TANU ilipochukua uongozi wa nchi 1961 ilikuwa na "wenye uzoefu wa kufanya kazi serikalini" wangapi? Na iliongoza vizuri sana.
Uzoefu walio nao hawa viongozi wakuu wa CCM ya leo ni wa kuiba sana mali ya nchi na kuficha Uswizi.
Hatutaki wenye uzoefu wa kuongoza serikali inayofanya vibaya. Tunataka kuanza upya, na viongozi wapya.
Sita and the other used leaders in CCM are shameful failures.
Nimeshangazwa na habari kwenye gazetu la mwananchi toleo la leo lenye kichwa cha habari SITTA: TISHIO LA URAISI CHADEMA NI DR SLAA TU.
Ni wazi kuwa mheshimiwa sitta amefilisika kimawazo. Anajua fika kuwa ndani ya CDM kuna watu wenye uzoefu lukuki wa kiuongozi ndo maana hata yeye amekuwa akifanya vikao vya siri na viongozi waandamizi wa CDM ili ikiwezekana 2015 ahamie CDM.
Nimemnukuu akimponda Kamanda Mbowe kuwa ana uzoefu wa kuendesha kumbi za muziki tu si kuongoza serikali. huu kwangu ni uendawazimu mwingine wa mzee Sitta, Kwani anajua fika kuwa chini ya uongozi imara kwa Mh Mbowe CDM kimekuwa chama imara kisichotetereka, kupitia busara, hekima na ubunifu wa Mbowe CDM inawanyima CCM usingizi ndo maana kila kukicha CCM hawachoki kukisema.
Nakumbuka wakati Reginald Mengi alipofiwa na Kaka yake mzee Elitira Mengi, mzee Sitta na wenzake 3 waliomba kukutana na Mbowe pale Aishi Hotel na moja ya mambo walioongea ni sitta na wenzake 3 kuhamia CDM uchaguzi ujao wa 2015 na kuhakikisha CCM inaondoka kabisa madarakani.
Mh Sitta anatakiwa kuelewa kuwa, you only need a single person at the top to make it or break it. Rwanda wamepiga hatua si kwa sababu ya watu '20' au '40' bali ni kwa sababu aliye juu ameweza ku-manage hao 20 au 40.