Sasa Najiunga Na Chama Cha Siasa Rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa Najiunga Na Chama Cha Siasa Rasmi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Nov 3, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa mwaka 2010 umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu.

  Baada ya kuishi miaka 30(umri wangu) katika maisha ya mazoea na kukata tamaa, sasa nina amini nchi hii kuna watu wanaoweza kuwaamsha Watanzania na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiutawala yanayoweza kuleta uwiano wenye usawa kimaisha katika jamii.

  Jamii nyingi za Watanzania hasa vijijini ni masikini, na wengi wanadhani kuwa Mungu aliwaumba kuwa masikini na hawajui kazi ya viongozi wa kisiasa.


  Ki ufupi ni kwamba ninatangaza kupitia jamii forums kuwa Ninajiunga na Chadema Rasmi.

  2005 nilikipigia kura nikiwa namtambua Mbowe(Freeman).
  Zito kabwe nilianza kumsikia kwenye sakata la Amina Chifupa (marehemu) kupitia magazeti ya Udaku.

  Nilishtuka pale nilipojua kuwa kumbe hata Professa Gwiji la Siasa za Kimataifa, Mwesiga Baregu naye pia ni mwanachama wa chama hiki makini.

  Heshima kwa Mzee Mtei.

  Heshima kwa Wibroa Slaa (PhD)

  Heshima kwa mwana harakati Tundu Lisu

  Heshima kwa Mpiganaji Rastafarai Chacha Zakayo Wangwe (Mungu Amlaze mahala pema)

  Heshima kwa Damu ya Nyerere (Vincent Nyerere, Leticia).

  Watanzania Wenzangu.

  Hakuna haja ya kupigana. Hakuna haja ya kutamani kufa.

  Ukombozi wa chi hii upo karibu.

  Matokeo ya Mwaka 2010 nimeyavulia kofia.

  Sasa Tuanze na Operation Nyangumi. Twende Vijijini. Tukawaamshe
   
 2. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Yaani umepatia kabisa! Ndivyo nilivyopata matumaini mapya uchaguzi wa mwaka huu. Kabla ya hapo hata kupiga kura nilikuwa nikiona ni kazi bure. Lakini uchaguzi wa mwaka huu umenipa matumaini ya ukombozi. Sitanyongea tena maana najua hata watoto wangu na wajukuu zangu watakuja kuishi Tanzania bora baada ya miaka hii 5. Huu ni mwanzo tu wa ukombozi. Hongera sana CHADEMA. Mumtunze Mzee wetu Dr. msimzeeshe na mijikazi kibaaaaoooo, mumpe wasaidizi, mumpe amani tumpigie debe na kura kwa wingi nchi nzima akionekana kijana zaidi kuliko mwaka huu. Nina raha sana jamani. :clap2::clap2::clap2:
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  chademaaaaaaaaaaaa,mimi ni shabiki wa siasa hasa za chadema ila mwaka huu kabla haujaisha mimi nitakua mwanachama halali na halisi wa chadema
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  safi sana amkeni tujiunde upya vijana tutaikomboa hii nchi 2015.
   
 5. B

  Brandon JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 336
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi pia nimepata mwamko mpya kabisa. Ninataka kupata kadi ya chadema niwe mwanachama. Naomba mnisaidie ofisi za chadema hapa maeneo ya ubungo nhc yapo wapi?
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  The Following User Says Thank You to Ng'wanangwa For This Useful Post:

  The Finest (Today) ​
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa kumekucha watanzania tuamkeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 8. T

  The King JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi pia niko mbioni kuzifahamu taratibu za kuomba uanachama chadema ili nitume maombi ya kuwa mwanachama wa chama hicho.

  Mimi naamini kabisa kuna uchakachuaji wa hali ya juu uliofanywa kwa kutumia form za uwongo katika matokeo mengi ya Madiwani, Ubunge na Urais na pia kutumia IT kama ambavyo alivyoelezea mwanachama mmoja wa jamvi hili na kuyaweka majina ya wahusika wa uchakachuaji kupitia IT.

  Haiwezekani kabisa katika majimbo mengi ambayo wabunge wa chadema wameshinda kwa kura nyingi lakini kwenye kura za Urais aliyeshinda ni mkwere, na pia tuliona na kusikia kampeni za Dr Slaa katika sehemu mbali mbali nchini, kampeni ambazo wengine ziliwagusa hadi kutoa machozi halafu hawa kitengo cha thithiem NEC wanataka tuamini kwamba Dr Slaa amepata kura chache kuliko hata Lipumba ambaye hakuwa na mvuto kama wa Dr Slaa katika sehemu alizofanyia kampeni zake. Maombi yangu kwa wale wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu wakati umefika sasa wa kujiunga na chadema kwa wingi sana na pia kuwashawishi ndugu, jamaa, marafiki na majirani umuhimu wa kujiunga na chadema.
   
