Mimi niko hapa samakisamaki (usiniulize ya wapi), nimemaliza kula nasubiri waniletee bia yangu,weekend ndo ishaanza. Natamani sana ile mvua ya jana ije tena ila tu isifanye uhabiribu,ikinyesha inafanya hali ya hewa kuwa nzuri sana.
wakati mvua inanyesha watu woooote wanakuwa na furaha,sababu mawazo asilimia kubwa yanafikiria mvua,ni ngumu sana kuichukia mvua,inaondoa stress,nadhani Mungu ufungulia mabomba ya maji mvua ishuke itupe faraja ya moyo,njia za Mungu ni nyingi hakuna awezaye kuzijua.
binafsi ikinyesha na nikawa napata bia yangu,najisikia raha sana, yaani mpaka naona haiwezekani hata siku moja binaadamu wakajiingiza kwenye mambo ya kuuana katika hali ya namna hii.
mvua nyeesha