Waziri wa Uchukuzi ambaye sasa anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni Samwel Sitta ameshambulia msimama wa Maaskofu nchini kwamba hauna nguvu yeyote
Akiushaumbulia waraka wa Maaskofu kuhusu upigaji wa kura ya maoni kiongozi huyo amesema maaskofu hawana mamlaka ya kuwaamulia watu.
Sitta pia amechekelea kwamba sababu nyingine ya msimamo wao kutokuwa na nguvu ni kwamba Maaskofu wenyewe wamegawanyika vipande vipande kuhusu Kura ya maoni.
Samwel Sitta amekuwa akituhumiwa kwamba wakati wa bunge la Katiba aliwatukana na kuwakashifu maaskofu na Kanisa pale waliposhauri bunge hilo lisitishwe.
Mi nadhani maaskofu ni viongozi wa wanachama wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama na itikadi tofauti ni bora wangewashauri wakristo wao waisome katiba inayopendekezwa waielewe na kuipigia kura kwa busara ya NDIO AU HAPANA. vinginevyo itakuwaje katiba hiyo ikipita? Watajionaje au watajisiaje? Na je nini kitatokea ikiwa viongozi wa kiislamu nao watawaambia waumini wao waikubali na kuipigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa?? Viongozi wa dini wasitupeleke kusikofaa..
Sijakusoma hasa hoja yako ni nini
DINI itusaidie sio tu kumpendeza ALLAH na kwenda peponi lakini pia TUISHI kwa upendo na amani na watu wote kadiri ya Mtume (SAW)
Tusikuze na kupanda chuki pasipo sanabu
Matusi yote haya ya Samwel Sitta wakiristo bado wanakata mbuno kuwa na umoja kuikataa katiba lakini silaumu ukiristo ulivyo unafiki unafiki na hofu
Viongozi wa dini wana maslahi. Hivyo, ni sehemu ya siasa katika ngazi zote. Wame influence na wao kuwa influenced na siasa kwa karne nyingi sasa. Katika baadhi ya nchi, viongozi wa kidini walikuwa ndio vuongozi wa serikali. Yaani dini ilikuwa ni sawa na serikali. Ni makosa makubwa kufikiri viongozi wa dini ni neutral. Analysis yoyote inayo assume viongozi wa kidini ni neutral is flawed. And nobody is neutral anyway. That's a myth. Just look around and you will quickly agree with me.
Nachomsifu samwel Sitta
Kawaambia ukweli
Mimi n mkiristu lakini siungi tamko lao
Huyu ni failure mkubwa hata ubunge hawezi kushinda tena.Sitta ajue kuwa hata kushindwa kwake kisiasa ni laana ya wakristo
Sawa lakini kumbuka kuna mapadri wanatumikia vifungo pale Rwanda kutokana tu na kauli zao ambazo zilipelekea Rwanda kuingia katika mauaji ya kimbali. Asante mkuu wangu.
Dada matamko haya ya ndugu zetu hayajaanza leo,2005 walitowa waraka.na sisi tukatoa waraka matokeo yake chuki za kidini zikakua,na kuna walio piga kura kwa SLAA na JK kwa miongozo hiyo ya MISIKITINI na MAKANISANI.sasa tunakokwenda hatuta angalia sera tutawasikiliza viongozi wetu wa dini.ninachoogopa mimi kuna baadhi ya wenzetu wenye misimamo mikali wanaamini hamna watakachopoteza,wakichoka na matamko haya ya sio na tija vurugu itatokea,na visasi.undugu wetu utavurugika,tutaikimbia nchi yetu mzuri.Tuna akili tuaamua wenyewe HAPANA au NDIO,Watanzaniawa leo sio mafala wanaelewa nini mahitaji yao.
Huyu Mzee sitta hajiheshimu hata kidogo. Wakati wa tafrani wanasiasa hujikomba kwa viongozi wa dini kuwa wana watu wawasaidie kushawishi jamii iache maovu. Leo wanapotoa ushauri wao unaopingana na serikali sasa wanakashifiwa.
Kisa ni kutetea kupitisha katiba ya mpito ambayo itafumuliwa tu baada ya kupitishwa kutokana na dosari kibao.