Sasa itoshe basi,CCM na Bulembo acheni kutusakama Walutheri

Sasa itoshe basi,CCM na Bulembo acheni kutusakama Walutheri

Bulembo ni aina ya wanasiasa wapuuzi kabisa kuwai kutokea ndani ya nchi hii.
 
Ccm ni tatizo kubwa sana katika hii nchi. Hatupaswi kuwapa kura tena. Wapumzike ili nchi nayo ipumue khaaaa!!?
 
Mimi Mkatoriki ila ntampigia Lowasa.... ni ukosefu wa busara kutamka hayo maneno mbele ya halaiki....
 
Nafikiri JF kipindi hiki saidieni kutupa nafasi ya kuwabana viongozi wapuuzi - kama kweli watu wa aina ya Abdallah Bulembo wanafaa kuitwa viongozi

Nikiwa Mlutheri na shabiki wa Magufuli,jana nikiwa na familia yangu tuliamua kufika katika viwanja vya People's katika mji wa Singida kumsikiliza Ndg.Magufuli aliyekuwa na mkutano hapa - lakini kwa hakika nilifedheheshwa na kauli za Ndg.Bulembo kwamba Lowassa abaki na kura za Walutheri na Wakristo wa Kanisa la Gwajima lkn asahau kura za Wakatoliki,Waislam na watu wa madhehebu mengine;na ni ajabu yeye kutamka vile mbele ya viongozi Walutheri Lazaro Nyalandu,Mwigulu Nchemba na Diana Chilolo ambao wote walikuwepo jukwaa kuu na walipata nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo.

CCM wanapaswa kumkemea Bulembo na hata ikibidi amwondoe kwenye msafara wa Ndg.Magufuli - sasa kwamba maana yake nini,kwamba sasa CCM wamekwishaamua kuwa hawahitaji kura za Walutheri na kwamba sisi Walutheri ni watu wabaya tunaopaswa kusimangwa kila siku kwenye mikutano ya kampeni za CCM?Jambo hili halikubaliki hata kidogo

Nachelea kusema kuwa watu aina ya Bulembo ni hatari sana na wakiachwa waendelee na upuuzi wao wataifikisha nchi yetu kwny machafuko sawa na yale ya makundi ya Seleka na Anti Balaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Na wewe 'jiongeze'.

Kama wewe haulikubali siyo lazima ulowataja hapo nao wasilikubali.
Pana nuru watu hawaoni. Watu wa Muumba wanaangamia kwa kukosa maarifa!
Ukiendelea kusubiri watu wote wakataye jambo unaloamini kuwa siyo sahihi ndo utende; utasubiri saaaana; mwisho utatenda dhambi ya kukata tamaa
 
Poa waendwlee tu kututukana na sisi tuna moyo wa nyama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom