Sasa itoshe basi,CCM na Bulembo acheni kutusakama Walutheri

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,384
Nafikiri JF kipindi hiki saidieni kutupa nafasi ya kuwabana viongozi wapuuzi - kama kweli watu wa aina ya Abdallah Bulembo wanafaa kuitwa viongozi

Nikiwa Mlutheri na shabiki wa Magufuli,jana nikiwa na familia yangu tuliamua kufika katika viwanja vya People's katika mji wa Singida kumsikiliza Ndg.Magufuli aliyekuwa na mkutano hapa - lakini kwa hakika nilifedheheshwa na kauli za Ndg.Bulembo kwamba Lowassa abaki na kura za Walutheri na Wakristo wa Kanisa la Gwajima lkn asahau kura za Wakatoliki,Waislam na watu wa madhehebu mengine;na ni ajabu yeye kutamka vile mbele ya viongozi Walutheri Lazaro Nyalandu,Mwigulu Nchemba na Diana Chilolo ambao wote walikuwepo jukwaa kuu na walipata nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo.

CCM wanapaswa kumkemea Bulembo na hata ikibidi amwondoe kwenye msafara wa Ndg.Magufuli - sasa kwamba maana yake nini,kwamba sasa CCM wamekwishaamua kuwa hawahitaji kura za Walutheri na kwamba sisi Walutheri ni watu wabaya tunaopaswa kusimangwa kila siku kwenye mikutano ya kampeni za CCM?Jambo hili halikubaliki hata kidogo

Nachelea kusema kuwa watu aina ya Bulembo ni hatari sana na wakiachwa waendelee na upuuzi wao wataifikisha nchi yetu kwny machafuko sawa na yale ya makundi ya Seleka na Anti Balaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati
 
Usipoteze muda kumjadili bulembo, pambana kumtafutia kura EL, bulembo Hana madhara yule!! Kashfa ndio sera ya CCM.
 
Hata Mimi kwa Mara ya kwanza nilipomsikiliza bulembo nilimstahi kuwa labda kateleza lakini nilipomsikia tena nimejikuta naanza kumchukia bulembo kuliko shetani,na hata kura Yangu ntaipa hata chauma
 
Na ndiyo anazidi kufanya walutheri wakasirike na kumtosa magufuli, kwani walutheri ni wanyama.?, walutheri ni binadamu wenye fikira na maamuzi kama binadamu wengine ila ni wavumilivu sana, ingekuwa waislamu moto ungeshawaka
 
Nafikiri JF kipindi hiki saidieni kutupa nafasi ya kuwabana viongozi wapuuzi - kama kweli watu wa aina ya Abdallah Bulembo wanafaa kuitwa viongozi

Nikiwa Mlutheri na shabiki wa Magufuli,jana nikiwa na familia yangu tuliamua kufika katika viwanja vya People's katika mji wa Singida kumsikiliza Ndg.Magufuli aliyekuwa na mkutano hapa - lakini kwa hakika nilifedheheshwa na kauli za Ndg.Bulembo kwamba Lowassa abaki na kura za Walutheri na Wakristo wa Kanisa la Gwajima lkn asahau kura za Wakatoliki,Waislam na watu wa madhehebu mengine;na ni ajabu yeye kutamka vile mbele ya viongozi Walutheri Lazaro Nyalandu,Mwigulu Nchemba na Diana Chilolo ambao wote walikuwepo jukwaa kuu na walipata nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo.

CCM wanapaswa kumkemea Bulembo na hata ikibidi amwondoe kwenye msafara wa Ndg.Magufuli - sasa kwamba maana yake nini,kwamba sasa CCM wamekwishaamua kuwa hawahitaji kura za Walutheri na kwamba sisi Walutheri ni watu wabaya tunaopaswa kusimangwa kila siku kwenye mikutano ya kampeni za CCM?Jambo hili halikubaliki hata kidogo

Nachelea kusema kuwa watu aina ya Bulembo ni hatari sana na wakiachwa waendelee na upuuzi wao wataifikisha nchi yetu kwny machafuko sawa na yale ya makundi ya Seleka na Anti Balaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ungefanya la maana pia kutaka lowassa akemewe kwa kuleta udini
 
Ni afadhali Burembo kuliko wewe mpika na mgeuza habari na majungu,kwa ulichokiandika wewe ndiye msambaza chuki za udini,alichokifanya Lowasa haikua sawa lakini pia unachokifanya wewe si sawa pia,kimtizamo, na kwa mwenye akili ataelewa kwamba na wewe ni msambaza chuki za udini humu mitandaoni,wewe unasambaza chuki kwa walutheri dhidi ya madhehebu mengine,watanzania tuache haya mambo ni upumbavu na hatari kwa taifa.
 
Ungefanya la maana pia kutaka lowassa akemewe kwa kuleta udini

Kasikilize ile kanda uone uongo wa Urembo na CCM. Tunachoshangaa ni kuwa mbona hawakemewi kwa kuendelea na uzushi, uchochezi. NEC vipi?
 
Wakumlaumu ni lowasa aliyekwenda kupiga kampeni kanisani akidhani ni hao tu ndio wanatosha kumfikisha ikulu
CCM haipendi Walutheri wote ndo maana inawatukana majukwaani! Wameishiwa hoja hawa! Mwisho wao umefika!
 
Ungefanya la maana pia kutaka lowassa akemewe kwa kuleta udini

Udini unaletwa na hao wanaozidi kuusambaza, kama lowasa alitamka kanisani, alishakemewa na tume ya taifa ya uchaguzi na ccm walishasema, sasa inakuwaje kila siku dini! dini! dini! Acheni ungese; nyie ndiyo mnaleta udini.
 
CCM wanapinga udini kidogo kwa kufanya udini mkubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Safari hii ccm wameamua kulivunja taifa vipande vipande ila kwa neema ya Mungu tutafika salama!
 
Back
Top Bottom