 9. coby

  coby JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa nina uhakika CHADEMA ni chama makini kuliko vyote nchi hii. cha muhimu kufanyika sasa hivi ni kuhakikisha kinapenyeza matawi yake hadi vijijini na kuwahamasisha vijana wengi zaidi wajitokeze kujiandikisha upigaji kura mara zoezi hilo linapofanyika. kwa sasa kimefaulu kupenyeza madiwani na wabunge katika kila kanda ukiacha zanzibar, hawa wanaweza kutumika kuendelea kukijenga chama zaidi na kuweka mizizi isiyoweza kuteteleka. Mpango huo ni vizuri ukaanza sasa ili kufikia 2015 tufanye suprise kwa CCM na kukiweka rasmi kuwa chama cha upinzani. ukweli ni kwamba safari hii hatukujiandaa kulinda kura za uraisi, tumeacha zikichakachuliwa wakati tukigombana na kura za ubunge
   
 10. b

  bojuka Senior Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ''Sasa Tuanze na Operation Nyangumi. Twende Vijijini. Tukawaamshe'' . umemalizia vyema lkn tusipende mabadiliko bila kushiriki ktk mabadililko hayo .NO PAINS NO GAINS, ITS A GOOD START LETS GO ON.:llama::whoo::fish2:
   
 11. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Naunga hoja
   
 12. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nami pia najiunga rasmi na chadema.
  mtaani kwetu tunaanzisha tawi ambalo litakuwa matata sana,wataalamu wa nyanja zote ndani.
  hatuachi kitu mtaani kuanzia sasa tunaanza uchaguzi wa serikali za mitaa. tunabeba kimoja kimoja mpaka urais i mean kiongozi wa mtaa,diwani,mbunge na rais. kwa sasa tumeshinda Mbunge(Kawe) kwa shida kidogo. next time tunataka tushinde hadi waone aibu hata kuyasogelea matokeo. Believe me tunaweza tena sana.

  Wanamageuzi wenzangu huu sio muda wa kuchangia mabadiliko ukiwa nje ya ulingo....njooni tuingie ndani kwa nguvu kubwa. tunatakiwa kupanga mikakati ya kuwaingiza ndani akina Ulimwengu,lwaitama,Mama Nkya,Mwakitwange and the likes we really need them now not later.
  tumehujumiwa matokeo kutokana na uoga wa mawakala sehemu nyingi sana na sehemu hawakuwa hata na uwezo wa kujumlisha.....i am 33yrs lakini sitagombea nafasi za juu mpaka nitumikie chama kwa at least 10yrs ndo nitajievaluate kuhusu kugombea nafasi za ubunge na kuendelea ila kwa sasa nitawezesha nikiwa ndani ya nyumba.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kweli na mm natangaza nia rasmi kujiunga na chadema rasmi
   
 14. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  du" hata mimi wazee nachukua kadi hivi punde. i thought i will never do politcs sababu nilijua kwa nchi hii ni kama mchezo wa kuigiza, but for now atleast i can see the light. its possible and it begins with me,
   
 15. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ninakuunga mkono, mimi nimeamua rasmi kujishughulisha na siasa tangu pale niliposoma quote hii maarufu ya gwiji Plato "The punishment which the wise suffer who refuse to take part in the government, is to live under the government of worse men."
  Nilishajiunga na Chadema mapema kupitia sms lakini sikuwahi kujua ofisi zao zilipo, hivyo sikufika mbali. Ninaomba kama kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA anayesoma thread hii, aitishe mkutano wa wapenzi na washabiki wa Chadema ili kuwasajiri rasmi kama wanachama na wanaharakati wa ukombozi wa kweli wa Tanzania. Harakati hizi zinatakiwa zianze mara moja, tunataka 2015 nchi hii iwe chini ya utawala mpya wa CHADEMA.
   
 16. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  mimi nimeshajiunga uanachama wa CHADEMA na nimehamasisha wamama wengine kama 4 na wameshajiunga tuko A towm maeneo ya kijenge na sitaishia hapo wandugu zangu huko mto wa mbu ndio wananisikitisha sana wanamuona EL kama mungu fulani hivi na huko nako nitaanza za chini chini mpaka kieleweke.
   
 17. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Pia mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa kama Ng'wanangwa. Nami natangaza rasmi kupitia JF ninajiunga na CHADEMA rasmi.
   
 18. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kweli muda wa kufanya mabadiliko nchi hii umewadia!
  Tuungane tuikomboe nchi yetu Tajiri sana
   
 19. s

  sauti Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimependa quote ya plato, na ni ukweli kabisaa, nami nachukua kadi kabla ya mwaka huu kuisha!
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Operation Nyangumi!! hiyo safi sana.
   
Loading...