Samwel Sitta: Wa kuogopwa urais 2015 ni Dr. Slaa tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samwel Sitta: Wa kuogopwa urais 2015 ni Dr. Slaa tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Aug 30, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,526
  Trophy Points: 280
  • ADAI WENGINE NI WAZOEFU WA KUONGOZA KUMBI ZA MUZIKI, ATAMBA CCM KINA ZAIDI YA WATU 20 WENYE SIFA ZA URAIS, ZITTO AMJIBU

  Edwin Mjwahuzi, Karagwe | Mwananchi | Agosti 30, 2012
  [​IMG]
  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akiwa ameshikilia silaha za jadi baada ya kusimikwa kuwa mzee wa kimila wa kabila la Wanyambo, katika hafla iliyofanyika juzi kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera. Picha na Edwin Mjwahuzi

  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM, Samuel Sitta amekiponda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akidai kuwa muda wake wa kutawala nchi bado, kwa kuwa hakina viongozi wa kutosha wa kufanya kazi za Serikali ukimwondoa Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa.

  Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wa Wilaya ya Karagwe, Kagera, alikokuwa katika ziara ya kutembelea ofisi za CCM.

  Alisema kuna upungufu mwingi katika safu ya uongozi wa chama hicho, kutokana na kutokuwa na watu wenye uzoefu wa kufanya kazi za Serikali, badala yake akidai kuwa kina baadhi ya viongozi wenye uzoefu wa kuongoza kumbi za muziki... "Wote hapa mnasikia kwamba Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe ni mjuzi wa disko za usiku, sasa huwezi kulinganisha na CCM hata akitoka mtu mmoja chama chetu hakiwezi kuyumba."

  Dk Slaa na Mbowe hawakupatikana jana kuzungumzia kauli hiyo ya Sitta baada ya taarifa kueleza kuwa Mbowe yuko nje ya nchi na alikuwa hapatikani kupitia simu yake ya mkononi kama ilivyokuwa kwa Dk Slaa.

  Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alipinga kauli hiyo akimtaka Sitta aachane na chama hicho kikuu cha upinzani na atumie muda wake kukijenga chama chake ambacho alidai kuwa kina makundi zaidi ya sita.

  "Mwaka 2005 tuliweka mgombea Mbowe, mwaka 2010 tukamweka Dk Slaa, mwaka 2015 anaweza akarudi Mbowe, Dk Slaa au mwanachama yeyote wa Chadema," alisema Zitto.

  Alisema Chadema ni taasisi na si chama cha makundi kama ilivyo kwa CCM hivyo hakiwezi kumtegemea mtu mmoja... "Sitta asigombane na Chadema, ajenge chama chake ili tukutane mwaka 2015."

  Akizungumza na viongozi hao wa CCM Karagwe, Sitta alisema hakuna kiongozi mwingine anayeweza kufanya kazi ya kukiongoza Chadema na kukifanya chama kikubalike kwa umma.

  "Hawa jamaa hawana hazina ya viongozi kama tulionayo CCM, ambapo tunaweza kusimamisha wagombea 20 wa urais wenye sifa zinazofanana tofauti na wao wanaye Dk Slaa tu ambaye inasemekana aliukimbia upadri."

  Kuhusu CCM
  Akizungumzia chama chake, Sitta aliwataka viongozi wa CCM Mkoa wa Kagera kutokaa kimya na badala yake wajitoe na kujibu hoja za upinzani wanazozitoa kuikosoa Serikali iliyopo madarakani ili ionekane haijafanya mambo ya maendeleo tangu kupatikana kwa uhuru.

  "Serikali ya CCM imefanikiwa katika maeneo mengi ya huduma za jamii kama elimu, barabara, afya na mawasiliano, sasa inashangaza kuona viongozi wa chama mnashindwa kufanya mikutano ya kuwaeleza wananchi mafanikio yanayotokana na utekelezaji wa sera na ilani ya chama chetu."

  Sitta aliwataka viongozi chama hicho nchini kuepuka mapambano na chuki miongoni mwao lakini akasisitiza kwamba kinaendelea na mkakati wake wa kuwaondoa viongozi wanaodaiwa kuwa ni mafisadi maarufu kwa jina la "magamba".

  Alisema chuki na mapambano yanayoendelea ndani ya chama hicho ndiyo yanayochangia kukidhoofisha na kuwapa la kusema wapinzani na hata kusababisha baadhi ya wanachama kukihama.

  "Mapambano ndani ya CCM ndiyo chanzo cha migogoro na mitafaruku inayosababisha viongozi na wanachama wetu kuombeana mambo mabaya na kutoa mwanya kwa watu wetu kuhamia upinzani."

  Sitta yupo katika ziara ya siku tano ya kiserikali mkoani Kagera kukagua miradi mbalimbali inayohusiana na mwingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Amesema kweli ila uckute katumwa na wenye ambition
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  M4C @ Work..!.!!!!
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Muulize yeye mabona alishindwa na mwanamke (sio kuwa nawadharau wanawake hapana hata kidogo) ila kwa anavyojiona yeye, makinda asingelimshinda hata kama alisukiwa zengwe. Mpiganaji mashuhuri hata hilo zengwe angelilishinda. Jizee linazeeka vibaya.
   
 5. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Kitu chema hadi maadui wanakitambua kwa hali tutegemee wengi kusadiki kuwa RAIS ajaye ni Dr Slaa.
   
 6. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimeshangazwa na habari kwenye gazetu la mwananchi toleo la leo lenye kichwa cha habari SITTA: TISHIO LA URAISI CHADEMA NI DR SLAA TU.

