Samsungs wanashida gani?

Mi na mdogo wangu tuko kwenye tasinia inayohusiana na simu zaidi ya miaka 7, hakuna tusichokijua kuhusu simu ndani na nje.

usinheshindwa kujua sababu ya hilo mkuu.

samsung ni baba wa android sio kimakosa,hakuna anachofanya kwa bahati mbaya.
 
Unalalamika Toyota Lexus inakula sana mafuta?
We tafuta Toyota Virtz, IST utakaa sana na mafuta

Vivyo hivo kwa smartphone
Unalalamika Samsung flagship hazikai na chaji tafuta za chini huko zinakaa na chaji kama akina Oppo nk

Kinachokula sana moto ni technology iliotumika kutengeneza simu
Inavyokua kubwa ndio na ulaji chaji unakua mkubwa pia
 
Changamoto kubwa hapo ninayoiona ni watu kununua samsung refurb na kusingizia ubora wa simu haswa hizi samsung flagship, note na s series
Mfano huu mwaka 2022 mtu anaenda makumbusho kununua samsung s7 mpya au note 8 unategemea nini kama sio kuja kumwaga lawama hapa kumbe umeshauziwa refurb
Mtu yoyote anayetumia genuine samsung flagship atakuwa shahidi wa ubora wa hizo simu kimatumizi na hata battery

NB: Kama unataka samsung flagship kwa sasa (2022) zipo available s20,s21 na s21 ultra ama note 20 na note 20 ultra ukienda kununua chini ya hizo kwa wakati huu usije hapa kulialia ni bora utafute midrange zipo nyingi tu at affordable cost
 
Nunua Plus version ya hizo simu na uache kulialia.
 
Mjadala ilibidi uishie hapa.
 
Samsung hawana shida.
Shida ipo kwako kuacha simu zinazokaa na chaji kukimbilia Sumsung kwa ajili ya kuwa classy...
Hahaaaaa
 
Tumia A series zinakaa na charge
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…