Samsung Galaxy Gear - Mwanzo wa Mapinduzi ya Saa

Samsung Galaxy Gear - Mwanzo wa Mapinduzi ya Saa

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

Samsung wameitangualia Apple kutoa saa ya mkononi, ni wazi kuwa 2013 ni mwaka wa gajeti za kuvaa (wearable tech), wakati iWatch imebaki kuwa ni mnon’gono Samsung wameshusha Galaxy Gear, saa ambayo imetoka na apps 70. Ni saa ya kwanza maarufu Duniani ambayo ina kamera. Hii si saa ya kwanza ya kiteknolojia ukizingatia uwepo wa saa ya Pebble, Nike Fuelband na Sony SmartWatch 2, lakini hatuna shaka kuwa Galaxy gear itabadili mwelekeo wa kampuni mbali mbali zinazotengeneza saa kwa sasa.

Ubora:

  • Ina apps 70, ikiwemo pedometa
  • Kamera ni kivutio kikubwa cha saa hii
  • Chaji inayodumu masaa 24
  • Kioo ni aina ya Amoled yenye skrini mguso
Kasoro:

  • £ 300 (TSh.782,600) ni ghali mno
  • Inarekodi Video ya Sekunde 10 tu
  • Memory bado ni ndogo (4GB)
  • Infanya kazi na Note 3 na tablet ya Note 10.1 (toleo la 2013) tu kwa sasa
  • Haina NFC
Apps mbali mbali ambazo ni muhimu ndio kivutio kikubwa cha saa hii; apps hizo ni kama vile S Voice ambapo unaweza kuipa amri mbali mbali za maneno na saa hii na ikatekeleza, S Voice hufanya kazi sawa na namna inavyotumika kwenye simu. Kamera pia ni kivutiko kikubwa katika saa hii, ingawa pixel ni chahce mno (1.9 MP) kasoro kubwa ya kamera hii inarekodi video za sekunde 10 tu na si zaidi ya hapo. Bila shaka Samsung wameweka hili ili kuzuia saa hi kujaa haraka disk ya ndani ambayo ina 4GB tu.

Hata hivyo saa hii ina mengi mazuri Smart Relay ni moja kati ya jambo zuri la saa hii, Smart Relay humuweza mtumiaji kuendeleza analolifanya kwenye saa hii kwenye simu, yaani unapotoa simu baada ya kuanza kusoma meseji, simu huwa moja kwa moja inafungua meseji unayoisoma, hivyo huna haja ya kufungua app ya meseji kwenye simu.

Kibwagizo kikubwa katika saa hii ni ule uwezo wa kupokea simu na kuongea kwa saa, yaani simu inapoingia unaweza kuiwacha mfukoni na ukapokea na kuanza kuongea kwa saa, unachotakiwa kufanya ni kunyanyua mkono na kuuweka kwenye sikio tu. Kwa maana hiyo basi saa hii ina microfone na spika. Saa hii pia humuwezesha mtumiaji kucheza muziki ulioko kwenye simu yake.

Saa hii kwa upande wa kimaumbile ni kivutio kwa vile sio tu utaweza kujua saa ngapi lakini pia unaweza kubadili muonekano wa saa ya kwa mitindo na rangi mbali mbali, pia unweza kujua hali ya hewa ya mahala ulipo. Ili kubadili sura au muonekano wa saa hivyo inakubidi kutumia ama simu (galaxy Note 3) au tableti (Galaxy Note 10.1 Toleo na 2013). Samsung wameahidi kuwa saa hii baadae itafanya kazi na simu bali mbali za kampuni hiyo kama vile Note II, S3 na S4 mara baada ya simu hizo kufanyiwa auboreshaji wa software (Android 4.3 Jelly bean)

Wafanya mazoezi watafurahishwa sana na pedometa ya Galaxy Gear; pedometa hiyo ambayo inatumia sensa za Gyroscope na akselerometa hivyo pedometa hiyo hutoa taarifa kama vile umbali uliokimibia na kalori ulizounguza katika mazoezi, taarifa hizi zinaweza kuhamishwa kwenye simu au tableti na kuhifadhiwa, Galaxy Gear huunganishwa na simu au tableti kwa teknolojia ya bluetooth. App nyingine ya wana mazoezi katika saa hii ni my fitness pal.