  Ni wazi kuwa mheshimiwa sitta amefilisika kimawazo. Anajua fika kuwa ndani ya CDM kuna watu wenye uzoefu lukuki wa kiuongozi ndo maana hata yeye amekuwa akifanya vikao vya siri na viongozi waandamizi wa CDM ili ikiwezekana 2015 ahamie CDM.

  Nimemnukuu akimponda Kamanda Mbowe kuwa ana uzoefu wa kuendesha kumbi za muziki tu si kuongoza serikali. huu kwangu ni uendawazimu mwingine wa mzee Sitta, Kwani anajua fika kuwa chini ya uongozi imara kwa Mh Mbowe CDM kimekuwa chama imara kisichotetereka, kupitia busara, hekima na ubunifu wa Mbowe CDM inawanyima CCM usingizi ndo maana kila kukicha CCM hawachoki kukisema.

  Nakumbuka wakati Reginald Mengi alipofiwa na Kaka yake mzee Elitira Mengi, mzee Sitta na wenzake 3 waliomba kukutana na Mbowe pale Aishi Hotel na moja ya mambo walioongea ni sitta na wenzake 3 kuhamia CDM uchaguzi ujao wa 2015 na kuhakikisha CCM inaondoka kabisa madarakani.
   
 7. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  huyu sitta anaeleweka yupo mguu ndani nje tokea wamnyime uspika.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Yeye mwenye uzoefu wakuendesha bunge mbona alishindwa na Yule bibi kiroboto ambaye hata kusema hawezi yeye anaweza kujilinganisha na Mbowe? Mnafiki mkubwa anazeeka vibaya Ngoja nimuitie Mzee wa mamvi amsulubu
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Wanakosea kama wadhani CDM ni mali ya Mbowe.
   
 10. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninawaomba CHADEMA tusijibu hoja za hawa MAZUMBUKUKU.
  Tuendelee na Harakati zetu za KUJIIMARISHA.
  Hawa Mazumbukuku wanataka tusijenge CHAMA ili tuishie KUJIBIZANA.
  M4C~CHADEMA~VEMA 2015.
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naona mzee sitta akili imesha expire kabisa... Tokea wamkosekose kumuua na kumpokonya uspika, amekuwa kama amechanganyikiwa vile... Anyway ndio magamba hao, wako kama zombis...
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Karushwa ka Richmond kamelevya pia anamtukana jk kwani naye ni mshiriki poa wa muziki wa disco. Kuendesha muziki kunaathiri vp taifa na pia haya matatizo tz yamesababishwa na nani? Kwa Sita unategemea nini zaidi ya kuchumia tumbo lake! Baada ya kuangalia namna ya kutatua kero za wananchi anahangaika na CHADEMA, hivi mijitu inaondoka lini kwenye utawala?
   
 13. mchina mweusi

  mchina mweusi Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye RED, inabidi aanze kumkataza baba mwanaasha kwanza kuende kwenye miduala....au anadhani huwa hatumuoni huku bagamoyo, rais mzima wa nchi anavaa kaptula na kwenda kwenye taarabu

  MY TAKE: SITA AANGALIE ANAZEEKA VIBAYA
   
 14. i

  iseesa JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bi Kiroboto ni zaidi ya Sitta. Ni mmoja wa hao MAGAMBA 20 aliowataja bwana6
   
 15. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anasema wanawamachama wenyesifa zaidi ya 20.wameifanyia nini nchi hii? Najua tanzania hatujapata mtu mwenye sifa za uraisi zaidi ya nyerere .dr.slaa anaonyesha kumkaribia.
   
 16. K

  KVM JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Sita inabidi ajue kuwa tulionao sasa hivi na wengine wengi wa CCM ni viongozi wanaoongoza kwenye wizi. Hawa hawatakiwi kabisa. Tanzania inahitaji viongozi wapya kabisa. Viongozi ambao siyo wezi. Mbona Rwanda wameweza kuongoza nchi wakati wote walikuwa wapya kabisa? Kwa nini Watanzania wasiweze?
   
 17. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  ninavyoijua akili ya binadamu ni kitu ambacho kinafanya kazi kwa graphs nikimaanisha kuwa inaweza kupanda, kuwa constant au hata kushuka chini ya mstari wa sifuri. Huyu bwana kuna kipindi uwezo wake (labda) ulikuwa juu ila sasa unaweza ikawa ndio ile theory maarufu ya 'diminishing return' inafanya kazi katika akili yake!
  Kweli kama anaweza kuamini kuwa katika Tanzania yenye watu karibia/zaidi ya million 60 ina wana CCM 20 na Dr. Wilbroad Slaa hivyo watu 21 tu wenye uwezo kwa kuongoza ni dhairi kuwa 'hatuko naye' tena kifikra!
   
 18. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee babaangu gamba linamwasha dr slaa atamkuna,,

  ngoja nipate kisusio
   
 19. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Dr Slaa ndie rais ajae.tunachotakiwa ni kumlinda kwa nguvu zetu zote kwa hali na mali,usiku na mchana ili hatimae aje kutuondolea umaskini tulionao.
   
 20. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  hahahhahaha!!!!!! Sitta naona kaibukia huko sasa, kazi imeanza, bado membe,lowassa, mwakyembe na januari makamba nao hawajalipuka. M4C inawatesa sana aisee!!!

  Sitta amesahau hapa africa kuna kiongozi (tena ni rais wa nchi sasa hivi) alikuwa DJ na anafanya mapinduzi ya kweli mpaka sasa nchini kwake wananchi wanamkubali sana.
   
Loading...