Samwel Sitta: Msimamo wa Maaskofu hauna nguvu yoyote

Samwel Sitta: Msimamo wa Maaskofu hauna nguvu yoyote

Sitta Ameshalaaniwa Tangu enzi za BMK mkuu....

Hakuna kosa kubwa kama kuwatusi wapakwa mafuta wa mungu.
NB; Ni mzee wa kanisa na mlezi wa kwaya KKKT kanisa moja kinondoni, mtakumbuka alimuomba Rostam msaada kwa kwaya yake
 
Namuunga mkono Sitta,maAskofu nao ni wanadamu kama sisi kwa nini watuamulie,kila mtanzania ana wajibu wa kuisoma Katiba pendekezwa na kuielewa na kutoa maamuzi kutokana na utashi wake,na kupiga kura ya ndiyo au hapana.Hawa maaskofu wastuambie tupige ndiyo au hapana,kila mtu ana maamuzi yake
Unasahau kwamba wazee wote wa CCM wanatuhimiza tupige kura ya ndiyo... Walipoyatamka hayo yote mlikaa kimyaaa.... TENA JUZI WAZIRI WA SHERIA NAYE KATUTAKA TUIPIGIE KURA YA NDIYO ... Hao hamuwaoni kwamba watatuchagulia cha kufanya, lakini maaskofu ndo mnawatazama kwa jicho hilo kwa vile tu wanakwenda tofauti na mnayoyataka.... Kweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha
 
Laana ya maaskofu aliyoipata wakati wa Bunge la Katiba imeanza kufanya kazi. Siku si nyingi atavua nguo huyo.
 
Kama hao MAASKOFU hawana nguvu anawasiwasi gani?Asubiri basi,asije akalia mwishoni.

Ninavyojua BINADAMU ni rahisi sana kumsikiliza kiongozi wake wa DINI kuliko kiongozi wa SIASA.

Angetuachia waumini tuamue kuwasikiliza au lah.Na nimategemeo yangu 90% ya WAKRISTU waliosomewa ujumbe huo watapiga kura ya HAPANA
 
Mwalimu Nyerere hakukosea kumcharaza bakora akiwa chuo kikuu.Bado alikua na -U-primary school katika level ya chuo

Ameacha kushughulikia masuala ya treni la Stesheni - Ubungo anaendeleza malumbano na Maaskofu, ni wiki ya tatu sasa usafiri wa treni hapa Dar haueleweki!
 
Kuna mpuuzi mmoja hapo juu anasema nchi hii waislamu ni 65% na wakristo 35%.vp kuhusu wapagani na tusio dini?pia anadai wakristo wanafki na hawana umoja.vp mbona Shura ya maimamu na BAKWATA wamegawanyika kuhusu Mahakama ya kadhi?huwa mnasoma shule gani nyie?
 
Kila mtu ataweza kushawishi ananyohisikia maaskofu=HAPANA, waislam=NDIYO AU HAPANA Kutegemea hongo ya kadhi, ukawa=HAPANA
.Serikali=NDIYO. Wote wana haki ya kushawishi wala msilaumiane. Tatizo ni mgawanyiko mtakao uacha kati ya raia
 
NB; Ni mzee wa kanisa na mlezi wa kwaya KKKT kanisa moja kinondoni, mtakumbuka alimuomba Rostam msaada kwa kwaya yake

Bado hajafukuzwa kwenye uzee wa Kanisa?

Ni mzee gani wa Kanisa anayemtukana Askofu wake Malasusa?
 
Kama hao MAASKOFU hawana nguvu anawasiwasi gani?Asubiri basi,asije akalia mwishoni.

Ninavyojua BINADAMU ni rahisi sana kumsikiliza kiongozi wake wa DINI kuliko kiongozi wa SIASA.

Angetuachia waumini tuamue kuwasikiliza au lah.Na nimategemeo yangu 90% ya WAKRISTU waliosomewa ujumbe huo watapiga kura ya HAPANA

Ni mkristo punguani tu atakayepiga kura ya Ndiyo baada ya Tamko la Maaskofu
 
Huyu mzee alizeeka yeye pamoja na akili yake tangu bunge maalum la katiba. Sidhani kama bado akili yake inauwaza urais.
 
Sitta anatapatapa na haeleweki. Ameshashindwa hoja na hana ushawishi. Amekuwa na tabia ya kutoa vitisho kwa kila mwenye hoja ambayo ni kinyume na msimamo wake

Na kwa CCM kuendelea kumtumia Sitta kama jembe leo - sioni akifanikiwa! Sitta anafanya kazi ambayo mzee Malecela alikuwa akiifanya (Bulldozer) Siamini kama Samwel Sitta anaweza kupewa cheo cha bulldozer!
 
Ukishakuwa tu kingozi wa CCm basi laana inakuwa automatic,hivi huyu mzee aliyechoka akili na mwili anaingia Kanisa gani kwanza hadi kuzarau viongozi wa Kanisa?Huyu na Pinda wanatakiwa kutengwa kwenye makanisa yao ipo siku nitajitolea kusimamisha kuingia Kanisani kiongozi msema viongozi wa Kanisa vibaya niko tayari kwenda jela kwa hili.
 
Mwalimu Nyerere hakukosea kumcharaza bakora akiwa chuo kikuu.Bado alikua na -U-primary school katika level ya chuo

Japo huwa anajidai eti standard and speed lakini nafikiri huyu jamaa ana mabreki mengi sana katika kichwa chake!
 
Back
Top Bottom