Galaxy Gear pia ina voice memo ambapo mtumiaji huweza kurekodi mazungumzo yanayoendelea kwa urahisi sana, au kutumia voice memo mabadala ya memo za maandishi. Saa hii pia ina muonekano mzuri, imetoka ikiwa na rangi sita mbali mbali ikiwemo nyeusi, nyeupe na manjano.

Kinacho vunja moyo zaidi katika saa hii ya aina yake ni bei, nchini Uingereza Samsung Galaxy Gear inauzwa £300.00 ambazo ni sawa na TSh. 782,600. Ili kupata picha halisi toleo jipya la Saa ya Sony yaani Sony Smartwatch 2 inauzwa nusu ya bei ya Galaxy Gear yaani £150.00, ila ni matarajio ya wadau wengi katika fani ya teknolojia na mauzo yake kuwa saa hii itapata mauzo mazuri mno.

Source: gajetek habari
​

​
 
Asante mkuu kwa kutuletea hapa kwa lugha yetu pendwa kabisa
 
dah mnawasahau kina peble walikua na smartwatch zamani pale mwc niliwacheki.

pebble ndo alioanzisha haya mapinduzi na saa yake ipo compatible na ios na android as long as zina bluetooth.

wakati galaxy gear haiwezi hata kutuma email huku peble zamani tu wanatuma txt na email

hizi ni baadhi ya feature za pebble
1. waterproof
2. unaicontrol kwa sauti
3. ina apps na games
4.inakaa na charge siku 5 hadi 7
5.inasomeka juani
6. unachange mikanda
7. ina themes zaidi ya 100
8. ina alarm na vibration
9.inatoa notification
10. ina backlight kutumia usiku

nafkiri pebble ndo anatakiwa apewe heshima ya kuwa wa kwanza kuanzisha mapinduzi ya saa na sio samsung

photo-main.jpg
 
Always You Do The Best Millah I Apreciate You Work...Thanks For Nice News
 
Last edited by a moderator:
Always You Do The Best Millah I Apreciate You Work...Thanks For Nice News
 
Last edited by a moderator:
its ugly looking for me afterall kama tayari nina simu y would i want a watch with a camera.... kama nina iyo pesa ya kununua hii saa kwa nini nisinunue s3 tu ambayo ntapata vitu kibao??
 
its ugly looking for me afterall kama tayari nina simu y would i want a watch with a camera.... kama nina iyo pesa ya kununua hii saa kwa nini nisinunue s3 tu ambayo ntapata vitu kibao??
bona una haki ya kuwaza hivi, kuna wengi wanaona kama watu naonana nao kwa nini nihitaji simu! Ni uamuzi tu ni kipi unakihitaji katika maisha yako.
 
Last edited by a moderator:
dah mnawasahau kina peble walikua na smartwatch zamani pale mwc niliwacheki.

pebble ndo alioanzisha haya mapinduzi na saa yake ipo compatible na ios na android as long as zina bluetooth.

wakati galaxy gear haiwezi hata kutuma email huku peble zamani tu wanatuma txt na email

hizi ni baadhi ya feature za pebble
1. waterproof
2. unaicontrol kwa sauti
3. ina apps na games
4.inakaa na charge siku 5 hadi 7
5.inasomeka juani
6. unachange mikanda
7. ina themes zaidi ya 100
8. ina alarm na vibration
9.inatoa notification
10. ina backlight kutumia usiku

nafkiri pebble ndo anatakiwa apewe heshima ya kuwa wa kwanza kuanzisha mapinduzi ya saa na sio samsung

photo-main.jpg

Ndo apo mkuu. Mi ninaijua kampuni moja ya italy wana smartwatch, inaitwa i'm watch, kabla ya Apple na samsung kuwa na idea ya smartwatch, tena kabla ya rumours hawa jamaa walikuwa washatoa yao tena iko vizuri sana tu! Samsung apo hajaketa mapinduzi bado! Naskia kazi yake kucheat tu katika benchmark
 
dah mnawasahau kina peble walikua na smartwatch zamani pale mwc niliwacheki.

