Najua Samweli Sita unajua ushauri mzuri na mbaya, Huyu aliyekushauri vizuri kwa haya ninani?
- Aliyekushauri kuzima maoni ya wananchi katika katiba mpya ukaweka ya chama tawala CCM.
- Aliyekushauri kupuuza wito wa kusitisha vikao vya bunge la katiba hata baada ya wajumbe wengi kulisusia hususan UKAWA
- Aliyekushauri kubuni mbinu ya marehemu kuipigia kura ya kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
- Aliyekushauri kuzuga watanzania kuwa mahujaji waliokuwa wakimrushia shetani mawe waliipigia kura ya ndiyo ya katiba ya Chenge kuwa katiba pendekezwa.
- Aliyekushauri kuchakachua kura za waliopiga kura za siri za hapana kwa katiba ya Chenge zikageuka kuwa za ndiyo baada ya kuahirisha bunge kuwa zitahesabiwa kesho yake wakati muda wa kuzihesabu ulikuwepo.
- Aliyekushauri kuaminisha wananchi kuwa wabunge wa bunge la katiba wamekubaliana kwa asilimia kubwa kuipitisha katiba ya Chenge kuwa katiba Pendekezwa.
- Aliyekushauri ukiwa waziri wa Uchukuzi kumuhonga Tulia Ackson ujumbe wa bodi ya bandari baada ya kubuni kanununi za kuvuruga bunge la katiba.
- Aliye ushauri kuwa kwa kazi mbovu uliyoifanya katika bunge la katiba sasa ungefaa kuwa rais wa Tanzania.
- Aliyekushauri kuwa, baada ya kukatwa katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi wa Tanzania sasa urudu kugombea uspika huku ukijua kuwa tayari wananchi waliishakerwa na uhuni wako na utapeli wa kisiasa.
Kama uliona ushauri wooote huo ni mzuri, bila shaka utawaona washauri wabaya wanaomshauri Rais Mheshimiwa, Dr. Magufuli
Surgeon wa Majipu kutumbua majipu ya TRA, TPA, RELI, N.K.
Kwanza nimekumbuka kuwa nawewe SITA ni mkusanyiko wa majipu. Hebu angalia,
- Pesa ya posho zizosusiwa na wajumbe wa UKAWA katika Bunge la Katiba ulizipeleka wapi?
- Ikiwa waziri mwenye dhamana, Ukiukwaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati ya standard gauge ulifanyika ukiwa wapi?
- Haraka ya kuingia mkataba huo kabla ya awamu ya nne kuisha na wewe kutema uwazili ilikuwa ya nini?
- Hilo jengo la ofisi ya spika ulilojenga Urambo Ndungai atalitumia je?
- Ukiwa spika 2005 hadi 2010 Kwanini ulizima hoja ya Richmond na kuifufua mwaka 2015 ulipoona Lowasa anagombea urais kupitia UKAWA?
- Ukiwa mkuu wa kitengo cha uwekezaji, we sindo uliileta Richmond? Hukujua kuwa ni kampuni ya mfukoni?
- We sindiye ulichapwa na Nyerere viboko kwa utovu wa nidhamu, ulitaka tuwe na rais mwenyesifa ya migomo?
- Nikiwa Mwana CCM MFU, Nashauri Rais wangu, Dr, (surgeon wa majipu) John Joseph Pombe Mgufuli mwana NGOSHA, apasue majipu ya Samweli Sita kwa SHOKA na Chain Saw, maana ni makubwa saaana kama mbuyu na magumu kama mpingo na yana harufu mbaya kama nanilii, nanilii, na, na ahhh, basi Bwana!