Samwel Sitta Live on Mlimani TV

Kwamba falsafa ya chama sasa sio tena kutumikia watu ni kujitajirisha na kwamba vikao vya chama Magamba huwa vinanunuliwa loh hii ni hatari ina maana kama NEC Ya Magamba unakuta tayari imepigwa bei!!!
Kwa kuendelea kwake kuwepo CCM ina maana moja tu ya kwamba anakubaliana na falsa hiyo vinginevyo angekwisha ondoka kwakuwa hakubaliani na Falsasa ya viongozi kutumikia utajiri badala ya wananchi. Na kama anazungumza kwamba hayo yanamchukiza na bado anaendelea kuwapo humo basi jamaa si Mnafiki tu bali ni BAZAZI pia.
 
Mbona yupo kwenye list
Muulize vyema nape atakuwa anajua zamu yake ni lini
Maana Mwandosya na Mwakyembe tayari

Nadhani akiendelea na huu utaratibu wake wa kuisemea hovyo CCM/Serikali basi si ajabu zikaandaliwa namna za kumkolimba huyu Mzee.
 
Hapa alikuwa kwenye maandamano Mbeya
 

Attachments

  • PICT2077.JPG
    658.1 KB · Views: 63
  • PICT2081.JPG
    634.5 KB · Views: 46
Alisema wananchi wanaichukia sisiyem kwa sababu ahadi hazitekelezwi sasa atafanya nn ili kuzifanya zitekelezwe kwa wakati? Akishindwa inamaana anawaambia watz wasiichague tena milele na milele
 
Nadhani akiendelea na huu utaratibu wake wa kuisemea hovyo CCM/Serikali basi si ajabu zikaandaliwa namna za kumkolimba huyu Mzee.
BAK,niliwafagilia mwanzo na kina Mama Killango,Mwakyembe nk.Hata hivyo waliniangusha sana kwasababu inaonekana kama wanapigania maslahi yao binafsi ya kisiasa zaidi ya maslahi ya Taifa.

Nasema hivyo kwasababu style ya upiganaji wanayoitumia siyo that decisive,mainly because ni kama wako mguu ndani mguu nje,which strategically can cost them dearly.

Sasa ndiyo maana vitendo vyao hivi navifananisha na kujaribu kukata tawi ulolikalia wewe mwenyewe.Wako ndani ya system,halafu bado wanadai wako against it.Wanasema mafisadi ndiyo wanapewa nafasi zaidi nyakati hizi.However mafisadi hao pia si ndiyo wanasiasa anaoshirikiana nao kila siku ndani na nje ya chama?Na si bado wanapeana madaraka?

Sasa hapo ndipo penye shida.Hakuna mwanasiasa anaye side na wananchi all the way.Na sina maana ya wananchi wachache wanaoichagua ccm every now and then,nazungumzia umma wa watanzania masikini wasio na mtetezi na wasiojuwa haki zao,wajinga na wenye uelewa mdogo.Hao wako wengi na wanatake a big portion of the country's population.Kwa ujumla ukiyapigania maslahi ya Taifa basi ina maana unawapigania hao pamoja na vizazi vijavyo.
 

Unataka kumaanisha hata Nyerere na Sokoine nao walikuwa wanafiki?Maana hata wao walikuwa wanapinga UOZA lakini wakiwa ndani ya CCM!Tukue kifikra jamani.
 
Hivi huyo mzee hajui kwamba sasa watanzania tunadaiwa bilioni 111 kwasababu ya siasa zake za kinafiki. Hasituongezee machungu,alipokua na uwezo wa kulisaidia taifa,alichagua kulinda chama chake kilichojaa wala rushwa. Analalamika nini sasa? Mnafiki mkubwa sana.
 
Huyu mzee kama kweli hakubaliani na mambo yanavyokwenda ajiuzulu uwaziri na kuwa mbunge wa kawaida hapo tutamsikiliza lakini sasa tunaona ni machungu tu ya kuukosa uspika na baadae akatuma ujumbe eti basi apozwe na uwaziri mkuu akatupiwa uwaziri na wengi walidhani atakataa lakini akaukubali.

Kwa kelele hizi ajue wazi hana chake CCM na uwaziri aliokuwa nao ndio ukomo wa atakachopata na asisahau alikoswakoswa kunyang'anywa uanachama muda flani.Kwa sasa ana options mbili tu,

1. Ajiuzulu uwaziri na akiwa mbunge wa kawaida hatabanwa na kuwa na uwezo wa kusema chochote.

2. Ajiuzulu uwaziri na ubunge na kuhamia upinzani.
 
Unataka kumaanisha hata Nyerere na Sokoine nao walikuwa wanafiki?Maana hata wao walikuwa wanapinga UOZA lakini wakiwa ndani ya CCM!Tukue kifikra jamani.

hawa uliowataja walikuwa wanashauri wakiwa nje ya uongozi lakini Sita yupo ndani na anaweza kushauri ndani kwann asifanye hivyo wakati nafasi yake inamruhusu ndio maana tunasema kama ushauri wake hausikilizwi hana budi ujiuzulu uwaziri kwa sababu huwezi fanya kazi na serikali ambayo inatenda mambo ambayo hayatendi haki na wewe haukubali haki isitendeke.
 
huyo ni mwanasiasa unataka mwanasiasa akwambie 1+1=2 haitowezekana hata siku moja.wanasiasa wote ni wanafiki, tofauti ni kati yao kuna wenye tamaa zaidi ya wenzao, wenye maamuzi kidogo kupita wenzao, wenye ari na uwezo wa kazi wanazopata kuliko wenzao, na wengine ni wazalendo zaidi kuliko wenzao.lakini wote ni wamoja
 
huyo ni mwanasiasa unataka mwanasiasa akwambie 1+1=2 haitowezekana hata siku moja.wanasiasa wote ni wanafiki, tofauti ni kati yao kuna wenye tamaa zaidi ya wenzao, wenye maamuzi kidogo kupita wenzao, wenye ari na uwezo wa kazi wanazopata kuliko wenzao, na wengine ni wazalendo zaidi kuliko wenzao.lakini wote ni wamoja
 
Unataka kumaanisha hata Nyerere na Sokoine nao walikuwa wanafiki?Maana hata wao walikuwa wanapinga UOZA lakini wakiwa ndani ya CCM!Tukue kifikra jamani.
Wewe sasa unachanganya CCM ya Nyerere na hili Pango la Mafisadi. CCM ya Nyerere na Sokoine ilikuwa ni ya Wakulima na Wafanyakazi. Nenda kaangalie hii ya sasa katika uongozi kuna Wakulima wangapi na wafanyakazi wa kawaida wangapi ambao wangeweza kutoa rushwa ili kupita kwenye mchujo wa kugombea uongozi. Ukianzia Ubunge, UWT, Wazazi, UVCCM, Urais, n.k. Kuifananisha CCM ya Mwalimu na hii ya Kikwete ni sawa na kufananisha Afya na Kifo. Tunachomshangaa Sita ni kujifanya kwamba haoni kwamba ndani ya CCM ya sasa hataweza kubadili chochote. Kama anabisha amuulize Kolimba na kama anaona itakuwa ngumu angoje asubiri yamkute ya Mwakyembe na Mwandosya. Utakuja kuwa shahidi wewe mwenyewe hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…