pebble ndo alioanzisha haya mapinduzi na saa yake ipo compatible na ios na android as long as zina bluetooth.

wakati galaxy gear haiwezi hata kutuma email huku peble zamani tu wanatuma txt na email

Pebble nimeitaja kwenye makala inaelekea hukusoma sawa sawa, tunachozungumza ambacho ungeweza kuelewa kama ungesoma bila ya pupa ni kuwa Samsung ni big brand katika smartphone (No 1 in marekt share kwa sasa) hivyo kampuni kama Samsung kutoa kitu kama hichi athari yake ni kubwa katika soko kuliko Pebble ambaye ilikuwa ni kickstarters project iliyokuwa funded kwa crowdsourcing, iliingia sokoni ikiwa bugs watu wakaanza kuzirudisha. Pia kuna Nikefuel Band ambao baada ya kutoa second generation nao wamekwama.

Angalia Pebble walivyo "watoto" Sony walitoa smart watch muda mrefu baada ya Pebble sasa hivi wanatoa Smart watch 2, Pebble bado wameganda pale pale.
 
unachoongea wewe ni kumtenga masikini kisa tajiri katoa kitu kama cha masikini bila kuangalia anachokupa tajiri in terms of features.

samsung kaleta saa ambayo hata function ya email haina wakati pebble ana hicho kitu long time ago tena kizuri kuliko samsung still tumuite samsung kafanya revolution

pebble saa yake ipo compatible na android 2.3 pamoja na ios wakati gear ni note3 na s4 inafata simu kama s2 na grand wasahau kupata suport ya hii saa, je kama samsung mwenyewe anazitenga simu zake bado unataka tuite mapinduzi wakati ipo saa inayosuport android zote bila kujali huyu tecno au huyu sony.

saa inakaa na chaj masaa 25 ina maana kila siku uchaji kweli haya ni mapinduzi bwana millah? wakati pebble inakaa na chaji siku 7 unachaj kila wiki

galaxy gear hata mikanda huwezi badili ukiniuliza mimi galaxy gear ni simu ilioletwa umbo dogo ikaekwa camera na touch screen ila imefeli tayari na ndio maana samsung wanaandaa saa nyengine kuja kuireplace na sio mapinduz ya saa
 
kula like..

Millah acha kuropoka
 
Kwa maongezi yenu bila kwenda source zao, pebble wako juu!! Over, Samsung ni copy na paste, halafu items zao nyiingi hazikai na charge, sijui wana shida gani na material ya battery hasa kwa hizi smartphones na hizo saa!!!???
 
unachoongea wewe ni kumtenga masikini kisa tajiri katoa kitu kama cha masikini bila kuangalia anachokupa tajiri in terms of features.

samsung kaleta saa ambayo hata function ya email haina wakati pebble ana hicho kitu long time ago tena kizuri kuliko samsung still tumuite samsung kafanya revolution

pebble saa yake ipo compatible na android 2.3 pamoja na ios wakati gear ni note3 na s4 inafata simu kama s2 na grand wasahau kupata suport ya hii saa, je kama samsung mwenyewe anazitenga simu zake bado unataka tuite mapinduzi wakati ipo saa inayosuport android zote bila kujali huyu tecno au huyu sony.

saa inakaa na chaj masaa 25 ina maana kila siku uchaji kweli haya ni mapinduzi bwana millah? wakati pebble inakaa na chaji siku 7 unachaj kila wiki

galaxy gear hata mikanda huwezi badili ukiniuliza mimi galaxy gear ni simu ilioletwa umbo dogo ikaekwa camera na touch screen ila imefeli tayari na ndio maana samsung wanaandaa saa nyengine kuja kuireplace na sio mapinduz ya saa

Nini kipimo chako cha kuonyesha Samsung imefeli? Kusema imefeli tayari ni utashi wako kwa vile Samsung kuandaa saa nyingine sio jambo geni (ikiwa uchachosema ni sahihi, kwa vile hakuna taarifa rasmi kutoka Samsung kuwa wanaandaa Saa nyingine), hivi Samsung kutoa Note III maana yake S 4 imefeli?

