Samwel Sitta: Msimamo wa Maaskofu hauna nguvu yoyote

Samwel Sitta: Msimamo wa Maaskofu hauna nguvu yoyote

Waziri wa Uchukuzi ambaye sasa anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni Samwel Sitta ameshambulia msimama wa Maaskofu nchini kwamba hauna nguvu yeyote

Akiushaumbulia waraka wa Maaskofu kuhusu upigaji wa kura ya maoni kiongozi huyo amesema maaskofu hawana mamlaka ya kuwaamulia watu.

Sitta pia amechekelea kwamba sababu nyingine ya msimamo wao kutokuwa na nguvu ni kwamba Maaskofu wenyewe wamegawanyika vipande vipande kuhusu Kura ya maoni.

Samwel Sitta amekuwa akituhumiwa kwamba wakati wa bunge la Katiba aliwatukana na kuwakashifu maaskofu na Kanisa pale waliposhauri bunge hilo lisitishwe.

Kwani wao wanapowataka wananchi wapige kura ya NDIYO wanayatoa wapi mamlaka ya kuwaamulia wananchi..?
 
anazeeka vibaya,sikutarajia mtu mwenye heshima akajitoa muhanga,wenzie wapo kmya mpaka leo

Sitta hana heshima yoyote kamwe asilani. Ameshazoea kuzomewa mana tuelewe tu kuwa sio yeye bali ni laana iliyo ndani mwake ndiyo ibayomtesa kwasasa..
Si lolote si chochote.
 
Kama chama cha mapinduzi kinafika mahali kinapuuza maaskofu na kuwaona hawana mamlaka yoyte basi sasa ni dhahiri kabisa mauti na mwsho wa mafisadi kuitawala nchi hii


Kamanda nakwambia ya kwamba hawa hawanaga mafisadi kikomo chao kimefika!!!!!
 
Mbona ccm inatapatapa hi yo hivi kweli unaweza kuilinganisha Tanzania na Rwanda? Hivi unalinganishaje kilichotokea Rwanda na nia njema ya maaskofu wa Tanzania kuhusu mustakabali wa taifa.

Huwa ninawashangaa sana viongozi wa ccm kujifunika mwamvuli wa mauji ya Rwanda au baada ya mipango yenu kufail cha mwisho ni kufanya mauaji ya Halaiki kama Rwanda nini?

Haina shida kaka Tupo Tanzania na Tanzania ni yetu. Tuiombee amani!
 
Sawa lakini kumbuka kuna mapadri wanatumikia vifungo pale Rwanda kutokana tu na kauli zao ambazo zilipelekea Rwanda kuingia katika mauaji ya kimbali. Asante mkuu wangu.

Mtu yoyote akivunja sheria huadhibiwa na viongozi wa dini are not immune. Kuwa sehemu ya siasa na kushiriki siasa si kuvunja sheria. What is politics by the way? It's all around us, hata kanisani na misikitini. It's just everywhere.
 
Jamani hivi elimu kuhusu katiba inatolewa wapi au ninaipata vipi??ninapenda nishiriki kura ya maoni baada ya kuielewa.

Swali zuri sana ambalo halitajibiwa. Tunachoambiwa ni kuwa Watanzania wa sasa wana akili (waliopita walikuwa hawana akili) wataamua wenyewe kupiga kura ya ndiyo au hapana. Wataamuaje na kwa kuzingatia nini, hilo hatuelezwi.
 
Mi nadhani maaskofu ni viongozi wa wanachama wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama na itikadi tofauti ni bora wangewashauri wakristo wao waisome katiba inayopendekezwa waielewe na kuipigia kura kwa busara ya NDIO AU HAPANA. vinginevyo itakuwaje katiba hiyo ikipita? Watajionaje au watajisiaje? Na je nini kitatokea ikiwa viongozi wa kiislamu nao watawaambia waumini wao waikubali na kuipigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa?? Viongozi wa dini wasitupeleke kusikofaa..


