Heshima kwa Wibroa Slaa (PhD)

Heshima kwa mwana harakati Tundu Lisu

Heshima kwa Mpiganaji Rastafarai Chacha Zakayo Wangwe (Mungu Amlaze mahala pema)

Heshima kwa Damu ya Nyerere (Vincent Nyerere, Leticia).

Watanzania Wenzangu.

Hakuna haja ya kupigana. Hakuna haja ya kutamani kufa.

Ukombozi wa chi hii upo karibu.

Matokeo ya Mwaka 2010 nimeyavulia kofia.

Sasa Tuanze na Operation Nyangumi. Twende Vijijini. Tukawaamshe

Unapoona umuhimu wa kuandika PhD basi pia uone umuhimu wa kuandika PhD ya kitu gani. Ni PhD ya Sheria za Kanisa!
 
Naunga mkono hoja. Kweli kabisa lazima pawe na campeni za makusudi kwenda vijijini na kuwaamsha waliolala. Mimi binafsi niko tayari kutumia muda wangu kulifanya hilo.
 
Naunga mkono hoja. Kweli kabisa lazima pawe na campeni za makusudi kwenda vijijini na kuwaamsha waliolala. Mimi binafsi niko tayari kutumia muda wangu kulifanya hilo.

Panda basi na anza safari ya vijijini immediately! No time wasting please! Teh teh teh!!!!
 
Yaani umepatia kabisa! Ndivyo nilivyopata matumaini mapya uchaguzi wa mwaka huu. Kabla ya hapo hata kupiga kura nilikuwa nikiona ni kazi bure. Lakini uchaguzi wa mwaka huu umenipa matumaini ya ukombozi. Sitanyongea tena maana najua hata watoto wangu na wajukuu zangu watakuja kuishi Tanzania bora baada ya miaka hii 5. Huu ni mwanzo tu wa ukombozi. Hongera sana CHADEMA. Mumtunze Mzee wetu Dr. msimzeeshe na mijikazi kibaaaaoooo, mumpe wasaidizi, mumpe amani tumpigie debe na kura kwa wingi nchi nzima akionekana kijana zaidi kuliko mwaka huu. Nina raha sana jamani. :clap2::clap2::clap2:

Mwaka 2015 hakuna hata mtu atakayepita bila kupingwa lazima kuwa na wagombea wazuri na wanaofahamika katika kila jimbo. kazi ya kuelimisha wananchi na kueleza sera na mipango ya chama lazima ianze leo na si kesho. Nami, kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, nitakuwa katika kinyang'anyiro hicho nadhani hilo jimbo la Kinondoni litanifaa. Kitaeleweka
 
Mkuu Ng'wanangwa,
hapa niliyo nina uchungu na hasira sanaa...tena sana, kwa sababu hiyo, tangu jana nimeshindwa kufanya kazi inavyotakiwa.
But, hii thread uliyoanzisha inaleta matumaini kwamba tunatakiwa kuangalia mbele zaidi wakati tunapopita katika kipindi cha majaribio kama hiki cha sasa..
 
Back
Top Bottom