Ninachozungumzia mimi sio ile ufahamu wako wa tajiri na masikini, lakini uhalisi wa uwezo katika kuwa na market share. NINAKUHAKIKISHIA muda mchache tu Samsung Galaxy Gear itaipita Pebble kwa mauzo. Mpaka sasa mwaka mzima au zaidi Pebble wameuza saa 250,000 kwa mujibu wa mtandao wao, sasa huoni kama hawa ni watoto tu wanacheza sokoni? Samsung watapitisha idadi hiyo kwa wiki tu.

Ngoja ni highlight udhaifu wa Pebble:

1. Poor marketing, Pebble ukiondoa wachache ambao ni tech geeks kama wewe, wengi bado hawajui hata kama hiyo saa ipo. Samsung Galaxy Gear ilipotoka tu ilikuwa Buzz word, na imetambuliwa na wengi kama inakuja kabla hata haijatoka.

2. Mpaka leo hakuna hata duka moja katika nchi kama UK ambalo linauza Pebble (Lazima ununue kutoka kwenye Website yao iliyopo Marekani) Samsung Galaxy Gear tayari iko kwenye maduka yote ya Carphonewarehouse nchi nzima, na sio tu iko madukani UK bali nchi kadhaa Ulimwenguni.

3. Pebble ilitoka na tatizo ambalo liliipoteze hadhi mapema, ilikuwa ukiizima au ikizimaka ndio adios haiwaki tena. Imewachukua zaidi ya mwezi kutatua tatizo hilo, na wengi walirudisha saa hiyo. Samsung haina mashaka kama hayo.

4. Imezungumzia kwamba Pebble ina email, hebu niambie practically ni vipi unatuma au kusoma email kwenye screen yenye ukubwa wa 1.26"? Kuna feature ambazo ukifikiri kidogo tu unajua kuwa ni useless.

5. Pebble huwezi kutumia kupokea simu ukazungumza kwa kutumia saa, Gear inafanya hivyo.

The list can be so long, lakini kuhusu apps labda nikuulize wewe: Unadhani developers watavutiwa na Pebble watch inayoumia Pebble OS au Galaxy Gear inayotumia Android?

Usifananishe simba na paka, japokuwa wote ni jamii moja.
 
millah mada yako inasema mapinduzi ya saa na mimi nikapinga nikasema samsung hajafanya mapinduzi ya saa sababu tayari watu walishatoa smartwatch kabla yake na nkatoa mfano wa peble na chilubi akatoa wake.
1. mauzo yanahusiana nini na ubora wa kimapinduzi?
2. supply kuwa kubwa inahusiana nini na mapinduzi ya ubora?
3. kupiga na kupokea simu hayo ni mapinduz ya simu na sio saa

tatizo we unaleta ufanboy na kuukimbia ukwel

mapinduzi yanafanywa na watu wa mwanzo tu wanaofatia sio mapinduzi tena bali ni watu ambao wamekua influenced na yale mapinduzi,

wanaofatia watahesabiwa wamefanya mapinduzi pale tu watakapoleta kitu kipya ambacho wanamapinduzi wa mwanzo hawakuweza kukifanya
 
Je Wachina hawana interest na ku-clone hizi, wafanye hivyo ili tuzinunue kwenye mzani buku!
 
Je Wachina hawana interest na ku-clone hizi, wafanye hivyo ili tuzinunue kwenye mzani buku!

mbona washaclone zamani tu sema bei sio rahisi sana ni around dola 50 ( shilingi elfu 80)

touch-screen-smart-bluetooth-watch-phone.jpg

magic-led-time-wrist-bluetooth-bracelet-vibrating.jpg

zote zina bluetooth na zinapiga na kupokea simu pia zinatumia android
 
Sidhani kama ni mapinduzi kiivyo kama device yenyewe ni tegemezi (ie it needs a cellphone to operate)
 
Back
Top Bottom