uhayawani wa kiumbe kiitwacho mwanadamu, mnyama hawezi kufanya haya...nini basi maana halisi ya maisha? Sanaa ya kifo ina mengi ya kutafakari...!kwanini kwenye maisha kuwe na vitu vya kuumiza kiasi hiki ? kwanini mmoja aishi maisha ya raha kuanzia kuzaliwa mpaka kifo wakati mwingine akiishi maisha ya mateso kuanzia kuzaliwa mpaka kifo? ??![]()
I can sense the vibrations in your tone...nakuombea upate wepesi ASAPHii picha inaniumiza sana kila ninapoiona, ila leo imeniumiza zaidi. Kwa bahati mbaya leo nimeiona huku nikiwa siko sawa kabisa, kuna vitu vinanisumbua sana kuviwaza ili nipate ufumbuzi.
Hii picha imezidi niharibia siku yangu. Imeniharibia sana, I wish ningemuona huyu mtu aliyefanya huyu mama akalala usingizi huu wa milele na kumuacha kipenzi chake, rafiki yake, mwanawe mpenzi.
Nisingejali ni mtu wa namna gani, ningemwadhibu kwa kiasi kilekile alichomwadhibu mtoto huyu kwa kumuondolea tumaini lake, mama yake mpenzi. Kwanini maisha yana nafasi ya wengine kuteseka hivi?
Ova
I can sense the vibrations in your tone...nakuombea upate wepesi ASAP
Sehemu ya pili
Kwahiyo hiyo kwa wale wafu ni kwamba wamekwenda kwenye hatua nyingine ya maisha wameingia kwenye daraja lingine wamefaulu mtihani wa kifo ndio maana wamevuka na kuendelea...kwahiyo kifo ni mafanikio....kwahiyo kama bado unaishi maana yake ni kwamba hujafikia hatua ya kwenda kifoni au umefeli mtihani wake...![]()
Hapa duniani tupo binadamu tunaokadiriwa kufikia bilioni sita wake kwa waume ni katika dakika hizi zenye sekunde sitini masaa 24 siku Saba na miezi 12 watu hufaulu kuingia kwenye daraja lingine la maisha
Kifo ni siri kama ulivyo mtihani ni wale tu wanaofaulu ndio huifahamu siri hiyo...! Tumeshawahi kusikia watu wakisema kuwa Eti fulani kanusurika kifo! Huyu hajanusurika bali kafeli mtihani wa kifo
Siri iliyo wazi ni kwamba kila mwanadamu ana siku saa na dakika yake ya kufanya mtihani wa kifo kufaulu na hatimaye kuendelea mbele
kweli elimu haina mwisho.......huishi kinishangaza mshana!!!! Eeh hilo la kifo bado najaribu kuchanganya na akili yangu nijue nimeelewaje!!je basi yafaa kusema; pumzika mahala ulipopachagua ulipokuwa duniani? Badala pumzika kwa amani?Sehemu ya tatu
Ukisoma katika maandiko yote ya kidini na philosophia za dini yoyote ile hata ile ya mashetani kila moja inakiri kuwa kifo sio mwisho wa maisha bali ni mwanzo wa kuingia katika hatua nyingine ya maisha kama kwenda mbinguni jehanam/motoni/kuzimu au kuzaliwa tena katika umbo lingine kwa zile imani nyinginezo![]()
Kama vile tunavyofaulu mitihani ya kielimu na kupata daraja fulani au kupanda daraja fulani na kupangiwa darasa chuo au kazi fulani sehemu tofauti na classmates wako ndio hivyo hivyo hata kwenye kifo...si kila mtu baada ya kifo atakwenda akhera au peponi, kila mmoja wetu atakwenda sehemu yake kwa style yake na kwa muda wake kutokana na uchaguzi wake na kufaulu kwake (uchaguzi huu huja kulingana na matakwa ya maisha yako ya duniani)
Furaha tuliyo nayo ndugu zetu wanapofaulu mitihani yao ndio furaha tunayopaswa kuwa nayo hata wapendwa wetu wanapofaulu kutwaliwa toka ulimwengu huu na kuingia ulimwengu mwingine....
Sanaa ya kifo ni fumbo tata ni nahau tasa ni philosophia iliyokengeuka kanuni na uelewa wa dunia ya kufikirika
Jaribu kujiuliza unapata hisia gani unapoambiwa mtu kafa kwa kujinyonga kunywa sumu ajali ugonjwa kuuliza nk nk!huwa tunahitimisha kwa kusema ni Majaliwa ya Mwenyezi Mungu! Ameyataka mwenyewe!zake zilikuwa zimefika! Nk nk...! Kamwe hatusumbuki kuufumua na kuushughulisha ufahamu wetu kwa kutafakari dakika zile za mwisho marehemu alikuwa katika hali gani aliwaza nini alijisikiaje alihisi nini aliona nini na hata kama ni wauaji maswali ni hayo hayo
Kwa kawaida kila kifo hakikosi sababu na kila kifo kina maelezo yake . .mara nyingi tunahoji kidogo tunasikitika kidogo tunashughulika na msiba tunazika na maisha yanaendelea . .!!!!
ITAENDELEA
Kwenye Bible ukisoma na kutafsiri mstari mmoja tuu utapotoka...ukisoma hii mada kwa utulivu utagundua kuwa kuna vifo vya aina nyingi...Kwenye biblia kuna MTU alikufa yesu akamfufua na watu wakaenda kumuuliza yule MTU akajibu yeye alikua hajui chochote ni kama alikua kwenye usingizi usio na ndoto
Hatoweza kuwa huru huyo muuaji...atajificha lakini nafsi itamsutaSanaa ya kifo ni kitu cha ajabu mno ! wazungu kuna usemi maarufu wanapenda kuutumia unasema the night has a story to tell
Mazingira ya kifo cha binti aliyekinyonga bar hayaleti picha ya mtu aliyeamua kutoa uhai wake
Najaribu tu kuwaza kwa sauti
-ujumbe wa madeni na wadeni aliouacha
-ujumbe wa kusema ni uamuzi wake mwenyewe na usihusishwe na yoyote yule
-picha hazionyeshi hari za kifo cha surphocation
Tu assume kama ameuawa
-muuaji aliwaza nini?
-alimrubunije?
-zile dakika za mwisho zilikuwaje?
-yuko wapi kwa sasa?
-anajisikiaje?
View attachment 333588
Na kweli aendelee kabla wavuruga mada hawajaja..Mshana endelea basi na mada.
Na hizo picha unazoweka mwanzoni mwa kila mada ni vyema ungekuwa unazitafsiri coz hazieleweki vizuri