Kiongozi wa dini kuwashawishi watu wasome kitu haramu kilichopishwa kwa kura haramu ni kosa kubwa sana hata kwa huyo Mungu/Allah wanaemuabudu kila siku katika nyumba za ibada.Sio sahihi kabisa kushiri kuhalalisha 'haramu'haifai na haipendezi na haitakiwi.

Sitta sio muadilifu hasa alipokiuka sheria ya mabadiliko ya katiba kwa kujitungia katiba yake na chama chake cha ccm kwa kuanza kupokea upya maoni na kutaingiza katika katiba hiyo.

Kama ambavyo alivyowataka viongozi wa dini kuwa hawana mamlaka ya kuwaanulia wananchi na yeye huyo huyo atueleze alipata wapi mamlaka ya kuwaanulia wananchi pale alipotupilia mbali maoni ya wananchi na kupachika ya kwake kwa faida ya chama chake?
 
Kwani wao wanapowataka wananchi wapige kura ya NDIYO wanayatoa wapi mamlaka ya kuwaamulia wananchi..?
Swali gumu sana kwao. Wamejiaminisha kwamba wao wana exclusive rights kwenye maisha ya mtanzania.
 
Ndiye kiongozi pekee kwenye serikali ya Kikwete kutandikwa bakora ktk utu uzima wake kwasababu ya mambo yake ya kipuuzi puuzi,Nyerere alikuwa sahihi kumramba bakora huyu mhuni asiyekuwa na sifa hata moja ya kiuongozi.Kwasababu yeye anadharaulika na kila mtu na pengine hata familia yake mwenyewe haimheshimu basi anafikiri na wengine hawaheshimiwi kama yeye?

Tusipotoshe ukweli mdogo wa kihistoria. Aliyechapwa viboko kwa agizo la Mwalimu ni marehemu Wilfred Mwabulambona wala sio Mhe. Sitta.
 
Hata Nebukadneza alianza vivyo hivyo. Hali kadhalika manase naye.
 
Swali zuri sana ambalo halitajibiwa. Tunachoambiwa ni kuwa Watanzania wa sasa wana akili (waliopita walikuwa hawana akili) wataamua wenyewe kupiga kura ya ndiyo au hapana. Wataamuaje na kwa kuzingatia nini, hilo hatuelezwi.

Naaam.... kauli yako ni SWADAKTA...nimekuelewa na sasa itabidi tuoneshe ujuzi wetu wa ku draw a square circle.
 
Ndiye kiongozi pekee kwenye serikali ya Kikwete kutandikwa bakora ktk utu uzima wake kwasababu ya mambo yake ya kipuuzi puuzi,Nyerere alikuwa sahihi kumramba bakora huyu mhuni asiyekuwa na sifa hata moja ya kiuongozi.Kwasababu yeye anadharaulika na kila mtu na pengine hata familia yake mwenyewe haimheshimu basi anafikiri na wengine hawaheshimiwi kama yeye?

lakini si nyinyi ambao mlikuwa mnamsifu kuwa alikuwa spika bora wa bunge?? kipindi kile kila mtu sita sita sita, au mmesahau hata hapa JF kila mtu alikuwa anampigia chapuo awe spika wa bunge la katiba?? nakumbuka prof kitila mkumbo aliposema ni makosa kumuunga mkono mgombea wa ccm wengi walimpinga kwa sababu eti wanamuamini sita
 
Say what again? Hauna nguvu!!

Hahahaaa acheni wajidanganye....hakuna mtu mwenye nguvu ya kiushawishi kama kiongozi wa kiimani.....safari hii hata kanisa limeona uozo na kuamua kutoa semina maalumu kwa jambo hili.
 
Nalo tamko la serikali la kuwataka Wananchi wapige kura ya Ndiyo halina maana PIA kwa sababu inawadharau Wananchi kuwa hawawezi kutumia utashi wao kuamua!
 
hii laana ya kuwadharau watu wa Mungu itamtafuna huyu mzee mpaka kaburini .
 
Back
Top Bottom