.....Hata mie bado nipo nipo tu, si mwanachama wa chama chochote cha siasa.......nilikuwa shabiki maandazi yaani nilikuwa nafuata upepo tu kama bendera.Hapa kweli watu mmeonyesha mwamko lakini jamani hebu muwe serious kufungua matawi mengi ya chadema hata huko vijijini hapo ndipo mtatambulika.
Nadhani hili si jukumu la Dr Slaa, Mnyika, Tundu Lisu Kitila, Baregu au Marando pekee, ni jukumu letu sote, chukua kadi ya chama, nunua bendera na sogeza chama mtaani kwako.
Ukombozi uanze sasa
Mimi ni mwanachama wa CHADEMA tangu 2004 lakini sasa natangaza rasmi kuingia kwenye siasa za majukwaani, nitagombea ubunge uchaguzi ujao